Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g16 Na. 6 kur. 10-11
  • Desiderius Erasmus

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Desiderius Erasmus
  • Amkeni!—2016
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • KUJIFUNZA NA IMANI
  • AGANO JIPYA KATIKA KIGIRIKI
  • Maandiko ya Kikristo Yana Usahihi Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Funzo Namba 6—Maandishi-awali ya Kigiriki ya Kikristo ya Maandiko Matakatifu
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
  • Tafsiri ya Complutensian Polyglot—Ni Kifaa Muhimu Katika Utafsiri
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Biblia Imependwa na Kukandamizwa Pia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2016
g16 Na. 6 kur. 10-11

TUNAYOJIFUNZA KUTOKANA NA HISTORIA

Desiderius Erasmus

Desiderius Erasmus

DESIDERIUS Erasmus (c. 1469-1536) alikuwa mtu aliyeheshimika sana, msomi bora zaidi katika bara la Ulaya, lakini baadaye alionekana kuwa mwoga na mwasi. Aliishi kipindi cha mageuzi makubwa ya kidini, na alifunua makosa ya Kanisa Katoliki na ya baadhi ya wale ambao baadaye wangekuwa wanaharakati wa kanisa hilo. Leo, Erasmus anajulikana kuwa mtu aliyechangia mabadiliko ya kidini barani Ulaya kwa kiasi kikubwa. Alifanya hivyo jinsi gani?

KUJIFUNZA NA IMANI

Kwa kuwa alielewa vizuri sana Kilatini na Kigiriki, Erasmus alianza kulinganisha tafsiri za Biblia za Kilatini, kama vile Vulgate, na nakala za kale za Maandiko ya Kigiriki, ambayo kwa kawaida hujulikana kuwa Agano Jipya. Uchunguzi huo ulimfanya aamini kwamba ujuzi wa Biblia ni muhimu. Hivyo, aliamini kwamba Maandiko Matakatifu yalipaswa kutafsiriwa katika lugha zilizozungumzwa na watu wengi wa siku hizo.

Erasmus alichochea mabadiliko katika Kanisa Katoliki kwa kuwa aliamini kwamba Ukristo unapaswa kuwa njia ya maisha wala si maadhimisho ya kidesturi yasiyo na maana yoyote. Kwa hiyo, wanaharakati walipoanza kuandamana na kudai mabadiliko ya Kanisa Katoliki, Kanisa lilianza kumtilia shaka Erasmus.

Erasmus alifunua makosa ya Kanisa Katoliki na ya baadhi ya wanaharakati

Katika machapisho yake, Erasmus alifunua waziwazi upotoshaji wa viongozi wa kidini, mfumo wao wa maisha uliojaa ubinafsi, na nia ya mapapa, ambao waliunga mkono vita. Alikuwa tofauti na viongozi wa kanisa wafisadi ambao walitumia desturi za kanisa kama vile kuungama dhambi, ibada ya watakatifu, kufunga, na safari za kwenda hija, ili kuwakandamiza waumini. Pia, alipinga mazoea ya kanisa kama vile kulipa pesa ili kufanyiwa maombi ya kupata msamaha na katazo la kufunga ndoa.

AGANO JIPYA KATIKA KIGIRIKI

Katika mwaka wa 1516, Erasmus alitoa tafsiri yake ya kwanza ya Agano Jipya katika Kigiriki, yaani, nakala ya kwanza ya Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo kuchapishwa. Tafsiri hiyo ilitia ndani maelezo ya ziada na tafsiri yake ya Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo katika Kilatini na ilitofautiana na Vulgate. Kadiri wakati ulivyopita aliendelea kurekebisha upya tafsiri yake, hivyo, toleo la mwisho lilikuwa tofauti sana na tafsiri ya Latin Vulgate.

Tafsiri ya Erasmus ya Agano Jipya katika Kigiriki

Tafsiri ya Erasmus ya Agano Jipya katika Kigiriki

Tofauti moja ilikuwa katika andiko la 1 Yohana 5:7. Ili kuunga mkono fundisho la utatu ambalo halitokani na Maandiko, maneno fulani yanayofahamika kuwa comma Johanneum, yaliongezwa katika andiko hilo kwenye tafsiri ya Vulgate. Yalisomeka hivi: “Mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu: na watatu hawa ni umoja.” Hata hivyo, Erasmus aliondoa maneno hayo katika matoleo yake mawili ya kwanza ya tafsiri ya Agano Jipya kwa kuwa hayakupatikana kwenye nakala za awali za Kigiriki. Baadaye, kanisa lilimshinikiza arudishe maneno hayo kwenye toleo la tatu la tafsiri yake.

Matoleo yaliyoboreshwa ya tafsiri ya Maandiko ya Kigiriki ya Erasmus yalitumiwa kutafsiri Maandiko katika lugha zingine barani Ulaya. Martin Luther alitumia matoleo hayo kutafsiri Maandiko ya Kigiriki katika Kijerumani, William Tyndale katika Kiingereza, Antonio Brucioli katika Kiitaliano, na Francisco de Enzinas katika Kihispania.

Erasmus aliishi kipindi chenye msukosuko mkubwa sana wa masuala ya kidini, na tafsiri yake ya Agano Jipya iliwasaidia sana wanaharakati Waprotestanti. Hata baadhi ya watu walimwona kuwa mwanaharakati mpaka Mabadiliko halisi yalipoanza. Erasmus alikataa kuunga mkono upande wowote katika mabishano ya kidini yaliyotokea baadaye. Zaidi ya miaka 100 iliyopita, msomi mmoja anayeitwa David Schaff aliandika kwamba Erasmus “alipokufa hakuwa akiunga mkono upande wowote. Iwe Wakatoliki au Waprotestanti, hakuna anayeweza kudai kwamba alikuwa upande wao.”

TAARIFA FUPI

  • Katika mwaka wa 1516, Erasmus alitoa tafsiri ya Agano Jipya katika Kigiriki. Safu moja ilikuwa na maandishi ya Kigiriki na ile nyingine maandishi ya Kilatini ya Erasmus pamoja na maelezo ya ziada.

  • Kwenye utangulizi wa tafsiri yake ya Agano Jipya, aliandika hivi: “Kwa moyo wote siwaungi mkono wale wanaowazuia watu wa kawaida kusoma Maandiko Matakatifu na wanaopinga [Maandiko] yasitafsiriwe katika lugha za kawaida.”

  • Vitabu vyake vilichomwa moto katika baadhi ya maeneo barani Ulaya na kwa miaka mingi viliwekwa kwenye orodha ya vitabu vilivyopigwa marufuku na mapapa jijini Roma.

Mtu Maarufu Sana

Kwa kweli Erasmus alikuwa msomi mwenye ujuzi mwingi wa mambo mbalimbali. Aliishi na kufanya kazi katika nchi mbalimbali barani Ulaya, na alikuwa rafiki ya watu maarufu katika makao ya kifalme na vyuo vikuu. Wasomi katika nchi nyingi walimwomba ushauri. Machapisho yake yalisomwa na kuthaminiwa na watu wengi, hivyo, kumfanya awe mtu maarufu. Kwa kipindi fulani cha wakati, alikaribishwa kwa heshima kubwa na viongozi wa nchi, wa kanisa, na wasomi kila mahali alipoenda. Hiyo ndiyo sababu mwandishi mmoja anasema Erasmus alikuwa “sawa na watu ambao ni maarufu sana leo.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki