Sura ya 8
Kujitahidi Kuwa Washindi
SMIRNA
1. (a) Ni kundi gani linalofuata kupokea ujumbe kutoka kwa Yesu aliyetukuzwa? (b) Kwa kujiita mwenyewe “wa Kwanza na wa Mwisho,” Yesu aliwakumbusha nini Wakristo katika kundi hilo?
LEO, Efeso la kale linalala likiwa magofu. Lakini kule ambako Yesu alipeleka ujumbe wake wa pili kungali ni mahali penye jiji lenye kuvuma shughuli nyingi. Kilometa zapata 56 kaskazini mwa magofu ya Efeso kuna jiji la Kituruki la Izmiri, ambako makundi manne yenye bidii ya Mashahidi wa Yehova yanapatikana hata leo. Hapo, katika karne ya kwanza, lilikuwako Smirna. Angalia, sasa, maneno yafuatayo ya Yesu: “Na kwa malaika wa kundi katika Smirna andika: Hivi ndivyo vitu ambavyo anasema, ‘yule wa Kwanza na wa Mwisho,’ ambaye akapata kuwa mfu na akaja kwenye uhai tena.” (Ufunuo 2:8, NW) Kwa kuwataarifu hivi Wakristo hao katika Smirna, Yesu anawakumbusha kwamba yeye alikuwa ndiye mshika ukamilifu wa kwanza ambaye Yehova alifufua moja kwa moja kwenye uhai wa kiroho usioweza kufa na ndiye wa mwisho kuinuliwa hivyo. Yesu mwenyewe angefufua Wakristo wengine wote wapakwa-mafuta. Yeye anastahili vizuri hivyo kuwapa shauri ndugu zake, ambao wanatumaini kushiriki naye uhai wa kimbingu usioweza kufa.
2. Ni kwa sababu gani Wakristo wote wanafarijiwa na maneno ya Mmoja ambaye “alipata kuwa mfu na akaja kwenye uhai tena”?
2 Yesu aliongoza njia katika kuvumilia minyanyaso kwa ajili ya uadilifu, naye alipokea thawabu aliyostahili. Uaminifu wake mpaka kifo na ufufuo uliofuata ndio msingi wa tumaini kwa Wakristo wote. (Matendo 17:31) Uhakika wa kwamba Yesu “akapata kuwa mfu na akaja kwenye uhai tena” unathibitisha kwamba lolote ambalo ni lazima livumiliwe katika kusudi la ukweli si kazi bure. Ufufuo wa Yesu ni chanzo cha kitia-moyo chenye kina kirefu kwa Wakristo wote, hasa wakati wanapoitwa wateseke kwa ajili ya imani yao. Je! hii ndiyo hali yako? Basi wewe unaweza kujipa moyo pia kutokana na maneno yanayofuata ya Yesu kwa kundi la Smirna.
3. (a) Ni kitia-moyo gani ambacho Yesu aliwapa Wakristo katika Smirna? (b) Ingawa Wakristo katika Smirna walikuwa maskini, ni kwa nini Yesu alisema wao walikuwa ‘matajiri’?
3 “Mimi najua dhiki na umaskini wako—lakini wewe u tajiri—na kufuru la wale ambao husema wao wenyewe ni Wayahudi, na kumbe wao sio bali ni sinagogi la Shetani.” (Ufunuo 2:9, NW) Yesu hana uchambuzi kwa ndugu zake katika Smirna, ana pongezi changamfu tu. Wao wamepatwa na dhiki nyingi sana kwa sababu ya imani yao. Kimwili wao ni maskini, yaelekea kwa sababu ya uaminifu wao. (Waebrania 10:34) Hangaikio lao kuu, hata hivyo, ni vitu vya kiroho, nao wamejiwekea akiba hazina katika mbingu, kama Yesu alivyoshauri. (Mathayo 6:19, 20) Kwa sababu hiyo, Mchungaji Mkuu anawaona wao kuwa “tajiri.”—Linga Yakobo 2:5.
4. Wakristo katika Smirna walipatwa na upinzani mwingi sana kutoka kwa nani, naye Yesu aliwaonaje wapinzani hao?
4 Yesu anataja hasa kwamba Wakristo katika Smirna wamechukuana na upinzani mwingi mikononi mwa Wayahudi wa kimnofu. Katika siku za mapema zaidi, wengi wa dini hii walipinga kwa dhati kuenea kwa Ukristo. (Matendo 13:44, 45, 14:19) Sasa, miongo michache tu baada ya Yerusalemu kuanguka, Wayahudi hao katika Smirna wanaonyesha roho ile ile ya kishetani. Si ajabu kwamba Yesu anawaona hao kuwa “sinagogi la Shetani”!a
5. Ni majaribu gani yaliyokuwa mbele kwa ajili ya Wakristo katika Smirna?
5 Wakikabiliwa na chuki kama hiyo, Wakristo katika Smirna wanafarijiwa na Yesu hivi: “Usiwe mwenye kuogopa vitu ambavyo wewe u karibu kupatwa navyo. Tazama! Ibilisi atafuliza kutupa baadhi ya nyinyi ndani ya gereza ili nyinyi mtiwe kenyekenye kwenye mtihani, na ili nyinyi muwe na dhiki siku kumi. Jithibitishe mwenyewe kuwa mwaminifu mpaka hata kifo, na mimi nitakupa wewe taji la uhai.” (Ufunuo 2:10, NW) Hapa Yesu mara tatu anatumia namna ya wingi wa Kigiriki kwa “nyinyi,” kuonyesha kwamba maneno yake yanatia ndani kundi kwa ujumla. Yesu hawezi kuahidi kwamba majaribu ya Wakristo katika Smirna yatakoma karibuni. Baadhi yao wataendelea kunyanyaswa na kutupwa gerezani. Wao watakuwa na dhiki kwa “siku kumi.” Kumi ni nambari ambayo huonyesha ukamili au uzima wote wa kidunia. Hata hao washika ukamilifu walio matajiri kiroho watapokea kutahiniwa kikamili wakati wamo katika mnofu.
6. (a) Ni kwa nini Wakristo katika Smirna hawakupaswa kuogopa? (b) Yesu alimaliziaje ujumbe wake kwa kundi katika Smirna?
6 Hata hivyo, hao Wakristo katika Smirna hawapaswi kuogopa au kuacha msimamo wao. Ikiwa wao wanabaki waaminifu mpaka mwisho, wamewekewa “taji la uhai” kuwa thawabu, kwao ikiwa ni uhai usioweza kufa katika mbingu. (1 Wakorintho 9:25; 2 Timotheo 4:6-8, NW) Mtume Paulo aliiona zawadi hii yenye thamani kubwa kuwa inastahili kudhabihiwa kila kitu kinginecho chote, hata uhai wake wa kidunia. (Wafilipi 3:8) Kwa wazi, hao waaminifu katika Smirna wanahisi jinsi iyo hiyo. Yesu anamalizia ujumbe wake kwa kusema: “Acheni yeye ambaye ana sikio asikie ambacho roho husema kwa makundi: Yeye ambaye hushinda hatadhuriwa kwa vyovyote na kifo cha pili.” (Ufunuo 2:11, NW) Washindi wanahakikishiwa uhai wa kimbingu usioweza kufa ambao hauwezi kuguswa na kifo.—1 Wakorintho 15:53, 54.
“Dhiki Siku Kumi”
7, 8. Kama vile kundi katika Smirna, kundi la Kikristo ‘lilitiwaje kenyekenye kwenye mtihani’ katika 1918?
7 Sawasawa na Wakristo katika Smirna, ile jamii ya Yohana na waandamani wao leo wamekuwa na wanaendelea “kutiwa kenyekenye kwenye mtihani.” Uaminifu wao chini ya jaribu huwatia alama ya kuwa watu wa Mungu mwenyewe. (Marko 13:9, 10) Muda mfupi baada ya siku ya Bwana kuanza, maneno ya Yesu kwa Wakristo katika Smirna yalileta faraja halisi kwa kikundi kidogo cha kimataifa cha watu wa Yehova. (Ufunuo 1:10) Tangu 1879, hao walikuwa wamekuwa wakichimbua kutoka Neno la Mungu utajiri wa kiroho ambao wao walishiriki na wengine bila malipo. Lakini wakati wa Vita ya Ulimwengu 1, walikutana na chuki na upinzani mkali, kwa sehemu kwa sababu wao hawakujitia katika ile harara ya vita na kwa sehemu kwa sababu wao walikuwa wakifunua wazi bila woga makosa ya Jumuiya ya Wakristo. Ule mnyanyaso ambao wao walipokea ukichochewa na baadhi ya viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo ulifikia upeo katika 1918 na ulilinganika na ule waliopokea Wakristo katika Smirna kutoka jamii ya Kiyahudi iliyokuwa huko.
8 Wimbi moja la mnyanyaso katika United States ya Amerika lilifikia upeo wakati yule msimamizi mpya wa Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi, Joseph F. Rutherford, na washiriki saba walipelekwa kwenye gereza katika Juni 22, 1918, walio wengi wao wakiwa na hukumu za kifungo cha miaka 20. Waliachiliwa kwa dhamana miezi tisa baadaye. Mei 14, 1919, mahakama ya rufani ilibadili hatia walizowekewa kimakosa; ilionyeshwa kulikuwako makosa 130 katika jaribio hilo. Jaji Manton, Mroma Katoliki, mwenye daraja la utawa wa Mtakatifu Gregori Mkuu, ambaye katika 1918 alikuwa amekataa dhamana kwa hao Wakristo, baadaye katika 1939, alihukumiwa kifungo cha miaka miwili na faini ya dola 10,000 kwa mashtaka sita ya kuomba na kupokea rushwa.
9. Mashahidi wa Yehova katika Ujeremani wa Nazi walitendwaje na Hitla, na kukiwa tendo-mwitikio gani kutoka viongozi wa kidini?
9 Wakati wa utawala wa Nazi katika Ujeremani, Hitla alipiga marufuku kabisa kabisa kazi ya kuhubiri ya Mashahidi wa Yehova. Kwa miaka kadhaa, maelfu ya Mashahidi walifungwa ndani ya kambi za mateso na magereza kikatili, ambako wengi walikufa, huku wanaume vijana 200 ambao walikataa kupigana katika jeshi la Hitla wakifishwa kwa amri ya serikali. Uungaji-mkono wa viongozi wa kidini wa yote haya unathibitishwa na maneno ya padri Mkatoliki, yaliyochapishwa katika ile nyusipepa The German Way ya Mei 29, 1938. Kwa sehemu, yeye alisema: “Sasa kuna nchi moja duniani ambako wale wanaoitwa eti . . . Wanafunzi wa Biblia [Mashahidi wa Yehova] wamekatazwa. Hiyo ni Ujeremani! . . . Wakati Adolf Hitla alipochukua mamlaka, nayo Episkopati ya Kikatoliki katika Ujeremani ikarudia ombi lao, Hitla akasema: ‘Hawa wanaoitwa eti Wanafunzi wa Biblia [Mashahidi wa Yehova] Wenye Bidii ni wafanyiza matata; . . . mimi nawaona kuwa wadanganyaji; mimi sivumilii kwamba Wakatoliki Wajeremani watatupiwa matope jinsi hiyo na huyu Mwamerika Jaji Rutherford. Mimi nafumua [Mashahidi wa Yehova] katika Ujeremani.’” Kwa hayo, yule padri akaongeza: “Hongera!”
10. (a) Kadiri ile siku ya Bwana imeendelea, Mashahidi wa Yehova wamekabili mnyanyaso gani? (b) Mara nyingi tokeo lilikuwa nini wakati Wakristo walipopigania uhuru wa kidini katika mahakama?
10 Kadiri ile siku ya Bwana imesonga mbele, yule Nyoka na mbegu yake hawakukoma kamwe kupiga vita dhidi ya Wakristo wapakwa-mafuta na waandamani wao. Wengi wa hawa wametiwa gerezani na kunyanyaswa kikatili sana. (Ufunuo 12:17) Maadui hao wameendelea ‘kutunga madhara kwa njia ya sheria,’ lakini watu wa Yehova kwa uthabiti husisitiza: “Ni lazima sisi tutii Mungu kuwa mtawala kuliko wanadamu.” (Zaburi 94:20; Matendo 5:29, NW) Katika 1954 gazeti Mnara wa Mlinzi liliripoti: “Zaidi ya nchi sabini katika wakati mmoja au mwingine katika muda wa miaka arobaini iliyopita zimefanyiza amri zuifu nazo zimenyanyasa Mashahidi wa Yehova.” Mahali ambako imewezekana kupigania uhuru wa kidini katika mahakama, Wakristo hawa wamefanya hivyo na katika nchi kadha wa kadha wamepata ushindi mwingi wenye mshindo mkubwa. Katika Mahakama Kuu Zaidi ya United States pekee, Mashahidi wa Yehova wameshinda maamuzi 50 yenye kupendeleka.
11. Ni unabii gani wa Yesu kuhusu ile ishara ya kuwapo kwake ambao umetimizwa juu ya Mashahidi wa Yehova wakati wa hii siku ya Bwana?
11 Hakuna kikundi kinginecho chote kimekuwa chenye kudhamiria kadiri hiyo katika kutii amri ya Yesu ya kulipa Kaisari vitu vya Kaisari. (Luka 20:25; Warumi 13:1, 7) Hata hivyo, hakuna kikundi kinginecho chote kimekuwa na washiriki waliotiwa gerezani katika mabara mengi hivyo chini ya namna nyingi hivyo mbalimbali za serikali, na jambo hili linaendelea mpaka wakati uu huu katika zile bara za Amerika, katika Europa, katika Afrika, na katika Esia. Unabii mkubwa wa Yesu kuhusu ile ishara ya kuwapo kwake ulitia ndani maneno haya: “Kisha watu watakabidhi nyinyi katika dhiki na wataua nyinyi, na nyinyi mtakuwa vitu vya kuchukiwa na mataifa yote kwa sababu ya jina langu.” (Mathayo 24:3, 9, NW) Bila shaka hilo limetimizwa juu ya Mashahidi Wakristo wa Yehova wakati wa hii siku ya Bwana.
12. Jamii ya Yohana imeimarishaje watu wa Mungu dhidi ya mnyanyaso?
12 Ili kuwaimarisha watu wa Mungu dhidi ya dhiki, ile jamii ya Yohana kwa kuendelea imewakumbusha maana ya maneno ya Yesu kwa Wakristo katika Smirna. Kwa mfano, mnyanyaso wa Kinazi ulipoanza, Mnara wa Mlinzi katika 1933 na 1934 ulikuwa na makala kama vile “Msiwaogope,” ambayo ilizungumzia Mathayo 10:26-33; “Lile Tanuri,” iliyotegemea Danieli 3:17, 18; na “Makanwa ya Simba,” Danieli 6:22 lilikuwa andiko kuu. Katika miaka ya muda wa tangu 1980, mwongo ambao katika huo kitabu hiki kilichapishwa kwa mara ya kwanza na Mashahidi wa Yehova wakanyanyaswa vikali katika mabara zaidi ya 40, Mnara wa Mlinzi uliimarisha watu wa Mungu kwa makala kama vile “Wenye Furaha Wajapoteswa!” na “Wakristo Wanaelekeana na Mateso kwa Uvumilivu.”b
13. Kama vile Wakristo katika Smirna, ni kwa nini Mashahidi Wakristo wa Yehova hawajakuwa wakiogopa mnyanyaso?
13 Kweli kweli, Mashahidi wa Yehova Wakristo wanapata mnyanyaso wa kimwili na mitihani mingine kwa siku kumi za mfano. Kama vile Wakristo huko nyuma katika Smirna, wao hawakuwa wakiogopa; wala hakuna yeyote wetu anayehitaji kuogopa taabu zizidipo kuwa mbaya hapa duniani. Sisi tuko tayari kuvumilia chini ya mateso na hata ‘kukubali kunyang’anywa mali zetu kwa furaha.’ (Waebrania 10:32-34) Kwa kujifunza Neno la Mungu na kulifanya liwe letu wenyewe, sisi tutatayarishwa tusimame tukiwa thabiti katika imani. Uwe na hakika kwamba Yehova anaweza kulinda na atalinda wewe katika ukamilifu wako. ‘Tupia yeye mahangaiko yako yote, kwa sababu yeye anakujali wewe.’—1 Petro 5:6-11, NW.
[Maelezo ya Chini]
a Yapata miaka 60 baada ya Yohana kufa, Polycarp mwenye umri wa miaka 86 aliteketezwa mpaka kifo katika Smirna kwa sababu yeye hangeweza kukana itikadi yake katika Yesu. The Martyrdom of Polycarp, kitabu kinachoitikadiwa kuwa cha wakati ule ule mmoja na tukio hili, hutaarifu kwamba wakati kuni zilipokuwa zikikusanywa za kuteketeza yeye, “wale Wayahudi walikuwa na bidii kupita kiasi, kama ilivyo desturi yao, katika kusaidia katika hili”—hata ingawa kufishwa huko kulitukia katika “siku kubwa ya Sabato.”
b Ona The Watchtower ya Novemba 1, 1933; Oktoba 1 na 15, Desemba 1 na 15, 1934; Mnara wa Mlinzi Oktoba 1, 1983.
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 39]
Kwa miaka mingi, wanahistoria wamekuwa wakiandaa ushahidi kuhusu ukamilifu wa Mashahidi wa Yehova Wajeremani wakati wa utawala wa Nazi. Kitabu Mothers in the Fatherland, cha mwanahistoria Claudia Koonz, kilichochapishwa 1986, kinasema: “Idadi iliyo kubwa sana ya Wajeremani wote kutoka asili zisizo za Kinazi walipata njia za kuishi chini ya utawala waliodharau. . . . Kwenye ule upande mwingine wa spektra ya kitakwimu na ya kiitikadi walikuwako Mashahidi wa Yehova 20,000, ambao, karibu kila mmoja wao, walikataa katakata kutoa namna yoyote ya utii kwa serikali ya Nazi. . . . Kikundi chenye kushikamana zaidi ya vyote cha wakinzani kilitegemezwa na dini. Tangu mwanzo, Mashahidi wa Yehova hawakushirikiana na sehemu yoyote ya serikali ya Nazi. Hata baada ya Gestapo kuharibu makao makuu yao ya taifa katika 1933 na wakapiga marufuku farakano hilo katika 1935, wao walikataa kufanya jambo hata lililo dogo kama vile kusema ‘Heil Hitler.’ Wapatao nusu (zaidi wakiwa wanaume) wa Mashahidi wa Yehova wote walipelekwa kwenye kambi za mateso, elfu moja yao walifishwa, na elfu nyingine ikafa kati ya 1933 na 1945. . . . Wakatoliki na Waprotestanti walisikia viongozi wao wa kidini wakiwahimiza washirikiane na Hitla. Ikiwa wao walipinga, wao walifanya hivyo kinyume cha maagizo kutoka kwa kanisa na serikali pia.”