Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g22 Na. 1 kur. 4-6
  • 1 | Linda Afya Yako

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • 1 | Linda Afya Yako
  • Amkeni!—2022
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • KWA NINI NI MUHIMU?
  • Unachopaswa Kujua
  • Unachoweza Kufanya Sasa
  • Njia za Kuboresha Afya Yako
    Amkeni!—2015
  • Jinsi ya Kukabiliana na Tatizo la Afya
    Habari Zaidi
  • Jinsi ya Kulinda Afya Yako
    Amkeni!—1999
  • Dumisha Imani na Afya Yako ya Kiroho
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2022
g22 Na. 1 kur. 4-6
Meza iliyo na vyakula mbalimbali vyenye lishe.

ULIMWENGU WENYE MISUKOSUKO

1 | Linda Afya Yako

KWA NINI NI MUHIMU?

Afya ya mtu inaweza kuathiriwa kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja na misukosuko au majanga.

  • Matatizo huwaletea watu mkazo, na mara nyingi mkazo usioisha husababisha matatizo ya afya.

  • Majanga yanaweza kusababisha mifumo ya afya kulemewa na kuzuia upatikanaji wa huduma za afya.

  • Majanga huathiri hali ya uchumi wa mtu na kufanya ashindwe kulipia huduma muhimu kama vile, chakula chenye lishe au huduma ya afya.

Unachopaswa Kujua

  • Ugonjwa mbaya na mkazo, unaweza kuathiri uwezo wako wa kufanya maamuzi hivi kwamba ukaanza kupuuza kufanya mambo yanayoweza kuboresha afya yako. Hilo linaweza kufanya uwe mgonjwa zaidi.

  • Usipotibiwa, afya yako itakuwa mbaya zaidi na huenda uhai wako ukawa hatarini.

  • Ukiwa na afya njema utaweza kufanya maamuzi mazuri unapokabili matatizo.

  • Hata uwe na hali gani ya kiuchumi, chukua hatua zinazofaa kulinda afya yako.

Unachoweza Kufanya Sasa

Kadiri inavyowezekana, mtu mwenye hekima hufikiria hatari anazoweza kukabili na kuchukua hatua zinazofaa ili kuziepuka. Unaweza kutumia ushauri huo inapohusu afya yako. Mara nyingi unaweza kupunguza hatari ya kupatwa na magonjwa kwa kudumisha usafi. Kinga ni bora kuliko tiba.

“Tumepunguza gharama ya kwenda kumwona daktari na kununua dawa kwa kudumisha usafi.”​—Andreas.a

a Baadhi ya majina katika gazeti hili yamebadilishwa.

JINSI YA KUKABILIANA NA HALI​—Madokezo Yanayofaa

Wakati wa misukosuko, linda afya yako kwa kuchukua hatua hizi zinazofaa

DUMISHA USAFI

Mwanamume akinawa mikono kwa sabuni na maji.

Dumisha usafi

Biblia inasema hivi: “Mtu mwerevu huona hatari na kujificha.” (Methali 22:3) Jaribu kufikiria na kuepuka hali zinazoweza kuhatarisha afya yako.

  • Safisha mikono yako mara kwa mara kwa kutumia sabuni na maji, hasa kabla ya kula chakula au baada ya kutumia choo.

  • Safisha nyumba yako kwa kutumia dawa ya kuua viini vya magonjwa, hasa katika vitu au maeneo yanayoguswa mara kwa mara.

  • Ikiwezekana, epuka kuwa karibu na watu wenye magonjwa ya kuambukiza.

KULA VYAKULA VYENYE LISHE

Meza iliyo na vyakula mbalimbali vyenye lishe.

Kula vyakula vyenye lishe

Biblia inasema hivi: “Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake, bali huulisha na kuutunza.” (Waefeso 5:29) Tunaonyesha kwamba tunaipenda miili yetu kwa kuilisha vizuri.

  • Kunywa maji ya kutosha.

  • Kula aina mbalimbali za matunda na mbogamboga.

  • Punguza matumizi ya mafuta, chumvi, na sukari.

  • Usitumie tumbaku au dawa za kulevya, au uepuke matumizi mabaya ya kileo.

“Ili tusiugue tunajitahidi kula vyakula vyenye lishe, tusipofanya hivyo tutalazimika kutumia kiasi kidogo cha pesa tulicho nacho ili kugharamia matibabu. Tunatumia pesa zetu kununua vyakula vyenye lishe.”​—Carlos.

FANYA MAZOEZI NA ULALE VYA KUTOSHA

Mwanamume akiwa anakimbia katika barabara.

Fanya mazoezi

Biblia inasema hivi: “Ni afadhali konzi moja ya pumziko kuliko konzi mbili za kazi ngumu na kukimbiza upepo.” (Mhubiri 4:6) Tunahitaji kuwa na usawaziko inapohusu kazi na kupumzika vya kutosha.

  • Fanya mazoezi kwa ukawaida. Unaweza kuanza kwa kutembea kwa miguu. Mazoezi yanaweza kuboresha afya yako hata ikiwa umezeeka, ni mlemavu, au una ugonjwa wa kudumu.

  • Mwanamke kijana akiwa amelala.

    Lala vya kutosha

    Pumzika vya kutosha. Ikiwa hutalala vya kutosha, baada ya muda mfupi utakuwa na mkazo na utashindwa kukazia fikira. Hali hiyo ikiendelea kwa muda mrefu inaweza kukusababishia matatizo makubwa ya afya.

  • Jiwekee ratiba ya wakati wa kulala na uifuate ratiba hiyo. Jitahidi kulala na kuamka wakati uleule kila siku.

  • Usitazame televisheni au kutumia vifaa vya kielektroni wakati wa kulala.

  • Usile chakula kizito, kafeini, au kileo kabla ya kulala.

“Nimegundua kwamba ratiba yangu ya kulala huathiri afya yangu yote. Nisipolala vya kutosha, mimi hupatwa na maumivu ya kichwa na mwili mzima. Lakini ninapolala vya kutosha, ninahisi kana kwamba ninaweza kutimiza mambo mengi, ninakuwa na nguvu na mara nyingi sipatwi na magonjwa.”​—Justin.

Sehemu ya video yenye kichwa, “Unaweza Kufanya Nini Magonjwa ya Mlipuko Yakitokea?” Mwanamke anafungua mlango na kuruhusu kisehemu cha kirusi kuingia ndani.

JIFUNZE MENGI ZAIDI. Tazama video yenye kichwa, Unaweza Kufanya Nini Magonjwa ya Mlipuko Yakitokea? Pia, soma makala yenye kichwa “Njia za Kuboresha Afya Yako.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki