Baada ya kubeba mimba kwa miezi miwili hivi, kwa kawaida sand cat huzaa watoto watatu
KATIKATI kabisa mwa jangwa, paka anayeitwa sand cat (yaani paka anayeishi mchangani) anatoka kwenye pango lake usiku wa manane kisha anasimama. Anatazama huku na huku na kusikiliza. Kisha, akiwa amechutama, anaanza kutembea kwenye mchanga kimyakimya.
Kwa ghafula, paka huyo anamrukia na kumkamata bukunyika anayeitwa gerbil. Baadaye, anaendelea kuwinda usiku wote huku akiruka hewani mara kwa mara ili kuwakamata wanyama wengine. Akishindwa kumaliza kula windo lake, paka huyo atafukia nyama inayosalia mchangani. Kisha anarudi kwenye pango lake mapema asubuhi na ni vigumu sana kumwona wakati wa mchana. Fikiria mambo fulani yenye kupendeza kuhusu mnyama huyo asiyeonekana kwa urahisi: