Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 12/12 kur. 19-21
  • Caucasus “Mlima Wenye Lugha Nyingi”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Caucasus “Mlima Wenye Lugha Nyingi”
  • Amkeni!—2012
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Unamna-namna Wenye Kushangaza
  • Kukabiliana na Mafuriko Huko Caucasus
    Amkeni!—2003
  • Watu “Kutoka Katika Lugha Zote” Wanasikia Habari Njema
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Lugha ya Watu Wote
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
  • Lugha—Viunganishi na Vizuizi vya Mawasiliano
    Amkeni!—2000
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2012
g 12/12 kur. 19-21
[Picture katika ukurasa wa 20]

Caucasus “Mlima Wenye Lugha Nyingi”

HEBU wazia unajikuta katika eneo lenye milima mingi lililo na ukubwa unaokaribia kulingana na nchi ya Hispania. Unagundua kuwa eneo hilo lina mataifa mengi, na kila taifa lina lugha yake. Katika baadhi ya maeneo, hata watu wanaoishi katika vijiji jirani hawaelewi lugha ya wenzao! Hata wanajiografia wa enzi za kati walishangazwa pia, hivi kwamba mmoja wao akalifafanua eneo la Caucasus kuwa “mlima wenye lugha nyingi.”

Eneo la Caucasus liko kati ya Bahari Nyeusi na Bahari ya Kaspiani, na kwa sababu hiyo liko kati ya mabara mawili na ustaarabu mbalimbali jambo ambalo limesaidia eneo hilo kuwa na aina mbalimbali za utamaduni na historia ndefu. Watu wa eneo hilo wanajulikana kwa kuheshimu watu wenye umri mkubwa, kupenda kucheza dansi, na kwa ukarimu wao. Lakini jambo linalowastaajabisha zaidi wageni ni unamna-namna wa vikundi vya kikabila na lugha—kwa kweli eneo hilo lina lugha nyingi zaidi kuliko maeneo yote ya Ulaya yenye ukubwa unaolingana nalo.

Unamna-namna Wenye Kushangaza

[Picture katika ukurasa wa 20, 21]

Katika karne ya tano K.W.K., mwanahistoria Mgiriki Herodoto aliandika hivi: “Watu wa mataifa mbalimbali wanaishi katika eneo la Caucasus.” Karibu mwanzoni mwa karne ya kwanza W.K., mwanafalsafa mwingine Mgiriki anayeitwa Strabo aliandika kuhusu makabila 70 ya eneo hilo. Kila kabila lilikuwa na lugha yake, na yote yalikuja kufanya biashara katika jiji la Dioscurias, eneo ambalo sasa kuna jiji la kisasa la Sukhumi, kwenye pwani ya Bahari Nyeusi. Miaka mingi baadaye, Plini Mkubwa, aliyekuwa msomi Mroma, aliandika kwamba Waroma walihitaji watafsiri wapatao 130 ili waweze kufanya biashara katika jiji la Dioscurias.

Leo bado kuna zaidi ya vikundi 50 vya makabila ambavyo vinaishi katika eneo la Caucasus. Kila kikundi kina desturi zake na mara nyingi kila kikundi kina aina yake yenyewe ya mavazi, sanaa, na ujenzi. Kuna angalau lugha 37 za kiasili katika eneo hilo, na baadhi ya lugha hizo zinazungumzwa na mamilioni ya watu, lakini nyingine zinazungumzwa katika vijiji fulani tu. Jamhuri ya Dagestan iliyo upande wa Urusi ndilo eneo lenye lugha nyingi zaidi, kwani karibu makabila 30 yanaishi katika eneo hilo. Mpaka sasa wataalamu wa lugha hawajui jinsi lugha hizo zinavyohusiana wala jinsi zilivyotokea.

[Picture katika ukurasa wa 21]
Picha katika ukurasa wa 21]

Mashahidi wa Yehova wakifundisha Biblia katika eneo la Caucasus

Je, ungependa kuona jinsi maandishi ya eneo la Caucasus yalivyo? Tovuti rasmi ya Mashahidi wa Yehova,www.jw.org/sw, ina machapisho ya lugha zaidi ya 400. Miongoni mwa lugha hizo kuna lugha kadhaa ambazo huzungumzwa katika eneo la Caucasus, eneo lenye kuvutia ambalo kwa kufaa linaitwa “mlima wenye lugha nyingi.”

[Picture katika ukurasa wa 19]

LUGHA ZENYE HERUFI NYINGI NA MATAMSHI MENGI

Lugha za eneo la Caucasus zina maandishi ya aina mbalimbali. Lugha za Kiarmenia na Kigeorgia zina alfabeti za pekee. Lugha zile nyingine zinatumia mfumo wa herufi za Kisirili au alfabeti za Kilatini zilizobadilishwa.

Lugha za eneo la kaskazini-magharibi mwa Caucasus zina konsonanti nyingi zaidi kuliko lugha zozote ulimwenguni, na vokali chache. Ensaiklopidia moja inasema kwamba lugha hizo hutumia konsonanti “ambazo lazima mtu atendeshe kila sehemu ya mdomo na koo lake ili azitamke.” Inasemekana kwamba lugha ya Ubykh, ambayo mwenyeji wa mwisho alikufa katika mwaka 1992, ina angalau konsonanti 80 na labda vokali mbili tu.

Hekaya moja inasimulia kuhusu msomi aliyetumwa na sultani wa Uturuki kwenda kwenye eneo la Caucasus ili akajifunze lugha ya Ubykh. Aliporudi, ili afaulu kumweleza sultani sababu iliyofanya ashindwe kujifunza lugha hiyo, msomi huyo alichukua mkoba uliojaa mawe madogo ya mviringo na kuyamwaga kwenye sakafu ya marumaru mbele ya sultani. Kisha akamwambia: “Sikiliza sauti hizi. Ni vigumu kwa wageni kutambua matamshi ya lugha ya Ubykh sawa na ilivyo vigumu kuelewa sauti inayotolewa na mawe haya.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki