Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w96 12/1 kur. 2-4
  • Misiba Asilia Ipigapo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Misiba Asilia Ipigapo
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Biblia Inasema Nini Kuhusu Misiba ya Asili?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Misiba ya Asili​—Kwa Nini Imeongezeka Sana?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Pambano la Mwanadamu Dhidi ya Misiba
    Amkeni!—1995
  • Misiba ya Asili-Je! Mungu Ndiye Huisababisha?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
w96 12/1 kur. 2-4

Misiba Asilia Ipigapo

Accra, Ghana, Julai 4, 1995: Mvua kubwa zaidi katika karibu miaka 60 ilisababisha mafuriko makubwa. Watu wapatao 200,000 walipoteza kila kitu, 500,000 walipoteza njia ya kufikia nyumba zao, na 22 walipoteza uhai wao.

San Angelo, Texas, Marekani, Mei 28, 1995: Pepo za chamchela na mvua ya mawe ziliuharibu mji huo wa wakazi 90,000, zikisababisha madhara yakadiriwayo kugharimu dola za Marekani milioni 120.

Kobe, Japani, Januari 17, 1995: Tetemeko la dunia lililodumu sekunde 20 tu liliacha maelfu ya watu wakiwa wamekufa, makumi ya maelfu wakiwa wamejeruhiwa, na mamia ya maelfu wakiwa bila makao.

SISI twaishi katika ule uwezao kuitwa muhula wa misiba. Ripoti ya Umoja wa Mataifa yafunua kwamba katika kile kipindi cha miaka 30 kuanzia 1963 hadi 1992, idadi ya watu waliouawa, kujeruhiwa, au kupotezewa makao na misiba, iliongezeka wastani wa asilimia 6 kila mwaka. Hali hiyo isiyo na tumaini imesababisha UM kuchagua miaka ya 1990 kuwa “Mwongo wa Kimataifa wa Kupunguza Misiba Asilia.”

Bila shaka, kani ya asili—kama vile dhoruba, mlipuko wa volkeno, au tetemeko la dunia—haileti msiba sikuzote. Mamia hutukia kila mwaka bila madhara kwa wanadamu. Lakini gharama kubwa ya uhai na mali inapohusishwa, kwa kufaa yaitwa msiba.

Ongezeko la misiba asilia laonekana kuwa lisiloepukika. Kitabu Natural Disasters—Acts of God or Acts of Man? chasema hivi: “Watu wanabadili mazingira yao na kuyafanya hivyo huyafanya yaelekee zaidi kukumbwa na misiba, nao wanatenda kwa kujifanya waelekee zaidi kupatwa na hatari hizo.” Kitabu hicho chatoa kielelezo hiki cha kukisiwa: “Tetemeko dogo la dunia katika mji wenye vibanda vilivyojengwa kwa matofali mazito ya matope kandokando ya bonde lenye mwinuko wa ghafula laweza kuthibitika kuwa msiba kwa habari ya vifo na kuteseka kwa kibinadamu. Lakini je, msiba huo ni tokeo hasa la mishtuko ya dunia au ni la lile jambo la hakika kwamba watu wanaishi katika nyumba hatari na kwenye eneo hatari?”

Kwa wanafunzi wa Biblia, bado kuna sababu nyingine inayofanya ongezeko katika misiba asilia lisiwe lenye kushangaza. Karibu miaka 2,000 iliyopita, Yesu Kristo alitabiri kwamba “umalizio wa mfumo wa mambo” ungetiwa alama na, kati ya mambo mengine, “njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali.” (Mathayo 24:3, 6-8, linganisha NW.) Biblia ilitabiri pia kwamba wakati wa “siku za mwisho” watu wangekuwa wenye kujipenda wenyewe, wapenda-fedha, wasio na shauku ya kiasili, na wasio na upendo wa wema.a (2 Timotheo 3:1-5) Vitabia hivyo mara nyingi humfanya mwanadamu atende dhidi ya mazingira yake, akifanya wanadamu waelekee zaidi kuathiriwa na kani za asili. Misiba iliyofanyizwa na mwanadamu ni tokeo pia la jamii isiyo na upendo ambamo walio wengi wanalazimika kuishi.

Sayari yetu izidipo kujawa na watu, tabia ya kibinadamu izidipo kuwaweka watu katika hatari kubwa zaidi, na mali za dunia zizidipo kutumiwa vibaya kwa kuongezeka, misiba itaendelea kuwapiga wanadamu. Kuandaa kitulizo hutokeza magumu, kama makala ifuatayo itakavyoonyesha.

[Maelezo ya Chini]

a Kwa habari zaidi juu ya ishara ya siku za mwisho, ona kitabu Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele, kurasa 98-107, kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]

Juu: Idara ya Utumishi wa Habari, Ghana; kulia: San Angelo Standard-Times

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 2]

COVER: Maxie Roberts/Courtesy of THE STATE

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki