Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 7/11 kur. 23-31
  • Mazungumzo ya Familia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mazungumzo ya Familia
  • Amkeni!—2011
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kuna Kasoro Gani Katika Picha Hii?
  • Kusanya na Ujifunze
  • Watu na Nchi
  • Watoto Watafute Picha
  • MAJIBU YA UKURASA WA 30 NA 31
  • Mazungumzo ya Familia
    Amkeni!—2012
  • Mazungumzo Ya Familia
    Amkeni!—2012
  • Mazungumzo Ya Familia
    Amkeni!—2012
  • Mazungumzo Ya Familia
    Amkeni!—2012
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2011
g 7/11 kur. 23-31

Mazungumzo ya Familia

Kuna Kasoro Gani Katika Picha Hii?

Soma Matendo 9:36-41. Ni mambo gani matatu katika picha hii ambayo si sahihi? Andika majibu yako kwenye mistari iliyo hapa chini, na ukamilishe picha hii kwa kuipaka rangi.

1. ․․․․․

2. ․․․․․

3. ․․․․․

ZUNGUMZENI PAMOJA:

Tabitha anajulikana kwa jina gani lingine, na majina yake yanamaanisha nini?

DOKEZO: Soma sanduku kwenye ukurasa wa 67 wa kitabu “Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu.

Je, Tabitha alikuwa mtu mwenye ubinafsi? Eleza.

DOKEZO: Soma Matendo 9:36, 39.

Maneno ya Yesu yanayopatikana katika Luka 6:38 yalithibitika kuwa ya kweli jinsi gani katika kisa cha Tabitha? Unaweza kuiga mfano wake jinsi gani?

DOKEZO: Soma Waefeso 4:28; Yakobo 2:14-17.

UTENDAJI WA FAMILIA:

Kila mshiriki wa familia na afikirie kuhusu mtu ambaye angependa kumpa zawadi. Kisha atengeneze zawadi moja rahisi kwa ajili ya mtu huyo. Kwa mfano, unaweza kutengeneza kadi, au kifaa cha kuwekea alama katika kitabu na kuandika andiko fulani la Biblia juu yake.

Kusanya na Ujifunze

Kata, kunja katikati, na uhifadhi

KADI YA BIBLIA 7 PETRO

MASWALI

A. Kwa nini Petro alianza kuzama?

B. Je, habari hii ni kweli au si kweli? Petro alibaki akiwa mseja.

C. Viongozi wa kidini walipowaamuru mitume waache kuhubiri, Petro na mitume wale wengine walijibu na kusema: “Lazima . . . ”

[Chati]

4026 K.W.K. 1 W.K. 98 W.K.

Adamu aumbwa Aliishi katika Kitabu cha

karne ya mwisho cha

ya kwanza W.K. Biblia

kinaandikwa

[Ramani]

Aliishi Bethsaida na Kapernaumu

GALILAYA

Kapernaumu

Bethsaida

Bahari ya Galilaya

PETRO

MAMBO MACHACHE KUMHUSU

Mvuvi mwenye bidii sana ambaye baadaye alikuja kuwa mmoja wa wanafunzi wa kwanza wa Yesu. Yesu alimchagua Petro awe mmoja wa mitume wake 12. Maneno ya Petro katika zile Injili nne ni mengi kuliko ya mtume mwingine yeyote. Yehova alimtumia sana katika kazi ya kuhubiri na ‘kuwatia nguvu ndugu zake.’—Luka 22:32; Marko 3:13-19.

MAJIBU

A. Alikuwa na shaka.—Mathayo 14:28-31.

B. Si kweli.—Marko 1:29-31; Yohana 1:42; 1 Wakorintho 9:5.

C. “. . . tumtii Mungu kuwa mtawala kuliko wanadamu.”—Matendo 5:18, 27-29.

Watu na Nchi

4. Jina langu ni Antonia. Nina umri wa miaka minane, na ninaishi nchini Chile, huko Amerika Kusini. Kuna Mashahidi wangapi wa Yehova nchini Chile? Ni 69,500, 96,500, au 106,500?

5. Ni alama gani inayoonyesha eneo ninaloishi? Chora duara kuzunguka alama hiyo, na uchore alama nyingine kuonyesha eneo unaloishi kisha uone kwenu ni umbali gani kutoka Chile.

A

B

C

D

Watoto Watafute Picha

Je, unaweza kupata picha hizi katika toleo hili? Kwa maneno yako mwenyewe, eleza jambo linalotendeka katika kila picha.

● Majibu ya “MAZUNGUMZO YA FAMILIA” kwenye ukurasa wa 23

MAJIBU YA UKURASA WA 30 NA 31

1. Petro hakuwa amesimama alipokuwa akisali; alipiga magoti.

2. Wanawake (wajane) walimwonyesha Petro mavazi ambayo Tabitha aliwashonea, si vyombo vya udongo.

3. Petro alisali akiwa peke yake, hakukuwa na watu wengine chumbani.

4. 69,500.

5. B.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki