Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w85 9/15 kur. 8-9
  • Mwenye Mimba Lakini Bado Kuolewa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mwenye Mimba Lakini Bado Kuolewa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Habari Zinazolingana
  • Mwenye Mimba Lakini Bado Kuolewa
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Maria​—Ana Mimba Lakini Hajaolewa
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Mfano wa Maria Unatufundisha Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • “Tazama! Kijakazi wa Yehova!”
    Igeni Imani Yao
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
w85 9/15 kur. 8-9

Maisha na Huduma ya Yesu

Mwenye Mimba Lakini Bado Kuolewa

MARIAMU yuko katika mwezi wake wa tatu wa kuchukua mimba. Utakumbuka kwamba wakati wa sehemu ya kwanza ya mimba yake aliutumia akimtembelea Elisabeti, lakini sasa amekwisha kurudi nyumbani Nazareti. Karibuni hali yake itajulikana na watu wote katika mji wa kwao. Hakika, yeye yuko katika hali ya kuhangaisha!

Jambo linaloharibu zaidi hali yenyewe ni kwamba Mariamu amechumbiwa awe mke wa seremala Yusufu. Na anajua kwamba, chini ya sheria ya Mungu kwa Israeli, mwanamke aliyechumbiwa na mwanamume mmoja, lakini ambaye kwa kupenda anafanya ngono na mwanamume mwingine, anapaswa kupigwa mawe afe. Anaweza kumwelezaje Yusufu alivyopata mimba?

Kwa kuwa Mariamu amekuwa safarini miezi mitatu, tunaweza kuwa na uhakika Yusufu anataka sana kumwona. Wanapokutana, inaelekea Mariamu anamweleza habari hizo. Huenda akafanya yote awezayo kueleza kwamba mimba yake ni kupitia roho takatifu ya Mungu. Lakini, kama unavyoweza kuwazia, hilo ni jambo gumu sana kwa Yusufu kuelewa.

Yusufu anajua Mariamu ana sifa njema. Na ni wazi anampenda sana. Lakini, yajapokuwa anayodai, kwa kweli inaonekana kama kwamba mimba hiyo ni ya mwanamume fulani. Hata hivyo, Yusufu hataki Mariamu apigwe mawe auawe wala aaibishwe mbele ya watu wote. Kwa hiyo anaamua kumtaliki kisiri. Katika siku hizo, watu waliopatana uchumba walionwa kama waliooana, na talaka ilitakiwa ili kumaliza uchumba.

Baadaye, Yusufu anapofikiria mambo hayo, analala. Malaika wa Yehova amtokea katika ndoto na kusema: ‘Usiogope kumchukua Mariamu nyumbani awe mkeo, kwa sababu ana mtoto kupitia roho takatifu ya Mungu. Nawe unapaswa kumwita mtoto huyo Yesu, kwa sababu atawaokoa watu wake katika dhambi zao.’

Yusufu anapoamka, anashukuru kama nini! Bila kukawia anafanya sawa na malaika alivyoelekeza. Anampeleka Mariamu nyumbani mwake. Kama ilivyo, tendo hilo la mbele ya watu, linakuwa kama sherehe ya kufunga ndoa, likijulisha kwamba Yusufu na Mariamu sasa wamefunga ndoa rasmi. Lakini Yusufu hafanyi ngono na Mariamu maadamu ana mimba ya Yesu.

Tazama! Mariamu amekuwa mja-mzito, na bado Yusufu anamweka juu ya punda. Wanaenda wapi, na ni kwa sababu gani wanafunga safari wakati Mariamu yuko karibu kuzaa? Luka 1:39-41, 56; Mathayo 1:18-25; Kumbukumbu la Torati 22:23, 24.

◆ Yusufu alikuwa na maoni gani akilini alipojua juu ya mimba ya Mariamu, na kwa sababu gani?

◆ Ingewezekanaje Yusufu amtaliki Mariamu kwa kuwa hawakuwa wameoana?

◆ Ni tendo gani la mbele ya watu lililokuwa sherehe ya ndoa ya Yusufu na Mariamu?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki