Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 2/15 uku. 9
  • Hekima Ni Ulinzi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Hekima Ni Ulinzi
  • Amkeni!—2015
  • Habari Zinazolingana
  • “Heri Mtu Yule Aonaye Hekima”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Hekima ya Kweli Inapaza Sauti Kubwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2022
  • Baraka ya Yehova Inatajirisha
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Utekaji-nyara—Je, Kuna Utatuzi?
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2015
g 2/15 uku. 9
Wanaume wawili wakiwa wamesimama gizani wakimtazama mwanamke anayeonekana kuwa tajiri akipita

Hekima Ni Ulinzi

“Fidia ya nafsi ya mtu ni utajiri wake, lakini maskini hajasikia kemeo.” —METHALI 13:8.

HATA ingawa utajiri unaweza kumletea mtu faida nyingi, unaweza pia kumletea mtu matatizo hasa katika nyakati hizi za hatari. (2 Timotheo 3:1-5) Katika sehemu fulani za ulimwengu, watu matajiri, kutia ndani watalii wameporwa na wezi au kutekwa nyara.

Katika nchi moja maskini, taarifa moja ya habari ilisema hivi: “Ujambazi, ulaghai, na utekaji-nyara ni matendo yanayosababisha uadui kati ya matajiri na maskini. Mikahawa hulindwa na walinzi wenye silaha; nyumba za matajiri huwa na kuta zenye nyaya zinazokata kama wembe, taa zenye mwanga mkali, kamera, na walinzi.” Hali hiyo iko katika nchi nyingi ulimwenguni.

Hata hivyo, Biblia inasema “maskini hajasikia kemeo.” Unawezaje kufaidika na ushauri huo wenye hekima? Ikiwa unaishi katika eneo lenye uhalifu na jeuri au ikiwa unahitaji kutembelea eneo kama hilo, usivae au kubeba vitu vitakavyofanya uonekane tajiri. Fikiria kwa makini nguo unazovaa na vitu unavyobeba hadharani, hasa ikiwa vitu hivyo vitaonekana waziwazi. Andiko la Methali 22:3, linasema hivi: “Mtu mwerevu ni yule ambaye ameona msiba na kujificha, lakini wasio na uzoefu wameendelea mbele nao lazima waumie.”

Hekima inayopatikana katika Biblia inaonyesha jinsi Muumba wetu anavyotujali, na kwamba anataka tuwe salama. Andiko la Mhubiri 7:12, husema hivi: “Hekima ni ulinzi . . . huwahifadhi hai waliyo nayo.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki