Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • my hadithi 94
  • Anapenda Watoto Wadogo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Anapenda Watoto Wadogo
  • Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Bishano Lafoka
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Kuwatayarisha Mitume kwa Ajili ya Kuondoka Kwake
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Bishano Lafoka
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • “Mkakae kwa Amani Ninyi kwa Ninyi”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
Pata Habari Zaidi
Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
my hadithi 94
Yesu akiwa amemkumbatia mtoto mdogo

HADITHI YA 94

Anapenda Watoto Wadogo

MTAZAME Yesu hapa akimkumbatia mtoto. Unaweza kujua kwamba Yesu anapenda sana watoto. Wanaume wanaotazama ni mitume wake. Yesu anawaambia nini? Acha tuone.

Sasa ndiyo Yesu na mitume wake wamerudi katika safari ndefu. Njiani mitume hao waligombana. Basi baada ya safari hiyo Yesu anawauliza: ‘Mlikuwa mkigombana njiani juu ya nini?’ Yesu anajua walichogombania. Lakini anauliza maulizo aone kama mitume watamwambia.

Mitume hawajibu, kwa sababu njiani waligombana juu ya nani kati yao aliye mkubwa zaidi. Mitume fulani wanataka kuwa wakubwa kuliko wenzao. Yesu atawaambia namna gani kwamba haifai kutaka kuwa mkubwa zaidi?

Amwita mvulana mdogo na kumsimamisha mbele yao wote. Kisha anawaambia wanafunzi wake hivi: ‘Nataka mjue hakika ya hili, kama hamgeuki mwe kama watoto wadogo, hamtaingia katika ufalme wa Mungu. Aliye mkubwa zaidi katika ufalme huo ni mtu anayekuwa kama mtoto huyu.’ Unajua sababu Yesu alisema hivyo?

Watoto wadogo sana hawataki kuwa wakubwa kuliko wenzao. Inawapasa mitume wawe kama watoto kwa njia hiyo, wasigombane juu ya ukubwa.

Nyakati nyingine pia, Yesu anaonyesha namna anavyopenda sana watoto wadogo. Miezi michache baadaye watu fulani wanaleta watoto wamwone Yesu. Mitume wanajaribu kuwazuia. Lakini Yesu anawaambia mitume wake hivi: ‘Acheni watoto waje kwangu, msiwazuie, kwa sababu ufalme wa Mungu ni wa watu kama hao.’ Ndipo Yesu anachukua watoto mikononi mwake, anawabariki. Ni vizuri kujua kwamba Yesu anawapenda watoto wadogo, sivyo?

Mathayo 18:1-4; 19:13-15; Marko 9:33-37; 10:13-16.

Maswali ya Funzo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki