Wimbo 124
Tunda la Kujiweza
1. E tunza nafusi yako;
Ushike ukweli.
Endelea kujiweza,
Ukashinde vita.
2. Tuonyeshavyo upendo
Hekima daima,
Tuwe kama Mungu juu.
Tunapojiweza.
3. Mwili tuutumikishe,
Na tusitamani.
Na ili tujiokoe,
Sharti tujiweze.
4. Tutulie jaribuni
Hata taabuni;
Usimame na Yehova
Kwa uadilifu.