Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 4/11 uku. 3
  • Huzuni Yenye Kulemea Sana

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Huzuni Yenye Kulemea Sana
  • Amkeni!—2011
  • Habari Zinazolingana
  • Kuwasaidia Watoto Wanaoomboleza
    Amkeni!—2012
  • Unapohisi Umechoshwa na Maisha
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu Wote)—2019
  • Mwishowe Mbegu Ilichipuka
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
  • Nifanyeje Ikiwa Ndugu Yangu Amejiua?
    Amkeni!—2008
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2011
g 4/11 uku. 3

Huzuni Yenye Kulemea Sana

Nicolle alikuwa msichana mwenye afya. Lakini jioni moja alisema kwamba anaumwa na kichwa, na wazazi wake wakampeleka hospitalini. Jioni iliyofuata, akiwa bado anapata matibabu, Nicolle alipatwa na mshtuko wa moyo. Uchunguzi zaidi ulionyesha kwamba alikuwa na maambukizo ya bakteria yasiyojulikana sana na maambukizo hayo yalikuwa yameenea kwenye mapafu, figo, na moyo wake. Katika muda wa saa 48, Nicolle alikuwa amekufa. Alikuwa na umri wa miaka mitatu tu.

KIFO cha mpendwa ni mojawapo ya mambo yenye kuumiza sana ambayo mwanadamu anaweza kukabili. Nyakati nyingine, huzuni hiyo inaweza kuwa yenye kulemea sana. “Ninamkosa sana Nicolle,” anasema Isabelle, mama ya msichana huyo. “Ninakosa kumbatio lake, harufu yake, wororo wake. Ninakosa ua alilokuwa akinipa kila siku. Mimi humfikiria Nicolle kila siku.”

Je, umefiwa na mpendwa wako—iwe ni mtoto, mwenzi wa ndoa, ndugu au dada, mzazi, au rafiki wa karibu? Ikiwa ndivyo, unaweza kukabiliana jinsi gani na huzuni yako?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki