Sura ya 12
Kashawishwa na Ibilisi
JE! Ye yote amepata kukuomba kufanya jambo fulani baya?— Je! alikushawishi ulifanye? Au alisema ingekuwa mchezo na isingekuwa vibaya kufanya?— Wakati mtu fulani anapofanya hivi kwetu, yeye anajaribu kutushawishi.
Imetupasa tufanye nini wakati tunaposhawishwa? Je! tukubali na kutenda baya?— Hiyo isingempendeza Yehova Mungu. Lakini unajua ambaye ingefurahisha?— Shetani Ibilisi.
Shetani ni adui ya Mungu naye ni adui yetu. Hatuwezi kumwona, kwa sababu yeye ni roho. Lakini yeye aweza kutuona. Siku moja Ibilisi alisema na Yesu, Mwalimu Mkuu, akajaribu kumshawishi. Na tuone Yesu alifanya nini. Ndipo tutajua jambo jema kufanya wakati tunaposhawishwa.
Yesu alikuwa amekwenda milimani kusali kwa Mungu. Yeye alitaka afikirie kazi ambayo Mungu alimpa aifanye.
Yesu alipokuwa huko milimani, siku arobaini mchana na usiku zikapita! Wakati wote huu Yesu hakula cho chote. Sasa Yesu aliona njaa sana.
Ndio wakati Shetani alijaribu kumshawishi Yesu. Ibilisi akasema: “Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hill liwe mkate.” Lo! namna mkate ungekuwa mtamu!
Lakini Yesu angeweza kugeuza jiwe liwe mkate?— Ndiyo, angeweza. Kwa maana Yesu ni Mwana wa Mungu. Ana nguvu za pekee.
Ikiwa Ibilisi angalikuambia ugeuze jiwe liwe mkate ungalifanya hivyo?— Yesu aliona njaa. Basi je! ingalifaa kufanya mara moja tu?— Yesu alijua ingekuwa vibaya kutumia nguvu zake katika njia hii. Yehova alimpa nguvu hizi awavute watu kwa Mungu, si kwa matumizi yake mwenyewe.
Basi, Yesu akamwambia Shetani kwamba imeandikwa katika Biblia: “Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.” Yesu alijua kwamba kufanya yampendezayo Yehova ni kwa maana hata zaidi kuliko chakula.
Lakini Ibilisi akajaribu tena. Akamchukua Yesu Yerusalemu akamsimamisha juu ya kilele cha hekalu. Ndipo Ibilisi akamwambia Yesu: ‘Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini. Kwa maana imeandikwa kwamba malaika za Mungu watakulinda usijiumize.’ Yesu alifanyaje?—
Tena, Yesu hakumsikiliza Shetani. Alimwambia Shetani kwamba ilikuwa vibaya kumjaribu Yehova kwa kuchezea uhai wake.
Hata hivyo Shetani hakuchoka. Akampeleka Yesu kwenye mlima mrefu sana sana. Akamwonyesha falme zote za ulimwengu na fahari yake. Kisha Shetani akamwambia Yesu: ‘Mambo yote haya nitakupa ikiwa utasuju-du na kuniabudu mimi.’ Wewe ungalifanyaje?—
Yesu asingefanya. Alijua ingekuwa vibaya kumwabudu Ibilisi si kitu angepata nini. Basi Yesu akamwambia Ibilisi: ‘Nenda zako, Shetani! Maana Biblia inasema, Ni Yehova Mungu wako ambaye inakupasa uabudu, na inakupasa umtumikie yeye peke yake.’—Luka 4:1-13; Mathayo 4:1-10.
Sisi vile vile tunapatwa na vishawishi. Unajua namna gani?— Hapa pana mfano.
Huenda mama yako akatengeneza maandazi matamu kwa chakula kikuu. Lakini labda atakuambia usile mojawapo mpaka wakati wa chakula. Labda utaona njaa sana. Basi utaona kushawishwa kula. Je! utamtii mama yako?— Shetani anataka usimtii.
Lakini mkumbuke Yesu. Yeye vile vile aliona njaa sana. Lakini alijua kumpendeza Mungu kulikuwa kwa maana zaidi.
Utakapokuwa mtu mzima kidogo, huenda watoto wengine watakuambia umeze dawa fulani. Au labda watakupa sigara uvute. Labda watakuambia hivi vitakufanya uone raha kweli kweli. Lakini vitu hivi huenda vikawa dawa zenye sumu. Vyaweza kukufanya uwe mgonjwa sana, na hata vyaweza kukuua. Utafanyaje?—
Mkumbuke Yesu. Shetani alijaribu kumshawishi achezee uhai wake kwa kumwambia aruke kutoka hekaluni. Lakini Yesu asingefanya. Hakumsikiliza Shetani. Wala wewe usimsikilize ye yote anayejaribu kukushawishi uchukue dawa zenye sumu.
Ni vyepesi kufanya mema wakati kila mtu anafanya. Lakini inaweza kuwa vigumu sana wakati wengine wanajaribu kutushawishi tufanye mabaya. Huenda wakasema wanalofanya si baya sana. Lakini ulizo kubwa ni, Mungu anasema nini juu yake? Yeye ajua zaidi.
Basi si kitu wengine waseme nini, sisi hatutafanya ambayo Mungu anasema si mazuri. Katika njia hiyo tutamfurahisha Mungu sikuzote, na hatutamtumikia Ibilisi hata kidogo.
(Shauri jema zaidi juu ya kushinda shawishi la kufanya mabaya linapatikana katika Mathayo 26:41, Mithali 22:24, 25 na Zaburi 1:1, 2.)