Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gt sura 6
  • Mtoto wa Ahadi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mtoto wa Ahadi
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Habari Zinazolingana
  • Mtoto wa Ahadi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Mtoto Aliyeahidiwa
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Alikata “Kauli Moyoni Mwake”
    Igeni Imani Yao
  • Alikata “Kauli Moyoni Mwake”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
Pata Habari Zaidi
Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
gt sura 6

Sura 6

Mtoto wa Ahadi

BADALA ya kurudi Nazareti, Yusufu na Mariamu wakaa Bethlehemu. Na Yesu anapokuwa na umri wa siku nane wamtahiri, kulingana na amri ya Sheria ya Mungu aliyompa Musa. Ni wazi pia ni desturi kumpa mtoto mvulana jina lake siku ya nane. Kwa hiyo wamwita mtoto wao Yesu, kama vile malaika Gabrieli alivyokuwa ameelekeza mapema kidogo.

Zaidi ya mwezi mmoja wapita, na Yesu ana umri wa siku 40. Sasa wazazi wake wampeleka wapi? Kwenye hekalu katika Yerusalemu, ambalo liko kilometa chache tu kutoka mahali wanapoishi. Kulingana na Sheria ya Mungu aliyompa Musa, siku 40 baada ya kuzaa mwana, mama apaswa kutoa sadaka ya utakaso hekaluni.

Ndivyo Mariamu anafanya. Ikiwa sadaka yake, yeye aleta ndege wawili wadogo. Jambo hilo latuonyesha hali ya kiuchumi ya Yusufu na Mariamu. Sheria ya Musa huonyesha kwamba kondoo mume mchanga, ambaye ni mwenye thamani zaidi ya ndege, apaswa kutolewa sadaka. Lakini ikiwa mama hangeweza kumnunua, njiwa au hua wawili wangetosha.

Huko hekaluni mwanamume mmoja mzee amchukua Yesu mikononi mwake. Jina lake ni Simeoni. Mungu amekwisha kumfunulia kwamba hatakufa kabla ya kuona Kristo, au Mesiya wa Yehova aliyeahidiwa. Simeoni anapokuja hekaluni siku hiyo, aelekezwa na roho takatifu kwenda alipo mtoto huyo anayebebwa mikononi na Yusufu na Mariamu.

Simeoni akiwa amemchukua Yesu mikononi amshukuru Mungu, akisema: “Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, kwa amani, kama ulivyosema; kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako, uliouweka tayari machoni pa watu wote; nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.”

Yusufu na Mariamu wastaajabu kusikia hayo. Halafu Simeoni awabariki na kumwambia Mariamu kwamba mwanaye “amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli” na kwamba huzuni, kama upanga mkali, itachoma nafsi yake.

Katika pindi hiyo yupo nabii wa kike mwenye umri wa miaka 84 aitwaye Ana. Kwa kweli, hakosi kamwe hekaluni. Saa iyo hiyo akaribia na kuanza kumtolea Mungu shukrani na kusema juu ya Yesu kwa wote watakaosikiliza.

Matukio hayo ya hekaluni yamefanya Yusufu na Mariamu wafurahi kama nini! Hakika, jambo hilo lawathibitishia kwamba mtoto huyo ndiye Mwahidiwa wa Mungu. Luka 2:21-38; Walawi 12:1-8.

▪ Kwa wazi ni wakati gani ilikuwa desturi kumpa mtoto mvulana Mwisraeli jina lake?

▪ Mama Mwisraeli alipaswa kufanya nini mwanaye alipokuwa na umri wa siku 40, na kutimizwa kwa takwa hilo kwaonyeshaje ilivyo hali ya kiuchumi ya Mariamu?

▪ Ni nani wafahamu utambulisho wa Yesu katika pindi hiyo, nao wafanyaje hivyo?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki