Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gt sura 12
  • Ubatizo wa Yesu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ubatizo wa Yesu
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Habari Zinazolingana
  • Yesu Abatizwa
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Ubatizo wa Yesu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Yohana Anambatiza Yesu
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Maana ya Ubatizo Wako
    Mwabudu Mungu wa Pekee wa Kweli
Pata Habari Zaidi
Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
gt sura 12

Sura 12

Ubatizo wa Yesu

YAPATA miezi sita baada ya Yohana kuanza kuhubiri, Yesu, ambaye sasa ana umri wa miaka 30, aja kwake katika Yordani. Kwa sababu gani? Je! ni ili amtembelee kirafiki? Je! Yesu apendezwa tu na kuona jinsi kazi ya Yohana inavyoendelea? La, Yesu amwomba Yohana ambatize.

Mara hiyo Yohana apinga: “Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?” Yohana ajua kwamba binamu yake Yesu ni Mwana wa pekee wa Mungu. Kwani, Yohana alikuwa ameruka kwa furaha kuu akiwa katika tumbo la mamaye wakati Mariamu, akiwa na mimba ya Yesu alipowatembelea! Bila shaka, Elisabeti, mama ya Yohana, alimwambia jambo hilo baadaye. Na angekuwa amemwambia pia juu ya tangazo la malaika kuhusu kuzaliwa kwa Yesu na vile malaika walivyowatokea wachungaji katika usiku ule Yesu alizaliwa.

Kwa hiyo Yesu si mtu asiyejulikana kwa Yohana. Na Yohana ajua kwamba ubatizo wake haumfai Yesu. Ni wa wale wanaotubia dhambi zao, lakini Yesu hana dhambi. Hata hivyo, Yohana ajapopinga, Yesu asisitiza: “Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.”

Kwa nini yafaa Yesu apatizwe? Kwa sababu ubatizo wa Yesu ni ufananisho, si wa kutubia dhambi, bali wa kujitolea kwake afanye mapenzi ya Baba yake. Yesu amekuwa seremala, lakini sasa wakati umefika aanze huduma ile ambayo Yehova Mungu alimtuma duniani aifanye. Je! wadhani Yohana anatarajia jambo lisilo la kawaida litukie anapombatiza Yesu?

Basi, baadaye Yohana aripoti hivi: “Yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka [roho ikishuka juu yake, NW] huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu [roho takatifu, NW].” Kwa hiyo Yohana atarajia roho ya Mungu ishuke na kukaa juu ya mtu fulani ambaye anabatiza. Kwa hiyo, labda, kwa kweli yeye hashangai wakati, Yesu apandapo kutoka katika maji, Yohana aona ‘kama hua roho ya Mungu ikishuka juu yake.’

Lakini mengi zaidi ya hayo yatukia wakati Yesu anapobatizwa. ‘Mbingu zamfunukia.’ Hiyo yamaanisha nini? Kwa wazi yamaanisha kwamba huku akiwa anabatizwa, kumbukumbu la kuwako kwake kabla ya kuwa binadamu katika mbingu lamrudia. Hivyo, Yesu sasa akumbuka kabisa maisha yake akiwa mwana wa kiroho wa Yehova Mungu, kutia na mambo yote ambayo Mungu alimwambia mbinguni wakati wa kuwako kwake kabla ya kuwa binadamu.

Kwa kuongezea, wakati wa ubatizo wake, sauti kutoka mbinguni yajulisha: “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.” Sauti hiyo ni ya nani? Je! ni sauti ya Yesu mwenyewe? Bila shaka sivyo! Ni ya Mungu. Kwa wazi, Yesu ni Mwana wa Mungu, si Mungu mwenyewe, kama vile watu fulani hudai.

Lakini, Yesu ni mwana wa kibinadamu wa Mungu, kama vile alivyokuwa mwanamume wa kwanza, Adamu. Mwanafunzi Luka, baada ya kueleza ubatizo wa Yesu, aandika hivi: ‘Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri wake kama miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, mwana wa Eli, . . . mwana wa Daudi, . . . mwana wa Abrahamu, . . . mwana wa Noa, . . . mwana wa Adamu, mwana wa Mungu.’

Kama vile Adamu alivyokuwa ‘mwana wa Mungu’ wa kibinadamu, ndivyo na Yesu. Yesu ndiye mtu mkuu kuliko wote aliyepata kuishi, jambo ambalo lawa wazi tuchunguzapo maisha ya Yesu. Hata hivyo, wakati wa ubatizo wake, Yesu aingia katika uhusiano mpya na Mungu, awa Mwana wa Mungu wa kiroho pia. Sasa Mungu amwita arudi mbinguni, kwa kumwanzisha katika mwendo utakaomwongoza kwenye kutoa uhai wake wa kibinadamu milele katika dhabihu kwa ajili ya aina ya kibinadamu iliyohukumiwa kifo. Mathayo 3:13-17; Luka 3:21-38; 1:34-36, 44; 2:10-14; Yohana 1:32-34; Wae-brania 10:5-9.

▪ Kwa nini Yesu si mtu asiyejulikana kwa Yohana?

▪ Kwa kuwa hakutenda dhambi zozote, kwa nini Yesu abatizwa?

▪ Kwa sababu ya yale ambayo Yohana anajua kuhusu Yesu, kwa nini huenda asishangae roho ya Mungu ishukapo juu ya Yesu?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki