Wimbo 136
Waabudu Washikamanifu Wambariki Yehova
1. Washikamanifu Na wakubariki;
Utufanikishe Ukipenda.
Wastahili sifa; Njia zako njema.
Kwa ushikamani Twatumika.
2. Tunakuheshimu —Asante zizidi
Tunajihadhari Kwa usafi.
E tusaidie Tukuze imani.
Ewe Bwana tuwe Kamilifu.
3. Tupe ufahamu Wa kusudi lako
Ambalo wakuza Wewe sana.
Tuonyeshe wema, Na tusianguke.
E tusikilize, Kila siku.
4. Ewe Baba yetu, Utusaidie,
Ili tutangaze Jina lako.
Tuwe na amani, Tukusifu wewe
Duniani kote, Usifike.