Wimbo 204
“Mimi Hapa, Nitume Mimi”
1. Leo watu hulisuta
Jina zuri lake Mungu.
Wasema Mungu dhaifu;
Wasema “Hakuna Mungu!”
Nani atalitetea?
Nani atasifu Mungu?
“Mimi hapa, N’tume mimi.
Nikwimbie sifa zako;
(Korasi)
2. Wacheka anakawia;
Hawajui kumwogopa.
Sanamu huziabudu;
Kaisari wamwabudu.
Nani ataonya mwovu?
Juu ya vita ya Mungu?
“Mimi hapa, N’tume mimi.
Mimi nitatoa onyo;
(Korasi)
3. Leo wapole hulia;
Kwani maovu yazidi.
Kwa unyofu watafuta
Ukweli wenye amani.
Nani atawafariji?
Waone uadilifu?
“Mimi hapa, N’tume mimi.
Nitawafunza wapole;
(KORASI)
Ni heshima kubwa zaidi.
Mimi hapa, nitume.”