Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w85 11/1 kur. 30-31
  • Ubatizo wa Yesu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ubatizo wa Yesu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Habari Zinazolingana
  • Ubatizo wa Yesu
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Yesu Abatizwa
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Yesu Anakuwa Masihi
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Yohana Anambatiza Yesu
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
w85 11/1 kur. 30-31

Maisha na Huduma ya Yesu

Ubatizo wa Yesu

KARIBU miezi sita baada ya Yohana kuanza kuhubiri, Yesu, ambaye sasa ana umri wa miaka 30, anamjia kwenye Yordani. Kwa sababu gani? Je! ni kumtembelea kirafiki? Je! Yesu anataka kuona tu jinsi kazi ya Yohana inavyoendelea? Hapana, Yesu anamwomba Yohana ambatize.

Bila kukawia Yohana anakataa. “Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?” anamuuliza. Yohana anajua kwamba Yesu binamu yake ni Mwana maalum wa Mungu. Kwani, Yohana aliruka kwa furaha akiwa tumboni mwa mamaye wakati Mariamu alipowatembelea, akiwa amemchukua Yesu mimba! Bila shaka Yohana aliambiwa hayo baadaye na Elisabeti mamaye. Pia alimwambia juu ya tangazo lililotolewa na malaika juu ya kuzaliwa kwa Yesu na jinsi malaika walivyowatokea wachungaji usiku aliozaliwa.

Kwa hiyo Yesu si mtu mgeni kwa Yohana. Naye Yohana anajua kwamba ubatizo anaobatiza watu haumpasi Yesu. Ni wa wale wanaotubu kwa sababu ya dhambi zao, lakini Yesu hana dhambi. Hata hivyo, ijapokuwa Yohana anakataa, Yesu anasisitiza hivi: “Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.”

Kwa sababu gani inafaa Yesu abatizwe? Kwa sababu ubatizo wa Yesu ni mfano, si wa toba kwa ajili ya dhambi, bali wa kujitoa kwake afanye mapenzi ya Baba yake. Yesu alikuwa seremala, lakini sasa wakati umefika aianze huduma ambayo Mungu alimtuma duniani aifanye. Je! wewe unafikiri Yohana alitazamia jambo lo lote lisilo la kawaida litukie wakati alipombatiza Yesu?

Baadaye Yohana aliripoti: “Yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona [roho ikishuka] na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa [roho takatifu].” Kwa hiyo Yohana alikuwa akiitazamia roho ya Mungu ije juu ya mtu fulani ambaye yeye angebatiza. Basi, labda yeye hakushangaa sana wakati ‘roho ya Mungu iliposhuka kama hua’ juu ya Yesu alipokuwa akitoka ndani ya maji.

Lakini si hayo tu yaliyotukia kwenye ubatizo wa Yesu. Yesu alifunguliwa mbingu, na sauti ikasema: “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.” Hiyo ilikuwa sauti ya nani? Je! ni sauti ya Yesu mwenyewe? Bila shaka sivyo! Ilikuwa ya Mungu. Kwa wazi, Yesu ni Mwana wa Mungu, wala siye Mungu mwenyewe, kama vile watu wengi wanavyodai. Mathayo 3:13-17; Luka 3:21-23; 1:34-36, 44; 2:10-14; Yohana 1:32-34;

◆ Kwa sababu gani Yesu hakuwa mtu mgeni kwa Yohana?

◆ Kwa sababu Yesu hakuwa ametenda dhambi zo zote, kwa sababu gani alibatizwa?

◆ Kwa sababu ya yale ambayo Yohana alijua juu ya Yesu, kwa sababu gani huenda akawa hakushangaa wakati roho ya Mungu ilipokuja juu ya Yesu?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki