Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 10/11 uku. 2
  • Ukurasa wa Pili

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ukurasa wa Pili
  • Amkeni!—2011
  • Habari Zinazolingana
  • Zoeza Mtoto Wako Tangu Utoto Mchanga Sana
    Siri ya Furaha ya Familia
  • Kulea Watoto tangu Uchanga
    Kufanya Maisha ya Jamaa Yako Yawe Yenye Furaha
  • Wazazi, Fikieni Moyo wa Mtoto Wenu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • Tafuta Mashauri Mazuri
    Amkeni!—2007
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2011
g 10/11 uku. 2

Ukurasa wa Pili

Kuwalea Watoto Wenye Kutegemeka

Huenda wazazi wasifikirie jambo moja wanapomtazama mtoto wao mpendwa ambaye ametoka tu kuzaliwa. Lakini ukweli wa mambo ni: Hatimaye mtoto huyo mchanga atakua na kuwa mtu mzima anayejitegemea. Ilikusudiwa iwe hivyo, kwa kuwa Biblia inasema kwamba “mwanamume atamwacha baba yake na mama yake.” (Mwanzo 2:24) Bila shaka, jambo hilohilo linaweza kusemwa kumhusu msichana.

Hata hivyo, wazazi wengi huwa na wasiwasi inapofika siku ya mwana au binti yao kuondoka nyumbani, na siku hiyo hutokeza hisia za furaha na pia huzuni. Wao hujiuliza, ‘Je, nimemlea mtoto wangu kwa njia inayofaa? Je, ataweza kufanya kazi kwa bidii, kutunza nyumba yake, na kuishi kulingana na mapato yake?’ Jambo muhimu hata zaidi ni, ‘Je, mtoto wangu ataishi kulingana na viwango ambavyo nimejaribu kumfundisha?’—Methali 22:6; 2 Timotheo 3:15.

Toleo hili la pekee la Amkeni! litaonyesha jinsi ambavyo mashauri ya Biblia yanaweza kuwasaidia wazazi katika kila hatua ya ukuzi wa mtoto wao.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki