Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • jy sura 31 uku. 76-uku. 77 fu. 2
  • Wakata Masuke ya Nafaka Siku ya Sabato

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wakata Masuke ya Nafaka Siku ya Sabato
  • Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Habari Zinazolingana
  • Kuvunja Masuke Siku ya Sabato
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Kuvunja Masuke Siku ya Sabato
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Je, Wakristo Wanapaswa Kushika Sabato?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Sabato
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
Pata Habari Zaidi
Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
jy sura 31 uku. 76-uku. 77 fu. 2
Wanafunzi wa Yesu wakata masuke na kula nafaka siku ya Sabato

SURA YA 31

Wakata Masuke ya Nafaka Siku ya Sabato

MATHAYO 12:1-8 MARKO 2:23-28 LUKA 6:1-5

  • WANAFUNZI WAKATA MASUKE YA NAFAKA SIKU YA SABATO

  • YESU NDIYE “BWANA WA SABATO”

Sasa Yesu na wanafunzi wake wanasafiri kuelekea kaskazini huko Galilaya. Ni majira ya kuchipua na katika mashamba, mimea imezaa nafaka. Kwa kuwa wanafunzi wana njaa wanakata masuke ya nafaka na kula. Lakini ni siku ya Sabato na Mafarisayo wanaona kile ambacho wanafunzi wanafanya.

Kumbuka kwamba hivi karibuni Wayahudi fulani huko Yerusalemu walitaka kumuua Yesu, wakimshtumu kwamba anavunja Sabato. Sasa Mafarisayo wanaleta mashtaka kuhusu jambo wanalofanya wanafunzi. “Tazama! Wanafunzi wako wanafanya jambo lisilo halali siku ya Sabato.”—Mathayo 12:2.

Mafarisayo wanadai kwamba kukata masuke ya nafaka na kuyapukusa mikononi ili kula, ni kuvuna na kupura. (Kutoka 34:21) Ufafanuzi wao usio na usawaziko kuhusu kazi unafanya Sabato iwe yenye kuchosha, ingawa ilipoanzishwa ilipaswa kuwa siku yenye shangwe na inayojenga kiroho. Yesu anapinga maoni yao yenye makosa kwa kutoa mifano inayoonyesha kwamba Yehova Mungu hakukusudia sheria Yake kuhusu Sabato itekelezwe kwa njia hiyo.

Mfano mmoja ambao Yesu anatoa unahusu Daudi na wanaume waliokuwa pamoja naye. Walipohisi njaa, walisimama kwenye hema la ibada na kula mikate ya wonyesho. Mikate hiyo ambayo ilikuwa tayari imeondolewa mbele za Yehova na badala yake mikate mingine ikawekwa, kwa kawaida ilipaswa kuliwa na makuhani. Hata hivyo, chini ya hali walizokuwa nazo, Daudi na wanaume hao hawakushutumiwa kwa kula mikate hiyo.—Mambo ya Walawi 24:5-9; 1 Samweli 21:1-6.

Yesu anatoa mfano wa pili, anasema: “Je, hamjasoma katika Sheria kwamba siku ya Sabato makuhani huvunja Sabato na wanabaki bila hatia?” Anamaanisha kwamba hata katika siku ya Sabato, makuhani huchinja wanyama kwa ajili ya dhabihu na kufanya kazi nyingine hekaluni. Yesu anasema: “Lakini ninawaambia, hapa pana mtu mkuu kuliko hekalu.”—Mathayo 12:5, 6; Hesabu 28:9.

Tena Yesu anatumia Maandiko kufafanua hoja yake: “Kama mngeelewa maana ya maneno haya, ‘Ninataka rehema si dhabihu,’ hamngewalaumu watu wasio na hatia.” Anamalizia kwa kusema: “Kwa maana Mwana wa binadamu ndiye Bwana wa Sabato.” Yesu anarejezea utawala wake unaokuja wa Ufalme wenye amani wa miaka elfu moja.—Mathayo 12:7, 8; Hosea 6:6.

Kwa muda mrefu, wanadamu wameteseka chini ya utumwa mgumu wa Shetani, uliojaa ukatili na vita. Hali zitakuwa tofauti sana chini ya Sabato kuu ya utawala wa Kristo, ambaye ataandaa muda wa kupumzika tunaotamani na kuhitaji sana!

  • Mafarisayo wanaleta mashtaka gani dhidi ya wanafunzi wa Yesu, na kwa nini?

  • Yesu anarekebishaje maoni ya Mafarisayo?

  • Yesu ni “Bwana wa Sabato” katika njia gani?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki