Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 3/14 kur. 12-13
  • Machozi Yako ya Ajabu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Machozi Yako ya Ajabu
  • Amkeni!—2014
  • Habari Zinazolingana
  • Mbona Machozi Yote Hayo?
    Amkeni!—1998
  • Masomo Tunayojifunza Kutokana na Machozi ya Yesu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2022
  • Machozi Yako Yana Thamani kwa Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2024
  • “Tazama! Ninafanya Vitu Vyote Kuwa Vipya”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2014
g 3/14 kur. 12-13
Mwanamume akitokwa na machozi

Machozi Yako ya Ajabu

KILIO huambatana nasi kuanzia siku tunayozaliwa. Mtaalamu mmoja anaeleza kwamba kwa watoto wachanga, uhai wao hutegemea kilio kwa kuwa wao hulia ili kupata mahitaji ya kimwili na ya kihisia. Lakini, kwa nini tunaendelea kulia hata tunapokuwa watu wazima?

Tunatokwa na machozi ya hisia kwa sababu mbalimbali. Tunaweza kulia kwa sababu ya huzuni, kuchanganyikiwa, na mateso ya kimwili au ya kiakili. Lakini pia msisimko, kitulizo, na mafanikio hutufanya tutoe machozi ya hisia, hayo huitwa machozi ya furaha. Machozi pia huambukiza. María anasema: “Nikiona mtu akilia, hata kama sijui sababu, mimi pia hutokwa na machozi.” Labda hata hadithi za kutungwa kwenye sinema au vitabu zimekufanya ulie.

Msichana akilia, mtoto akilia, na mwanamke akilia

Vyovyote vile, kulia ni lugha kubwa isiyo na maneno. Kitabu kimoja kuhusu kulia (Adult Crying) kinaeleza: “Kulia ni moja kati ya njia chache za kusema mengi katika muda mfupi.” Machozi hutuchochea kutenda. Kwa mfano, wengi wetu hatuwezi kupuuza tunapoona mtu akitokwa na machozi ya huzuni kwani yanatuambia kwamba mtu huyo anateseka. Hivyo, tunaweza kuitikia kwa kumfariji au kumsaidia mtu anayelia.

Wataalamu fulani wanaamini kulia ni njia nzuri ya kutoa yaliyo moyoni na tukizoea kuepuka kulia tunaweza kudhuru afya zetu. Wengine wanabisha, wakidai kwamba faida za kimwili au za kiakili za kulia bado hazijathibitishwa kisayansi. Hata hivyo, utafiti unaonyesha kwamba asilimia 85 ya wanawake na asilimia 73 ya wanaume huhisi vizuri baada ya kulia. Noemí anasema: “Kuna wakati najua nahitaji kulia, ili niweze kutulia na kuona mambo kwa njia nzuri zaidi.”

Utafiti unaonyesha kwamba asilimia 85 ya wanawake na asilimia 73 ya wanaume huhisi vizuri baada ya kulia

Lakini hisia hii ya kupata nafuu haisababishwi tu na machozi tunayotoa. Jinsi watu wanavyoitikia wanapotuona tukilia pia huchangia hali hiyo. Kwa mfano, machozi yetu yanapowachochea wengine kutufariji na kutusaidia, tunapata nafuu. Lakini wakitupuuza, basi tunaweza kuhisi aibu au hata kuhisi hatupendwi.

Kwa kweli, bado kilio ni fumbo. Tunachojua kwa uhakika ni kwamba kulia ni moja ya njia za ajabu ambazo Mungu ametupa ili tuonyeshe hisia zetu.

JE, WAJUA?

Kwa kawaida, watoto wachanga hawatoi machozi wanapolia. Wana unyevunyevu wa kutosha kulinda macho yao, lakini machozi halisi huanza kutoka majuma kadhaa baada ya vifereji vyao vya machozi kukomaa kikamili.

Aina Tatu za Machozi

  • Machozi ya Msingi. Tezi za machozi hutengeneza umajimaji huu ambao hulowanisha na kulinda macho yetu. Pia, huboresha jinsi tunavyoona. Tunapopepesa kope za macho, majimaji hayo husambazwa machoni.

  • Machozi ya Ghafula. Machozi haya hufurika unapoingiwa na kitu kinachokera machoni. Machozi ya ghafula hutoka pia kwa sababu ya vitendo fulani, kama vile kupiga miayo na kucheka.

  • Machozi ya Hisia. Haya ni machozi ambayo binadamu hutoa ili kuonyesha hisia nzito. Machozi hayo yana asilimia 24 zaidi ya protini kuliko machozi ya ghafula.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki