Wimbo Na. 10
“Mimi Hapa! Nitume Mimi”
Makala Iliyochapishwa
1. Leo watu hulisuta,
Jina zuri lake Mungu.
Wasema “Hakuna Mungu!”
Eti Mungu ni dhaifu.
Nani atamutetea?
Nani atamupa sifa?
‘Bwana, Mimi hapa! N’tume.
Sifa zako Nikwimbie.
(KORASI)
Ni pendeleo kubwa sana.
Bwana nitume mimi.’
2. Wadai anakawia;
Hawamuogopi Mungu.
Sanamu huziabudu;
Kaisari wamwabudu.
Nani atamwonya mwovu,
Kuhusu vita ya Mungu?
‘Bwana, Mimi hapa! N’tume.
Nitawaonya waovu.
(KORASI)
Ni pendeleo kubwa sana.
Bwana nitume mimi.’
3. Wapole wanaugua,
Mbona maovu yazidi.
Kwa unyofu watafuta
Ukweli wenye amani.
Nani atawafariji?
Waone uadilifu?
‘Bwana Mimi hapa! N’tume.
Nitawafunza wapole.
(KORASI)
Ni pendeleo kubwa sana.
Bwana nitume mimi.’
(Ona pia Zab. 10:4; Eze. 9:4.)