Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 10/14 uku. 16
  • Mguu wa Farasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mguu wa Farasi
  • Amkeni!—2014
  • Habari Zinazolingana
  • Wapanda Farasi wa Kitabu cha Ufunuo—Jinsi Unavyopatwa na Matokeo ya Upandaji Wao
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Soko Linalofanywa Oktoba “Soko la Farasi la Kimataifa la Kale Zaidi Katika Ulaya”
    Amkeni!—1999
  • “Farasi Wanaocheza Dansi Hewani”
    Amkeni!—2005
  • Mlima Wachongwa Kuwa Sanamu ya Ukumbusho
    Amkeni!—2002
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2014
g 10/14 uku. 16
Farasi wakikimbia

JE, NI KAZI YA UBUNI?

Mguu wa Farasi

FARASI anaweza kukimbia kwa kasi ya mwendo wa kilometa 50 kwa saa. Ingawa hilo linahusisha misuli yenye uwezo wa pekee, yeye hutumia nguvu kidogo tu. Hilo linawezekanaje? Siri ni miguu yake.

Fikiria kinachotukia farasi anapokimbia. Misuli na kano hufyonza nishati mguu unapokanyaga chini, kisha huachilia mguu kwa ghafula kama springi na kumwezesha farasi kusonga mbele.

Isitoshe, farasi anapokimbia miguu yake hutikisika sana, jambo linaloweza kumuumiza kano. Hata hivyo, misuli yake ya miguu hupunguza mtikisiko. Watafiti wamesema muundo huo ni “ushirikiano wa kipekee kati ya misuli na kano” unaomwezesha farasi kuwa na kasi na pia nguvu.

Wahandisi wanajaribu kuiga muundo wa miguu ya farasi wanapotengeneza roboti zenye miguu minne. Hata hivyo kulingana na Maabara ya Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts, ni vigumu kuiga muundo huo tata hata kwa kutumia vifaa vya kisasa na ujuzi wa uhandisi uliopo.

Una maoni gani? Je, muundo wa mguu wa farasi ulijitokeza wenyewe? Au ulibuniwa?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki