Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 11/11 uku. 29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—2011
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Misiba ya Asili ya 2010
  • Je, Neanderthal Walikuwa Kama Sisi?
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—2014
  • Misiba ya Asili​—Kwa Nini Imeongezeka Sana?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Pambano la Mwanadamu Dhidi ya Misiba
    Amkeni!—1995
  • Je, Wahitaji Bima?
    Amkeni!—2001
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2011
g 11/11 uku. 29

Kuutazama Ulimwengu

Nchini Ujerumani, watoto 7 kati ya 10 tayari wanaonekana katika Intaneti. Wazazi wao huwafungulia akaunti za mawasiliano na za barua-pepe au wanapachika picha zao au zile za eksirei ya mtoto aliye tumboni. Hata hivyo, wataalamu wanatoa maonyo kuhusu jambo hilo kwa kuwa picha zinazopachikwa kwenye Intaneti zinaweza kutumiwa vibaya wakati ujao.—BABY UND FAMILIE, UJERUMANI.

Kulingana na takwimu za serikali, kila mwaka wanawake 14,000 nchini Urusi hufa kwa sababu ya jeuri wanayotendewa nyumbani.—RIA NOVOSTI, URUSI.

Theluji inayoanguka kuanzia mita 6,858 hadi mita 7,752 juu ya usawa wa bahari kwenye Mlima Everest ina kiasi kikubwa cha aseniki na kadimiamu ambayo ni hatari katika maji ya kunywa. Inasemekana kwamba uchafuzi huo umesababishwa na wanadamu.—SOIL SURVEY HORIZONS, MAREKANI.

Hivi karibuni, kampuni pekee iliyoidhinishwa kuchapisha Biblia nchini China ilichapisha nakala ya milioni 80. Kampuni hiyo huchapisha Biblia milioni 1 kila mwezi—na hiyo ni robo ya idadi ya Biblia zinazochapishwa ulimwenguni pote.—XINHUA, CHINA.

“Zaidi ya asilimia 10 ya watu wazima nchini Marekani (asilimia 10.1) wameliacha kanisa Katoliki ingawa walilelewa wakiwa Wakatoliki.”—NATIONAL CATHOLIC REPORTER, MAREKANI.

Misiba ya Asili ya 2010

Kampuni moja kubwa ya bima ilionyesha kwamba katika mwaka wa 2010 kulikuwa na misiba 950 ya asili ulimwenguni pote, idadi inayozidi wastani wa misiba 785 iliyokadiriwa kwamba ilitokea kila mwaka katika muda wa miaka kumi iliyopita. Misiba mitano mibaya zaidi kutukia ilikuwa matetemeko ya nchi huko Chile, China, na Haiti; mafuriko yaliyoikumba Pakistan; na wimbi la joto lililoipiga nchi ya Urusi, ambako makumi ya maelfu walikufa kutokana na joto na athari za uchafuzi wa hewa. Huko Ulaya kaskazini, majivu kutoka kwa mlima wa volkano huko Iceland hayakusababisha madhara mengi ya moja kwa moja lakini karibu yazuie kabisa usafiri wa ndege. Nchini Australia, dhoruba ya mvua ya mawe iliyonyesha mara mbili ilisababisha uharibifu wa zaidi ya dola bilioni 2 (za Marekani). “Kwa ujumla, hasara ya kifedha, kutia ndani hasara ambazo hazikulipiwa na bima,” linasema gazeti The Telegraph la London, “ilifikia dola bilioni 130 tofauti na hasara ya dola bilioni 50 iliyotokea mwaka uliopita.”

Je, Neanderthal Walikuwa Kama Sisi?

“Wazo ambalo limeendelezwa kwa muda mrefu kwamba Neanderthal walikuwa wanyama wa hali ya chini kwa kulinganishwa na Homo sapiens (wanadamu wa kawaida) linabadilika kwa kuwa, imeanza kuonekana kwamba walikuwa na uwezo wa kufanya mambo ambayo yalifikiriwa kuwa ni wanadamu tu wanaoweza kuyafanya,” linasema gazeti New Scientist. Uvumbuzi wa hivi karibuni unaonyesha kwamba Neanderthal walijenga makao na meko, walidhibiti moto, walivaa nguo, walipika, walitengeneza vifaa, na walitokeza gundi ya kuunganisha chuma kwenye sehemu ya mbele ya mkuki. Pia kuna uthibitisho unaoonyesha kwamba waliwatunza wagonjwa, walivalia mapambo yaliyokuwa na ishara fulani, na waliwazika wafu wao. Kulingana na Erik Trinkaus, profesa wa elimu kuhusu wanadamu (anthropology) katika Chuo Kikuu cha Washington, huko St. Louis, Missouri, Marekani, “Neanderthal walikuwa watu, na huenda walikuwa na uwezo uleule wa akili kama wetu.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki