Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • my hadithi 113
  • Paulo Katika Roma

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Paulo Katika Roma
  • Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Filemoni—Ushuhuda wa Ukristo Wenye Matendo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Kitabu cha Biblia Namba 57—Filemoni
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
  • Filemoni na Onesimo—Wenye Kuungana Katika Udugu wa Kikristo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • ‘Kuhimiza kwa Msingi wa Upendo’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
Pata Habari Zaidi
Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
my hadithi 113
Mtume Paulo anamwambia Timotheo maneno ya kuandika katika barua huku askari Mroma akimlinda

HADITHI YA 113

Paulo Katika Roma

UTAZAME mnyororo mikononi mwa Paulo, mtazame askari wa Roma anayemlinda. Paulo amefungwa Roma. Anangojea Kaisari wa Roma aamue atamfanyia nini. Akiwa bado mfungwa, watu wanakubaliwa wamtembelee.

Siku tatu baada ya Paulo kufika Roma anapeleka ujumbe ili viongozi fulani wa Kiyahudi waje wamwone. Wayahudi wengi katika Roma wanakuja. Paulo anahubiri habari za Yesu na ufalme wa Mungu. Wengine wanaamini na kuwa Wakristo, lakini wengine wanakataa kuamini.

Pia Paulo anawahubiri askari mbalimbali wanaomlinda. Kwa miaka miwili ambayo Paulo amefungwa humu anamhubiri kila mtu. Matokeo ni kwamba, wale wa nyumba ya Kaisari wanasikia habari njema za Ufalme, na wengine wao wanakuwa Wakristo.

Timotheo anaandika maneno ya Paulo

Lakini mgeni huyu anayeandika mezani ni nani? Unaweza kuwazia? Ni Timotheo. Timotheo pia alikuwa amefungwa kwa sababu ya kuhubiri habari za Ufalme, lakini amefunguliwa. Amekuja kumsaidia Paulo. Unajua anachoandika Timotheo? Na tuone.

Unakumbuka ile miji ya Filipi na Efeso katika Hadithi ya 110? Paulo alisaidia kuanzisha makundi ya Kikristo katika miji hiyo. Sasa, akiwa gerezani, Paulo anawaandikia barua Wakristo hao. Barua hizo zimo katika Biblia, nazo zaitwa Waefeso na Wafilipi. Sasa Paulo anamwambia Timotheo mambo ya kuandikia rafiki Wakristo katika Filipi.

Wafilipi wamemwonyesha Paulo fadhili nyingi. Walimpelekea zawadi kifungoni, hivyo Paulo anawashukuru. Epafrodito ndiye aliyeleta zawadi hiyo. Lakini akawa mgonjwa karibu kufa. Sasa amepona na yuko tayari kwenda nyumbani. Atachukua barua hii ya Paulo na Timotheo akirudi Filipi.

Akiwa gerezani Paulo anaandika barua nyingine mbili tulizo nazo katika Biblia. Moja ni kwa Wakristo walio katika mji wa Kolosai. Unajua inavyoitwa? Wakolosai. Nyingine ni barua ya binafsi aliyomwandikia Filemoni, rafiki yake mkubwa. Yeye pia anakaa Kolosai. Barua hiyo ni juu ya Onesimo mtumishi wa Filemoni.

Onesimo alimkimbia Filemoni akaja Roma. Onesimo akajua Paulo amefungwa huku. Akaja kumtembelea, naye Paulo akamhubiri Onesimo. Upesi Onesimo pia anakuwa Mkristo. Sasa Onesimo anasikitika kwa vile alivyokimbia. Unajua jambo ambalo Paulo anamwandikia Filemoni katika barua hiyo?

Paulo anamwomba Filemoni amsamehe Onesimo. ‘Ninamrudisha kwako,’ Paulo anaandika. ‘Lakini sasa si mtumishi wako tu. Yeye pia ni ndugu Mkristo mzuri.’ Onesimo anaporudi Kolosai anachukua barua hizo mbili, moja ya Wakolosai na nyingine ya Filemoni. Twaweza kuwazia Filemoni anavyofurahi anapojua kwamba mtumishi wake sasa amekuwa Mkristo.

Paulo anapoandikia Wafilipi na Filemoni, ana habari njema kweli kweli. ‘Namtuma Timotheo kwenu,’ Paulo anawaambia Wafilipi. ‘Lakini mimi pia nitawatembelea upesi.’ Na kwa Filemoni, anaandika hivi: ‘Unitayarishie mahali pa kukaa huko.’

Paulo anapofunguliwa anatembelea ndugu na dada zake Wakristo mahali pengi. Lakini baadaye Paulo anafungwa tena Roma. Wakati huu anajua atauawa. Basi anamwandikia Timotheo akimwomba aje upesi. ‘Nimekuwa mwaminifu kwa Mungu,’ Paulo anaandika, ‘naye Mungu atanilipa.’ Miaka michache baada ya Paulo kuuawa, Yerusalemu unaharibiwa tena, wakati huu na Warumi.

Lakini kuna mambo zaidi katika Biblia. Yehova Mungu amwagiza mtume Yohana aandike vitabu vya mwisho, kutia na kitabu cha Ufunuo. Kitabu hicho cha Biblia kinasimulia juu ya wakati ujao. Sasa na tujifunze yatakayotokea wakati ujao.

Matendo 28:16-31; Wafilipi 1:13; 2:19-30; 4:18-23; Waebrania 13:23; Filemoni 1-25; Wakolosai 4:7-9; 2 Timotheo 4:7-9.

Maswali ya Funzo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki