Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 4/14 uku. 16
  • Mabawa ya Kipepeo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mabawa ya Kipepeo
  • Amkeni!—2014
  • Habari Zinazolingana
  • Sehemu ya Juu ya Bawa la Kipepeo
    Amkeni!—2012
  • Bawa la Kipepeo Linalofyonza Mwangaza
    Amkeni!—2014
  • Umbo la V la Kipepeo Anayeitwa Cabbage White
    Je, Ni Kazi ya Ubuni?
  • Masomo Yangu ya Biblia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2014
g 4/14 uku. 16
Kipepeo aina ya Blue Morpho

JE, NI KAZI YA UBUNI?

Mabawa ya Kipepeo

MABAWA ya kipepeo ni mepesi sana hivi kwamba yakipatwa na vumbi au unyevunyevu anaweza kushindwa kuruka. Hata hivyo, mabawa yake hubaki safi na makavu wakati wote. Kwa nini?

Magamba yaliyolaliana kwenye bawa la kipepeo

Bawa la kipepeo lina magamba madogo yaliyolaliana

Fikiria hili: Watafiti kwenye Chuo Kikuu cha Ohio, waliomchunguza kipepeo aina ya Giant Blue Morpho (Morpho didius) wamegundua kwamba ingawa bawa lake huonekana kuwa limelainika, kwa kweli lina magamba madogo yaliyolaliana kama vigae vilivyoezeka nyumba. Mpangilio wa magamba hayo hufanya iwe vigumu kwa vumbi au matone ya maji kukwama kwenye bawa. Wahandisi wanajaribu kuiga muundo wa bawa la kipepeo ili kubuni vifaa vitakavyotumiwa viwandani au hospitalini ambavyo havishiki maji au uchafu.

Bawa la kipepeo linaonyesha jinsi wanasayansi wanavyojaribu kuiga muundo wa viumbe hai. Mtafiti Bharat Bhushan anasema hivi: “Viumbe wa asili wamebuniwa kwa njia ya kustaajabisha, kuanzia viumbe wadogo hadi wakubwa, wana miundo ambayo imewashangaza wanadamu kwa miaka mingi.”

Una maoni gani? Je, bawa la kipepeo lilibuniwa? Au lilijitokeza lenyewe?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki