Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g20 Na. 1 kur. 5-7
  • Mkazo Ni Nini?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mkazo Ni Nini?
  • Amkeni!—2020
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • MKAZO UNAOFAA NA USIOFAA
  • Jinsi Mfadhaiko Unavyotuathiri
    Amkeni!—2010
  • Mkazo Mzuri, Mkazo Mbaya
    Amkeni!—1998
  • Visababishi na Madhara ya Mfadhaiko
    Amkeni!—2005
  • Jinsi ya Kudhibiti Mfadhaiko
    Amkeni!—2010
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2020
g20 Na. 1 kur. 5-7
Mfanyabiashara akikimbia kuelekea jengo la ofisi.

UNAWEZA KUKABILIANA NA MKAZO—JINSI GANI?

Mkazo Ni Nini?

Mkazo hutokea mwili unapojitayarisha kuchukua hatua ili kukabiliana na changamoto au hatari fulani. Ubongo husababisha tezi zitoe homoni nyingi na kusafirishwa sehemu mbalimbali mwilini. Homoni hizo huongeza kasi ya mapigo ya moyo, hudhibiti shinikizo la damu, hufanya mtu apumue haraka-haraka, na misuli kukaza. Hata kabla ya mtu kutambua kinachoendelea, mwili unakuwa tayari kuchukua hatua. Hali inayoleta mkazo inapokwisha, mwili hurudia hali yake ya kawaida.

MKAZO UNAOFAA NA USIOFAA

Mkazo ni hali ya asili ambayo mwili hujitayarisha kuchukua hatua dhidi ya changamoto au hatari fulani. Hali hiyo huanzia kwenye ubongo. Mkazo unaofaa hukuwezesha kutenda au kuchukua hatua haraka. Kiwango fulani cha mkazo kinaweza kukusaidia pia kufikia malengo yako au kufanya vizuri, labda wakati wa mtihani, mahojiano ya kazi au katika mchezo.

Hata hivyo, mkazo mwingi sana na unaoendelea kwa muda mrefu unaweza kukudhuru. Ikiwa mwili unakuwa katika hali ya ‘tahadhari’ kwa sababu ya mkazo mwingi mara kwa mara, huenda mtu akaanza kuugua kimwili, kihisia na kiakili pia. Tabia yako kutia ndani jinsi unavyowatendea wengine huenda ikabadilika. Mtu anapokuwa na mkazo kupita kiasi anaweza kuanza kutumia kileo sana, dawa za kulevya au kujihusisha na mazoea mengine mabaya. Pia, mkazo unaweza kusababisha mtu ashuke moyo, achoke kupita kiasi au hata kuwa na mawazo ya kujiua.

Ingawa mkazo huathiri watu kwa njia tofauti-tofauti, unaweza kusababisha matatizo ya afya kwa kiasi kikubwa. Na unaweza kuathiri karibu kila sehemu ya mwili.

JINSI MKAZO UNAVYOATHIRI MWILI WAKO

Mfumo wa Neva.

Mwanamume ameshika paji la uso wake kwa sababu ya kulemewa na mkazo.

Mfumo wako wa neva huwezesha homoni kama vile adrenalini na cortisol kutolewa. Homoni hizo husababisha moyo upige kwa kasi, na pia shinikizo la damu na kiwango cha sukari kuongezeka. Mambo hayo yote yanafanya mwili uchukue hatua haraka dhidi ya hatari. Mkazo ukizidi sana unaweza kusababisha

  • kukasirika haraka, wasiwasi, kushuka moyo, maumivu ya kichwa, kukosa usingizi

Mifupa na misuli.

Misuli yako hukaza ili kukulinda dhidi ya majeraha. Mkazo ukizidi sana unaweza kusababisha

  • maumivu ya mwili, maumivu makali sana ya kichwa, misuli kukaza ghafla

Mfumo wa upumuaji.

Mtu hupumua haraka ili apate hewa nyingi ya oksijeni. Mkazo ukizidi sana unaweza kusababisha

  • kupumua haraka-haraka, kukosa hewa ya kutosha, na pia kuwa na wasiwasi kupita kiasi

Mfumo wa mishipa ya damu ya moyo.

Moyo wako hupiga kwa kasi na kwa nguvu ili kusambaza damu mwilini. Mishipa ya damu hutanuka au kusinyaa ili kuelekeza damu sehemu zilizo na uhitaji mwingi zaidi kama vile kwenye misuli. Mkazo ukizidi sana unaweza kusababisha

  • shinikizo la damu, mshtuko wa moyo, kiharusi

Mfumo wa homoni.

Tezi za mwili hutoa homoni aina ya adrenalini na cortisol, homoni ambazo husaidia mwili unapokabili mkazo. Ini huongeza kiwango cha sukari ili kuupa mwili nguvu. Mkazo ukizidi sana unaweza kusababisha

  • ugonjwa wa kisukari, kupungua kwa kinga mwilini na hivyo kupatwa na magonjwa kwa urahisi, kubadilika-badilika kwa hisia, kuongeza uzito wa mwili

Mfumo wa kumeng’enya chakula.

Mkazo huathiri jinsi mwili unavyomeng’enya chakula. Mkazo ukizidi sana unaweza kusababisha

  • kichefuchefu, kutapika, kuharisha, kushindwa kupata haja kubwa

Mfumo wa uzazi.

Mkazo unaweza kusababisha kukosa hamu ya ngono. Mkazo ukizidi sana unaweza kusababisha

  • kukosa nguvu za kiume, kutopata hedhi kwa ukawaida

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki