Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 7/22 kur. 4-8
  • Pambano la Mwanadamu Dhidi ya Misiba

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pambano la Mwanadamu Dhidi ya Misiba
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mbadiliko wa Maoni Wahitajiwa
  • Kuweka Malengo
  • Mwendo Wenye Kutatiza
  • Kwa Nini Ongezeko Lote Hilo?
  • Isiyoepukika ama Ipungukayo?
  • Lile Uwezalo na Usiloweza Kufanya
  • Biblia Inasema Nini Kuhusu Misiba ya Asili?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Misiba Asilia Ipigapo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Misiba ya Asili-Je! Mungu Ndiye Huisababisha?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Misiba ya Asili​—Kwa Nini Imeongezeka Sana?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 7/22 kur. 4-8

Pambano la Mwanadamu Dhidi ya Misiba

MIAKA mitatu ilikuwa imepita, na katibu mkuu wa UM Boutros Boutros-Ghali hakuwa na furaha. “Hatujasonga kwa haraka vya kutosha,” akakiambia kikundi cha wataalamu mapema katika 1993. “Katika kuwaomba nyinyi kukutana sasa badala ya baadaye, nia yangu ilikuwa kuona kama tungeweza kulipia wakati uliokuwa umepotea.” Eti wakati uliokuwa umepotea? Ni nini kilikuwa katika akili yake? Herufi tano: IDNDR. Je, zinamaanisha nini? Na kwa nini haraka?

Mmoja wa wataalamu waliohudhuria mkutano huo alikuwa Frank Press, mwanajiofizikia na “baba” wa IDNDR. Miaka 11 iliyopita, Dakt. Press alianza kukusanya jamii ya wanasayansi ulimwenguni pote ili kuzidisha pambano layo dhidi ya misiba ya asili. Miaka mitano baadaye, katika Desemba 1989, Umoja wa Mataifa uliitikia wito wayo wa kumaliza ukimya kwa kuteua miaka ya kuanzia 1990 hadi 2000 kuwa International Decade for Natural Disaster Reduction (Mwongo wa Kimataifa Kuhusu Upunguzaji wa Misiba ya Asili), ama IDNDR. Kusudi lawo ni nini?

Mbadiliko wa Maoni Wahitajiwa

Profesa wa jiolojia wa Brazili na mshiriki wa Kamati ya Kisayansi na Kiufundi ya IDNDR, Umberto G. Cordani, aliambia Amkeni! kwamba IDNDR ni sihi kwa jamii ya kimataifa kuchangia ujuzi na rasilimali na kazi zayo pamoja katika kupunguza mteseko, uharibifu, mvurugiko, na kupotezwa kwa uhai kunakosababishwa na misiba ya asili. “Kufikia lengo hilo,” alikazia Profesa Cordani, “kunahitaji mbadilisho wa uangalifu ulimwenguni pote kutoka itikio la baada ya msiba hadi utendaji wa kabla ya msiba.”

Hata hivyo, kubadili kufikiri kwa tufeni, ni kugumu zaidi kuliko kuupa mwongo jina, kwani “wafanya-maamuzi” lataarifu UNESCO Environment and Development Briefs, “huelekea kutoa uangalifu juu ya kutoa msaada wakifutilia mbali uzuiaji.” Kwa kielelezo, kati ya fedha zote zinazotumiwa leo kwa usimamizi wa hatari za asili katika Amerika ya Kilatini, zaidi ya asilimia 90 huelekea kwa msaada wa hatari na chini ya asilimia 10 kwa uzuiaji. Iwavyo vyote, yaonelea barua-habari ya IDNDR Stop Disasters, wanasiasa “huungwa mkono zaidi kwa kufariji majeruhi wa msiba kuliko kuomba fedha kwa ajili ya hatua zisizovutia sana ambazo zingekuwa zimeepusha ama kupunguza msiba.”

Kuweka Malengo

Ili kubadili maelekeo haya ya matumizi, Umoja wa Mataifa ulifafanua malengo matatu kwa ajili ya huu mwongo. Kufikia mwaka 2000, nchi zote zapaswa kuwa zimetayarisha (1) uchanganuzi wa hatari zinazotokezwa na hatari za asili, (2) mipango ya muda mrefu ya matayarisho na uzuiaji, na (3) mifumo yao ya kutoa onyo. Kamati za kitaifa zilibuniwa ili kubadili falsafa na manuio mazuri ya IDNDR kuwa mipango thabiti, na katika Mei 1994, Japani ilikuwa mwandalizi wa Kongamano la Ulimwenguni juu ya Upunguzaji wa Misiba ya Asili lililothaminiwa na UM. Mipango hii yote ikiwa imepangwa ama katika mwendelezo, kwa nini Boutros-Ghali alikuwa haridhiki? Kwa sababu ya mwendo wenye kuvuruga.

Mwendo Wenye Kutatiza

Kwa upande mmoja, jitihada za IDNDR zinafaulu. Uelewevu wa wanasayansi kuhusu kupunguza misiba umeongezeka, na baadhi ya hatua, kama vile mifumo ya kutoa onyo iliyoboreshwa, yaokoa uhai mwingi na kupunguza hasara. Hata hivyo, licha ya mafanikio haya, aonelea Dakt. Kaarle Olavi Elo, mkurugenzi wa ukatibu wa IDNDR, “idadi na ukubwa wa misiba zaendelea kukua, zikiathiri watu zaidi na zaidi.” Tumeona “ongezeko mara tatu kuanzia miaka ya 1960 hadi miaka ya 1980,” ahakikisha mtaalamu mwingine wa UM, “na mpando mkuu wa ziada katika miaka ya 1990.” Hakika, katika 1991, misiba mikuu 434 iliua watu 162,000 ulimwenguni pote, na katika 1992, hasara zilipita dola bilioni 62 (za Marekani). Ulimwengu, amalizia James G. Speth msimamizi wa UNDP (Programu ya Usitawishaji ya Umoja wa Mataifa), umekuja kuwa “mtambo wa msiba, ukitokeza masaibu kwa ukawaida yenye kuhuzunisha.” (UNDP Update, Novemba 1993) Ni nini kinachosababisha mwendo huu wenye kuvuruga?

Kwa Nini Ongezeko Lote Hilo?

Ili kujibu, kwanza ona tofauti kati ya hatari ya asili na msiba wa asili. Ile ya kwanza ni tukio la asili—kama lile furiko ama tetemeko la dunia—ambalo lina uwezo wa kuwa msiba lakini sikuzote haliwi hivyo. Mathalani, mafuriko katika jaruba lisilokaliwa na watu la Amazon ya Brazili ni matukio ya asili yanayofanya madhara madogo. Hata hivyo, mafuriko yapigayo Bangladesh katika delta yake ya mto Ganges iliyo na watu wengi husababisha hasara zilizoenea za binadamu, mali, na mazingira. Mara nyingi hasara kama hizo hutokeza misiba mikubwa hivi kwamba jamii zilizofikwa haziwezi kumudu bila msaada kutoka nje. Katika kisa hicho, hatari ya asili imekuja kuwa msiba wa asili. Hata hivyo, kwa nini migongano hii yenye kutokeza msiba kati ya mwanadamu na asili inaongezeka?

Mtaalamu wa misiba James P. Bruce aonelea kwamba “mwendo fulani uelekeao kwenye hatari kali na za kawaida zaidi” huenda ukawa “kisababishi kichangiacho.” Hata hivyo, yeye pamoja na wanasayansi wengine wakubaliana kwamba kisababishi kikuu katika misiba si ongezeko la hatari za asili bali ongezeko katika kuhatarishwa kwa mwanadamu na hatari hizi. Kuhatarishwa huku kulikoongezeka, gazeti la World Health lataja, kwasababishwa na “mchanganyiko wa idadi ya watu, ikolojia na hali za kitekinolojia.” Ni vipi baadhi ya vijenzi vya mchanganyo huu wenye kuchochea msiba?

Kijenzi kimoja ni idadi ya watu yenye kupanuka ulimwenguni. Kiasi cha familia ya binadamu chaendelea kukua, uwezekano wa kwamba hatari za asili zitapata baadhi ya watu bilioni 5.6 wa ulimwengu katika kijia chacho unazidi kukua pia. Isitoshe, msongo wa idadi ya watu huendelea kulazimisha mamilioni ya watu walio maskini kukaa katika majengo yasiyo salama katika maeneo yaliyo hatari kupata mashambulio ya kawaida kutokana na hatari za asili. Matokeo hayashangazi: Tangu 1960, idadi ya watu ulimwenguni imerudufika, lakini hasara kutokana na msiba zimeongezeka kwa yapata mara kumi hivi!

Mabadiliko ya kimazingira yaongezea kwa matatizo. Kutoka Nepal hadi Amazon na kutoka nyanda za chini za Amerika ya Kaskazini hadi visiwa vya Pasifiki, mwanadamu anazidi kufyeka misitu, kulima ardhi kupita kiasi, kuharibu miamba ya pwani, na kuacha kijia cha alama za miguu za kimazingira—lakini si bila kulipia. “Tunapokazia uwezo wa kustahimili wa mazingira yetu na kurekebisha tabia yayo,” asema aliyekuwa mkurugenzi wa IDNDR, Robert Hamilton, “ndivyo kulivyo na uwezekano mkubwa zaidi kwamba hatari ya asili huenda ikaja kuwa msiba.”

Hata hivyo, ikiwa utendaji wa mwanadamu unachangia mitokeo ya misiba katika vichwa vikuu vya habari leo, basi kinyume kingekuwa kweli pia: Kwa kuchukua hatua za kuzuia, mwanadamu anaweza kubadili vichwa vikuu vya habari vya kesho. Kifo na uharibifu vyaweza kupunguzwa. Kwa kielelezo, asilimia 90 ya vifo kutokana na matetemeko ya ardhi, asema mtaalamu, vinaweza kuepukwa. Hata hivyo, ingawa yale mawazo ya kuzuia ni yenye nguvu, watu wengi huendelea kuiona misiba kama isiyoepukika. Oni hili la majaliwa, laripoti UNESCO Environment and Development Briefs, ndicho “kizuizi pekee kikubwa kuliko vyote vya kupunguza misiba.” Wewe uko upande upi wa kizuizi hicho?

Isiyoepukika ama Ipungukayo?

Hasa katika ulimwengu unaositawi, hisia hii ya kukata tamaa imeenea sana—na si ajabu! Kati ya watu wote waliouawa na misiba ya asili wakati wa miaka 50 iliyopita, asilimia 97 waliishi katika ulimwengu unaositawi! Katika baadhi ya nchi hizi, likaonelea Stop Disasters, “ile idadi ya misiba iko juu sana hivi kwamba ni vigumu kubainisha kati ya mwisho wa msiba mmoja na mwanzo wa mwingine.” Kwa kweli, asilimia 95 ya misiba yote hutukia katika ulimwengu unaositawi. Ongezea juu ya hili mifululizo isiyomalizika ya misiba ya kibinafsi—umaskini, kukosa kazi, hali mbaya za kuishi—nawe waweza kuona kwa nini kukata tamaa hukumba maskini kama wimbi lizukalo. Wao hukubali hasara zilizosababishwa na misiba iliyojirudia-rudia kama zenye kuhuzunisha lakini kuwa majaliwa ya maisha. Hata hivyo, je, hasara hizi ni zisizoepukika?

Lile Uwezalo na Usiloweza Kufanya

Kweli, huwezi kudhibiti ukawaida au kiasi cha hatari za asili, lakini hilo halikufanyi ukate tamaa kabisa. Unaweza kupunguza kuhatarishwa kwako kwa matukio haya. Jinsi gani? Ebu fikiria ulinganisho huu.

Tuseme mtu fulani anataka kupunguza kuhatarishwa kwake kwa jua (tukio la asili) ili kuzuia kupatwa na kansa ya ngozi (msiba). Ni hatua gani anayoweza kuchukua? Ni wazi, hawezi kudhibiti kuzuka na kutua kwa jua (ukawaida wa tukio). Wala hawezi kupunguza kiwango cha miale inayofikia mazingira yake (kiasi cha hilo tukio). Lakini je, hilo lamfanya mtu huyo akate tamaa? La, anaweza kupunguza kujihatarisha kwa jua. Mathalani, anaweza kukaa chumbani wakati wa siku jua liwakapo sana, au ikiwa hilo haliwezekani, anaweza kuvaa kofia na vazi lenye kukinga anapokuwa nje. Jambo hili linaongeza ulinzi wake dhidi ya jua (tukio) na hupunguza uwezekano wake kuwa mgonjwa wa kansa ya ngozi (msiba). Matendo yake ya kujizuia yanaweza kufanyiza tofauti!

Vivyo hivyo, wewe pia unaweza kuchukua hatua ambazo huongeza ulinzi wako dhidi ya matokeo ya baadhi ya hatari za asili. Kwa njia hiyo, utapunguza ujihatarishaji na hasara msiba upigapo. Kwa wale wanaoishi katika ulimwengu uliositawi, yale madokezo katika sanduku “Je, Wewe Uko Tayari?” huenda yawe yenye manufaa. Ikiwa unaishi katika ulimwengu unaositawi, vile vielelezo katika sanduku “Viboresho vya Gharama ya Chini Vinavyofanya Kazi” huenda vikupe wazo fulani la aina ya hatua sahili zinazopatikana sasa. Huenda viwe vyenye manufaa katika kuokoa uhai mwingi na kupunguza hasara. Kukiwa na tekinolojia inayopatikana leo, hili humkumbusha mwanajiofizikia Frank Press, “kujaliwa hakukubaliwi tena kamwe.” Bila shaka, inapohusu misiba ya asili, kwa hakika kuzuia ni bora kuliko kuponya.

[Sanduku katika ukurasa wa 6]

Je, Wewe Uko Tayari?

Shirika la U.S. Federal Emergency Management Agency lapendekeza idadi kadhaa ya njia za kukabiliana na hatari. Yafuatayo ni baadhi ya mambo makuu.

Pata habari. Wasiliana na ofisi ya mahali penu ya usimamizi wa dharura na ujue ni msiba upi ambao ungeweza kufika jumuiya yako. Huenda ukawa na habari kuhusu baadhi yayo, lakini mingine huenda ikupate bila kutazamia. Ukijua kwamba nyumba yako imehatarishwa na hatari za asili:

◻ Kutana na familia yako na mzungumze aina za hatari ambazo zingeweza kuwahatarisha nyinyi. Eleza jambo la kufanya katika kila kisa.

◻ Panga jinsi familia yako itadumisha uwasiliano kati ya mmoja na mwingine ikiwa mtatenganishwa na tukio kama hilo. Chagua mahali pawili kwa kukutana: pamoja pawe nje ya nyumba yenu iwapo kuna dharura ya ghafula, kama vile moto, na pengine nje ya ujirani wenu iwapo hamwezi kurudi nyumbani.

◻ Mwombe rafiki mmoja kuwa mwasiliani wa familia yako ikiwa hamwezi kufika mahali mlipopanga, washiriki wote wa familia wanaweza kupigia simu mwasiliani huyo na kueleza mahali walipo. Chagua rafiki ambaye anaishi mbali na eneo lenu kwa sababu baada ya msiba ni rahisi kupiga simu mbali kuliko kupiga simu mnamo eneo lililoathiriwa. Wafunze watoto jinsi ya kumpigia simu rafiki huyo. Zungumza jambo la kufanya inapokuwa ni lazima kuachana. Fikiria jinsi ungewasaidia jirani zako ambao huenda wakahitaji msaada maalumu. Panga jinsi ya kushughulikia wanyama wa kufugwa wako.

◻ Bandika nambari za simu za dharura kwa kila simu.

◻ Onyesha mahali kisanduku kikuu cha umeme kilipo, tangi la maji, mahali bomba la gesi ya asili lilipo. Onyesha washiriki wa familia wenye kuchukua madaraka jinsi na wakati wa kuzima hizi, na uweke vifaa vihitajiwavyo karibu na swichi kuu.

◻ Jitayarishe kwa ajili ya moto. Weka kidadisi moshi, hasa karibu na vyumba vya kulala.

[Sanduku katika ukurasa wa 8]

Viboresho vya Gharama ya Chini Vinavyofanya Kazi

KARIBU chini ya nusu ya idadi ya watu ulimwenguni, yaripoti Benki ya Dunia, hujimudu kwa dola tano kwa juma ama hata chini ya hizo. Hata ikiwa uko katika hali hiyo, wasema wataalamu, kuna hatua zilizothibitishwa ambazo unaweza kutumia. Jifunze kuzihusu, kwa sababu elimu, akazia Alberto Giesecke mtaalamu wa misiba ya Peru, “ni ufunguo wa hatua za gharama za chini ya kupunguza athari za misiba ya asili.” Kuna vielelezo viwili kutoka Amerika Kusini:

Kile kitabu cha mwongozo Mitigating Natural Disasters cha UM chaeleza linaloweza kufanywa ili kujenga nyumba bora za matofali, ama udongo:

◻ Katika halinchi yenye milima-milima, chimba ardhi ili kufanyiza mahali pa mkao wa nyumba.

◻ Nyumba za mraba ni zenye nguvu zaidi; ukitaka jengo la pembe nne mraba, jenga ukuta mmoja ukiwa na urefu mara mbili na nusu kuliko ule mwingine.

◻ Tumia misingi ya mwamba ama saruji ili kupunguza kani za mtetemeko.

◻ Jenga kuta zilizo sambamba zikiwa na uzito, nguvu, na urefu sawia. Ziweke zikiwa nyembamba na chini. Nyumba zilizojengwa kwa njia hii hutokeza uharibifu mdogo wakati wa tetemeko la dunia kuliko nyumba za udongo zilizo za wastani.

Ujenzi wa kitamaduni fito zilizoingiliana (quincha) ni ufundi mwingine uliothibitishwa. Nyumba za quincha, chasema Stop Disasters, zina viunzi vya mafunjo yaliyofumwa kwa vitawi vidogo vilivyotegemezwa kwa nguzo zilizolala na kusimama na kiasi kidogo cha udongo. Jengo la aina hii, lenye kuta zenye unene wa sentimeta 10 hadi 15, huruhusu nyumba itikisike wakati wa tetemeko la dunia, na tetemeko linapokoma, majengo hujirekebisha kurudia hali zayo za awali tena. Tetemeko la dunia lilipopiga katika 1991, nyumba kama hizo zilibaki zikiwa zimesimama ilhali nyumba nyinginezo 10,000, zenye kuta thabiti za unene wa meta moja, ziliangushwa, zikiua watu 35. Kulingana John Beynon stadi wa majengo wa UNESCO, matetemeko ya dunia hayaui watu; majengo yanayoporomoka hufanya hivyo.

[Picha katika ukurasa wa 7]

Katika maeneo mengine, mwanadamu anafyeka misitu bila kujali, ikifungulia njia misiba ya asili zaidi

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki