Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gt sura 31
  • Kuvunja Masuke Siku ya Sabato

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuvunja Masuke Siku ya Sabato
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Habari Zinazolingana
  • Kuvunja Masuke Siku ya Sabato
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Wakata Masuke ya Nafaka Siku ya Sabato
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Je, Wakristo Wanapaswa Kushika Sabato?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Sabato
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
Pata Habari Zaidi
Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
gt sura 31

Sura 31

Kuvunja Masuke Siku ya Sabato

BAADA ya muda mfupi Yesu na wanafunzi wake waondoka Yerusalemu kurudi Galilaya. Ni wakati wa masika, na mashambani kuna masuke ya nafaka. Wanafunzi wana njaa. Kwa hiyo wanavunja masuke na kuyala. Lakini kwa kuwa ni Sabato, vitendo vyao havipiti bila kuonwa.

Viongozi wa kidini katika Yerusalemu walikuwa wamejaribu kumwua Yesu muda mfupi tu kabla ya hapo ikisemekana kwamba yeye alikuwa amekosa kufuata Sabato. Sasa, Mafarisayo waleta shtaka. “Tazama! Wanafunzi wako wanafanya neno ambalo si halali kulifanya siku ya sabato,” wao wanashtaki.

Mafarisayo wanadai kwamba kuvunja masuke na kufikicha zile punje mikononi ili kuzila ni kuvuna na kupura. Lakini fasiri yao kali juu ya kile ambacho ni kazi imefanya Sabato iwe mzigo, hali ilikusudiwa iwe wakati wa shangwe, wenye kujenga kiroho. Kwa hiyo Yesu anapinga kwa kutumia mifano ya Kimaandiko kuonyesha kwamba Yehova Mungu hakukusudia kamwe sheria Yake ya Sabato itumiwe vikali hivyo bila sababu.

Yesu anasema kwamba wakati Daudi na watu wake walipokuwa na njaa, walitua kwenye hema takatifu, wakaila mikate ya wonyesho. Mikate hiyo ilikuwa tayari imeondolewa mbele ya Yehova na mingine mipya ikawekwa badala yayo, na kwa kawaida makuhani ndio waliowekewa waile. Hata hivyo, chini ya hali hizo, Daudi na watu wake hawakushutumiwa kwa sababu ya kuila.

Akiandaa kielelezo kingine, Yesu anasema: “Hamkusoma katika torati kwamba, siku ya sabato makuhani hekaluni huinajisi sabato wasipate hatia?” Ndiyo, hata katika siku ya Sabato makuhani wanaendelea kuchinja wanyama na kufanya kazi nyingine hekaluni wanapotayarisha dhabihu za wanyama! “Lakini nawaambieni,” Yesu asema, “kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu.”

Akiwaonya Mafarisayo kwa upole, Yesu anaendelea: “Kama mngalijua maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka, msingaliwalaumu wasio na hatia.” Halafu anamalizia hivi: “Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.” Yesu amaanisha nini kwa kusema hivyo? Yesu anarejezea utawala wake wa Ufalme wenye amani wa miaka elfu moja.

Kwa miaka 6,000 sasa, ainabinadamu wametoa jasho la utumwa wakiwa chini ya Shetani Ibilisi, jeuri na vita yakiwa ndiyo mambo ya kila siku. Kwa upande mwingine, utawala wa ile Sabato kuu wa Kristo utakuwa wakati wa pumziko bila mateso na uonevu huo wote. Mathayo 12:1-8; Walawi 24:5-9; 1 Samweli 21:1-6; Hesabu 28:9; Hosea 6:6.

▪ Ni shtaka gani linalofanywa dhidi ya wanafunzi wa Yesu, naye Yesu analijibuje?

▪ Yesu anatambulisha kosa gani la Mafarisayo?

▪ Ni katika njia gani Yesu ndiye “Bwana wa sabato”?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki