Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g18 Na. 3 uku. 3
  • Uchungu wa Kufiwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Uchungu wa Kufiwa
  • Amkeni!—2018
  • Habari Zinazolingana
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2018
  • Katika Toleo Hili: Kukabiliana na Huzuni ya Kufiwa
    Amkeni!—2018
  • Hali Unazoweza Kutazamia
    Amkeni!—2018
  • Wewe Unajua Kuvumilia Huzuni Nyingi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2018
g18 Na. 3 uku. 3
Mwanamume aliyefiwa akiwa amekaa peke yake mkahawani

KUKABILIANA NA HUZUNI YA KUFIWA

Uchungu Wa Kufiwa

“Baada ya miaka zaidi ya 39 ya ndoa, mke wangu, Sophia,a aliugua kwa muda mrefu na hatimaye akafa. Rafiki zangu walinitegemeza sana, na nilijishughulisha na mambo mengi ili kuondoa mawazo. Lakini kwa mwaka mzima, nilihisi uchungu usioelezeka. Hisia zangu zilikuwa zikipanda na kushuka, na sikuweza kuzidhibiti. Na hata sasa, ingawa miaka mitatu hivi imepita tangu alipokufa, bado nyakati fulani huwa ninapata hisia kali za uchungu, na mara nyingi huwa zinakuja wakati nisiotarajia.”—Kostas.

Je, umefiwa na mtu unayempenda? Ikiwa ndivyo, basi unaelewa hali ya Kostas. Kuna mambo machache sana yanayoweza kutokeza uchungu mwingi kama ule unaotokana na kufiwa na mwenzi wa ndoa, mtu wa ukoo, au rafiki wa karibu. Makala iliyochapishwa na jarida fulani (The American Journal of Psychiatry) inasema kwamba “kifo hufanya tuhisi waziwazi kwamba tumempoteza kabisa mtu tunayempenda, wazo linaloleta uchungu mwingi sana.” Baada ya kufiwa, huenda mtu akajiuliza: ‘Nitahisi uchungu huu hadi lini? Kweli nitawahi kuwa na furaha tena? Ni nini kitanisaidia kupunguza huzuni niliyo nayo?’

Toleo hili la Amkeni! litajibu maswali hayo. Makala inayofuata itazungumzia hali unazoweza kutazamia baada ya kufiwa. Halafu tutachunguza mambo yanayoweza kukusaidia kupunguza huzuni ya kufiwa.

Tunatumaini kwamba makala hizo zitawafariji wote waliofiwa na kuwasaidia wakabiliane na uchungu walio nao.

a Baadhi ya majina katika makala za toleo hili yamebadilishwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki