Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 2/14 uku. 16
  • Taa ya Kimulimuli Anayeitwa Photuris

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Taa ya Kimulimuli Anayeitwa Photuris
  • Amkeni!—2014
  • Habari Zinazolingana
  • Mwangaza wa Kimulimuli Usio na Joto
    Amkeni!—2010
  • “Mwangaza Kamili”
    Amkeni!—2002
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2014
  • Mabawa ya Kipepeo
    Amkeni!—2014
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2014
g 2/14 uku. 16
A Photuris firefly

JE, NI KAZI YA UBUNI?

Taa ya Kimulimuli Anayeitwa Photuris

TAA, au kiungo kinachotoa mwangaza cha kimulimuli anayeitwa Photuris kimefunikwa na magamba yaliyochongoka ambayo hufanya mwangaza unaotokezwa na mdudu huyo ung’ae zaidi.a

Misfit scales

Jagged scales

Fikiria hili: Watafiti wamegundua kwamba viungo vya kutoa mwangaza vya jamii fulani za vimulimuli hao vimefunikwa kwa magamba madogo yenye mikunjo iliyolaliana kama vigae au mbao zilizoezeka nyumba. Magamba hayo yameinuka kidogo sana upande mmoja, mwinuko mdogo kuliko upana wa unywele wa mwanadamu. Lakini, mwinuko huo mdogo hufanya taa hiyo ing’ae kwa asilimia 50 zaidi kuliko kama magamba hayo yangepangwa bila kuinuka.

Je, muundo kama huo unaweza kutumiwa kuboresha mwangaza wa balbu zinazotumiwa katika vifaa vya kielektroniki? Ili kuchunguza hilo, wanasayansi walifunika balbu kwa kitu kilicho na mikunjo kama taa ya kimulimuli. Matokeo yalikuwa nini? Balbu hizo ziliangaza kwa karibu mara mbili zaidi! Mwanafizikia Annick Bay anasema: “Jambo muhimu linalotokana na utafiti huo ni kwamba tunajifunza mengi kwa kuchunguza viumbe kwa makini.”

Una maoni gani? Je, taa ya kimulimuli anayeitwa Photuris ilijitokeza yenyewe? Au ilibuniwa?

a Wanasayansi hawajachunguza jamii zote za kimulimuli huyo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki