Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 4/11 uku. 26
  • Gundi ya Mnyoo Anayeitwa Sandcastle

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Gundi ya Mnyoo Anayeitwa Sandcastle
  • Amkeni!—2011
  • Habari Zinazolingana
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2011
  • Nyungunyungu wa Gini—Siku Zake za Mwisho
    Amkeni!—1993
  • Minyoo wa Ajabu
    Amkeni!—2003
  • Uteute wa Konokono Unaonata
    Je, Ni Kazi ya Ubuni?
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2011
g 4/11 uku. 26

Je, Ni Kazi ya Ubuni?

Gundi ya Mnyoo Anayeitwa Sandcastle

● Madaktari wapasuaji huunganisha mifupa ilivyovunjika kwa kutumia pini, mabati ya aina fulani, na skrubu, lakini ni vigumu sana kutumia vifaa hivyo kuunganisha mifupa midogo. Watafiti wametatizwa kwa muda mrefu jinsi wanavyoweza kutokeza gundi inayoweza kunata ndani ya mwili wa mwanadamu ulio na umajimaji. Walipata suluhisho kwa kuchunguza mnyoo anayeitwa sandcastle!

Fikiria hili: Mnyoo huyo hujenga makao yake chini ya maji kutokana na mchanga na makombe. Kila chembe huunganishwa kwa kutumia gundi ambayo mnyoo huyo hutokeza ndani ya tezi fulani iliyo kifuani mwake. Gundi hiyo inanata kuliko gundi za kisasa zinazotengenezwa na wanadamu. Ina mchanganyiko fulani wa protini ambazo zinapounganishwa zinafanya gundi hiyo ishikamane upesi sana chini ya maji! Mnyoo huyo amesemekana kuwa mwashi stadi, na inafaa sana kwamba anaitwa hivyo. Russell Stewart, wa Chuo Kikuu cha Utah, anasema kwamba mnyama huyo mdogo amesuluhisha “tatizo tata sana kuhusu gundi.”

Watafiti wametokeza gundi kama ya mnyoo huyo ambayo inanata kwa nguvu zaidi kuliko hata ya mnyoo huyo. Gundi ambayo mwishowe itatumiwa katika upasuaji inapaswa kuwa na uwezo wa kuoza ili inapotumiwa kuunganisha mifupa iliyovunjika, iweze pia kuyeyuka mfupa unapopona. Iwapo gundi hiyo itawasaidia wanadamu, bila shaka itakuwa ugunduzi muhimu wa kitiba.

Una maoni gani? Je, gundi ya pekee ya mnyoo anayeitwa sandcastle ilijitokeza yenyewe? Au ilibuniwa?

[Picha katika ukurasa wa 26]

Watafiti wanatumaini wataweza kurekebisha mifupa iliyovunjika bila kutumia vifaa vya chuma

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 26]

Sandcastle worm: © Peter J. Bryant, University of California, Irvine

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki