Utangulizi
Je, teknolojia inakutawala au inakusaidia? Watu wengi wangejibu kwamba wana uwezo wa kudhibiti vifaa vyao vya kielektroni, na kwamba vifaa hivyo haviwezi kuwaongoza. Lakini teknolojia inaweza kuwaathiri watu kwa njia isiyo ya wazi—hata kuwasababishia matatizo.