Sura 4
Mwenye Mimba Lakini Bado Kuolewa
MARIAMU yuko katika mwezi wake wa tatu wa kuchukua mimba. Utakumbuka kwamba wakati wa sehemu ya kwanza ya mimba yake aliutumia akimtembelea Elisabeti, lakini sasa amekwisha rudi nyumbani Nazareti. Karibuni hali yake itajulikana na watu wote katika mji wa kwao. Hakika, yeye yuko katika hali ya kuhangaisha!
Jambo linalofanya hali hiyo iwe baya zaidi ni kwamba Mariamu amechumbiwa awe mke wa seremala Yusufu. Naye ajua kwamba, chini ya sheria ya Mungu kwa Israeli, mwanamke ambaye amechumbiwa na mwanamume mmoja, lakini ambaye kwa kupenda anafanya ngono na mwanamume mwingine, apaswa kupigwa mawe afe. Anaweza kumwelezaje Yusufu alivyopata mimba?
Kwa kuwa Mariamu amekuwa safarini miezi mitatu, tunaweza kuwa na hakika Yusufu anataka sana kumwona. Wanapokutana, inaelekea Mariamu amweleza habari hizo. Huenda akafanya yote awezayo kueleza kwamba mimba yake ni kupitia roho takatifu ya Mungu. Lakini, kama unavyoweza kuwazia, hilo ni jambo gumu sana kwa Yusufu kuelewa.
Yusufu ajua Mariamu ana sifa njema. Na ni wazi ampenda sana. Lakini, yajapokuwa anayodai, kwa kweli inaonekana kama kwamba mimba hiyo ni ya mwanamume fulani. Hata hivyo, Yusufu hataki Mariamu apigwe mawe auawe wala aaibishwe mbele ya watu wote. Kwa hiyo aamua kumtaliki kisiri. Katika siku hizo, watu waliochumbiana walionwa kama wameoana, na talaka ilitakiwa ili kumaliza uchumba.
Baadaye, Yusufu akiwa angali anafikiria mambo hayo, alala usingizi. Malaika wa Yehova amtokea katika ndoto na kusema: ‘Usiogope kumchukua Mariamu nyumbani awe mke wako, kwa sababu ana mtoto kupitia roho takatifu ya Mungu. Nawe wapaswa kumwita mtoto huyo jina lake Yesu, kwa sababu atawaokoa watu wake katika dhambi zao.’
Yusufu aamkapo, ashukuru kama nini! Bila kukawia afanya sawasawa na malaika alivyoelekeza. Ampeleka Mariamu nyumbani kwake. Tendo hilo linalofanywa waziwazi mbele ya watu, linakuwa kama sherehe ya kufunga ndoa, likijulisha kwamba Yusufu na Mariamu sasa wamefunga ndoa rasmi. Lakini Yusufu hafanyi ngono na Mariamu maadamu ana mimba ya Yesu.
Tazama! Mariamu ni mja-mzito, na bado Yusufu amweka juu ya punda. Waenda wapi, na ni kwa nini wafunga safari wakati Mariamu yuko karibu kuzaa? Luka 1:39-41, 56; Mathayo 1:18-25; Kumbukumbu 22:23, 24.
▪ Yusufu ana hali gani ya akili anapojua habari za mimba ya Mariamu, na kwa nini?
▪ Yusufu awezaje kumtaliki Mariamu wakati hawajafunga ndoa?
▪ Ni tendo gani la waziwazi linalotumika kuwa sherehe ya ndoa ya Yusufu na Mariamu?