Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g20 Na. 3 kur. 12-13
  • Uwe na Upendo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Uwe na Upendo
  • Amkeni!—2020
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Tatizo
  • Kanuni ya Biblia
  • Mambo Unayoweza Kufanya
  • Walifaulu Kuushinda Ubaguzi
    Amkeni!—2020
  • Ubaguzi—Je, Umekuathiri?
    Amkeni!—2020
  • Nilitaka Kupigania Haki
    Biblia Inabadili Maisha
  • Ubaguzi Utakwisha Lini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2020
g20 Na. 3 kur. 12-13
Mwanamke Mhindi akiwa amebeba mzigo na akimsaidia mwanamke Mzungu kupanda ngazi.

Uwe Na Upendo

Tatizo

Hisia za ubaguzi haziishi haraka. Inachukua muda mrefu kuangamiza virusi vinavyosababisha magonjwa. Vivyo hivyo, inachukua muda mrefu kuondoa kabisa hisia za ubaguzi. Unaweza kufanya nini ili kuondoa hisia za ubaguzi moyoni mwako?

Kanuni ya Biblia

Picha: 1. Mwanamume mwenye asili ya Asia akiwa amefungua mlango ili mwanamume mweusi aliyebeba vikombe vya kahawa aweze kupita. 2. Mwanamume huyo mweusi akiwapa wafanyakazi wenzake kahawa kutia ndani mwanamke Mhindi aliyetajwa awali.

“Jivikeni upendo, kwa maana huo ni kifungo kikamilifu cha muungano.”​—WAKOLOSAI 3:14.

Kanuni hiyo inamaanisha nini? Kuwatendea wengine mema hutusaidia tuwe na umoja. Kadiri unavyowaonyesha wengine upendo, ndivyo hisia za ubaguzi zinavyozidi kupungua. Na kadiri unavyositawisha upendo zaidi, ndivyo unavyozidi kuondoa hisia za chuki.

Mambo Unayoweza Kufanya

Picha: 1. Mwanamke Mzungu akisaidiwa kupanda ngazi na mwanamke Mhindi aliyebeba mzigo. 2. Mwanamke Mzungu akimpatia biskuti jirani yake; jirani yake ni mwanamume mwenye asili ya Asia aliyetajwa awali.

Fikiria njia hususa ambazo unaweza kuwaonyesha upendo watu ambao una maoni yasiyofaa kuwahusu. Si lazima ufanye mambo makubwa. Jaribu kufanya jambo moja au zaidi kati ya haya:

Kila tendo dogo la upendo litakusaidia kushinda ubaguzi

  • Waonyeshe heshima kwa kuwaelekeza njia ikiwa wamepotea au kwa kuwapisha waketi sehemu yako unapotumia usafiri wa umma.

  • Jaribu kuzungumza nao hata ikiwa hawazungumzi lugha yako vizuri.

  • Uwe na subira wanapofanya mambo kwa njia ambayo huielewi.

  • Sikiliza kwa huruma wanapokueleza matatizo yao.

Simulizi: Nazaré (Guinea-Bissau)

“Zamani niliwabagua wahamiaji. Niliambiwa kwamba wahamiaji wengi hudanganya serikali ili wapate msaada wa kifedha na wengi wao ni wahalifu. Jambo hilo lilifanya niwe na mtazamo usiofaa kuwaelekea. Hata hivyo, sikuona hisia zangu kuwa ni ubaguzi kwa sababu watu wengi walikuwa na maoni hayo.

“Baada ya muda, nilitambua kwamba hisia hizo zilikuwa ni ubaguzi. Ushauri wa Biblia umenisaidia kuwaonyesha upendo zaidi. Sasa, siwaepuki tena. Badala yake, ninawasalimia na kuzungumza nao. Ninajitahidi kumjua mtu mmoja-mmoja. Na sasa nina mtazamo mzuri kuwaelekea na sina wasiwasi ninapokuwa nao.”

“Nilitaka Kupigania Haki”

Rafika Morris.

Rafika alijiunga na kikundi cha wafanya-mabadiliko ili kupambana na ubaguzi wa rangi. Hatimaye, alipata umoja aliokuwa akitafuta alipohudhuria kusanyiko la Mashahidi wa Yehova.

Tazama video Rafika Morris: Nilitaka Kupigania Haki. Tafuta video hiyo kwenye tovuti ya jw.org/sw

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki