Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 4/14 uku. 6
  • Usikate Tamaa!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Usikate Tamaa!
  • Amkeni!—2014
  • Habari Zinazolingana
  • Tatizo la Ulimwenguni Pote
    Amkeni!—2001
  • Kujiua—Pigo la Vijana
    Amkeni!—1998
  • Kwa Nini Watu Hukata Tamaa ya Kuishi?
    Amkeni!—2001
  • Kujiua Tatizo Lililojificha Linaloenea Kasi
    Amkeni!—2000
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2014
g 4/14 uku. 6
Mwanamume ambaye amefadhaika na anafikiria kujiua

HABARI KUU

Usikate Tamaa!

IKIWA ungekutana na Dianaa ungeona jinsi alivyo msichana mwenye urafiki, mwenye akili, na mchangamfu. Hata hivyo, licha ya kuonekana mwenye furaha na urafiki, mara nyingi Diana huwa amevunjika moyo. Anasema: “Kila siku mimi hutamani kufa. Ninaamini kabisa kwamba ulimwengu haunihitaji.”

“Uchunguzi fulani umeonyesha kwamba kwa kila mtu anayejiua, wengine 200 wamejaribu kujiua na wengine 400 wamefikiria kujiua.”—JARIDA LA THE GAZETTE, MONTREAL, KANADA.

Diana anasema kwamba hawezi kujiua. Hata hivyo, mara nyingine haoni sababu ya kuendelea kuishi. Anasema: “Jambo ninalotamani zaidi ni kufa katika aksidenti. Nimekuja kuona kifo kama rafiki badala ya adui.”

Watu wengi wanaweza kuelewa hisia za Diana na wengine wao wamefikiria au hata wamejaribu kujiua. Hata hivyo, wataalamu husema kwamba, lengo la wengi wanaojaribu kujiua si kukomesha maisha yao bali ni kukomesha mateso yanayowapata. Kwa ufupi, wanaamini kwamba wana sababu nzuri ya kufa, wanachohitaji ni sababu ya kuendelea kuishi.

Usikate tamaa! Chunguza sababu tatu za kuendelea kuishi.

MAONI YA WATU: Kuzungumza kuhusu kujiua huwachochea watu watamani kujiua.

UKWELI: Kuzungumzia waziwazi jambo hilo mara nyingi humsaidia mtu anayefikiria kujiua abadili maoni yake.

a Jina limebadilishwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki