Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 10/12 uku. 6
  • Tunza Afya Yako

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Tunza Afya Yako
  • Amkeni!—2012
  • Habari Zinazolingana
  • Ni Nini Kitakachonichochea Kufanya Mazoezi?
    Vijana Huuliza
  • Kwa Nini Nitunze Afya Yangu?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 1
  • Kwa Nini Nitunze Afya Yangu?
    Amkeni!—2010
  • Njia ya 3—Fanya Mazoezi
    Amkeni!—2011
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2012
g 10/12 uku. 6

Tunza Afya Yako

Kutunza afya yako kunaweza kuboresha utendaji wako shuleni na pia kuboresha maisha yako.

NI JAMBO linalopatana na akili kutunza mwili ambao Mungu alikupa. (Zaburi 139:14) Kwa mfano: Wazia kwamba una gari, lakini hulitunzi. Muda si muda, gari hilo litaharibika. Jambo hilohilo linaweza kutukia kwa mwili wako. Mwili wako unahitaji utunzaji wa aina gani?

[Picha katika ukurasa wa 6]

Pumzika.

Kukosa kulala vya kutosha kunaweza kukufanya uonekane mnyonge, ujihisi mchovu, umechanganyikiwa, na hata umeshuka moyo. Tofauti na hilo, unapopumzika vya kutosha, unakuwa na nguvu nyingi. Pia kupumzika vya kutosha kunaweza kufanya ukue haraka, uboreshe utendaji wa ubongo wako, uimarishe mfumo wako wa kinga, na uboreshe hali yako ya kihisia. Bila shaka, utapata faida nyingi kwa kufanya jambo hilo linalohitaji jitihada ndogo tu!

Dokezo: Ikiwezekana, jaribu kulala saa zilezile kila usiku.

[Picha katika ukurasa wa 6]

Vyakula.

Vijana hukua haraka. Kwa mfano, katika kipindi cha kati ya umri wa miaka 10 na 17, uzito wa mwili wa wavulana wengi huongezeka maradufu. Wasichana pia hukua haraka katika kipindi hicho. Miili inayokua inahitaji chakula kingi chenye lishe na kinachoupa mwili nguvu. Hakikisha kwamba unakula vizuri.

Dokezo: Usikose kula kiamsha-kinywa. Kula kiamsha-kinywa kabla ya kwenda shule kunaweza kukusaidia ukaze fikira zaidi na kuboresha kumbukumbu yako.

[Picha katika ukurasa wa 6]

Mazoezi.

Biblia inakubali kwamba “mazoezi ya mwili yana faida.” (1 Timotheo 4:8, Biblia Habari Njema) Yanaweza kuimarisha misuli na mifupa, kufanya uwe na nguvu, kudhibiti uzito wako, kuongeza uwezo wako wa akili, kuboresha mfumo wako wa kinga, kupunguza mkazo, na kuboresha hali yako ya kihisia. Bila shaka, kufanya mazoezi kunaweza kufurahisha kwa kuwa unaweza kutia ndani utendaji ambao wewe hufurahia!

Jambo kuu: Kulala vya kutosha, kula vyakula vyenye lishe, na kufanya mazoezi ya kiasi kutasaidia mwili wako ufanye kazi inavyofaa. Na hilo litaboresha utendaji wako darasani.a

Anza sasa! Panga ratiba inayofaa ya kufanya mazoezi. Chunguza mazoea yako ya kulala na ya kula kwa mwezi mmoja kisha uone mahali unapohitaji kufanya marekebisho.

“Ninapofanya mazoezi ya kutembea, mimi hupata nguvu zaidi—hata kama nilikuwa mchovu nilipoanza mazoezi.”​—Jason, New Zealand.

“Mimi ninafikiri kwamba Mungu aliumba chakula kiwe kama petroli kwa miili yetu, nami ninataka kutia petroli bora zaidi katika mwili wangu!”​—Jill, Marekani.

“Mimi hufanya mazoezi ya kukimbia mara tatu kwa juma, na ninafanya mazoezi ya kuendesha baiskeli au kutembea mara mbili kwa juma. Mazoezi hunipa nguvu zaidi na kupunguza mkazo.”​—Grace, Australia.

a Kwa habari zaidi kuhusu afya yako, ona sura ya 10 ya kitabu Maswali Ambayo Vijana Huuliza​—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 1, kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki