Wimbo 39
Mashujaa wa Mungu Wanasonga Mbele
1. Mashujaa wasonga;
Wanathibitika
Waheshimu Yehova,
Watetea jina.
Lijapokuwa joka
Lipigane nao,
Kukinga jeshi lake
Mungu yumo sana.
2. Vita ni ya jeuri
Siku hii ya Yah.
Twahubiri hakika.
Hatuwaogopi
Mwana ni Jemadari
Kwa haki ashinde.
Apinga shambulio;
Tu upande wake.
3. Na Mungu tunasonga
Atashinda sana.
Tujikaze kufika
Atetewe sana.
Ushindi ni hakika,
Zawadi ni yao
Waliojaribiwa,
Na waaminifu.