Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gt sura 43
  • Kufundisha kwa Vielezi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kufundisha kwa Vielezi
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kunufaishwa na Vielezi vya Yesu
  • Wabarikiwa kwa Mafundisho Zaidi
  • Mifano Kuhusu Ufalme
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Kufundisha kwa Mifano
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Wabarikiwa kwa Mafundisho Zaidi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Kunufaika Kutokana na Mifano ya Yesu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
Pata Habari Zaidi
Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
gt sura 43

Sura 43

Kufundisha kwa Vielezi

YESU inaonekana yuko Kapernaumu wakati anapokemea Mafarisayo. Baadaye siku iyo hiyo, yeye anaondoka katika nyumba ile na kutembea kwenda kwenye Bahari ya Galilaya iliyo karibu, ambako umati wa watu unakusanyika. Huko anapanda mashua, aenda mbali kidogo na ufuo, na kuanza kufundisha watu walio ufuoni juu ya Ufalme wa mbingu. Yeye afanya hivyo kupitia kwa mfululizo wa mifano, au vielezi, kila mmoja ukiwa na kikao kinachofahamiwa na watu.

Kwanza, Yesu asimulia juu ya mpanzi anayepanda mbegu. Mbegu fulani zinaanguka kando ya barabara na kuliwa na ndege. Mbegu nyingine zinaanguka juu ya udongo ambao chini yao pana tungamo-mwamba. Kwa kuwa mizizi haina kina, mimea ile mipya inanyauka chini ya jua lenye kuichoma sana. Bado mbegu nyingine zinaanguka miongoni mwa miiba, ambayo inaisonga mimea wakati inapotokeza. Hatimaye, mbegu fulani zinaanguka juu ya udongo mzuri na kuzaa mara 100, nyingine mara 60, na nyingine mara 30.

Katika kielezi kingine Yesu analinganisha Ufalme wa Mungu na mtu anayepanda mbegu. Kadiri siku zipitavyo, wakati mtu yule amelala na wakati ameamka, mbegu ile inakua. Mtu yule hajui inakuaje. Inakua yenyewe tu na kuzaa tete. Wakati nafaka imeiva, mtu yule anaivuna.

Yesu anasimulia kielezi cha tatu juu ya mtu anayepanda mbegu ya aina inayofaa, lakini “huku watu walipokuwa wanalala,” adui anakuja na kupanda magugu miongoni mwa ngano. Watumishi wa mtu yule wanauliza kama inawapasa kung’oa magugu. Lakini yeye anajibu: ‘Hapana, mtang’oa baadhi ya ngano mkifanya hivyo. Acheni vyote viwili vikue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Ndipo mimi nitawaambia wavunaji wachague magugu na kuyateketeza na kuweka ngano katika ghala.’

Akiendelea na hotuba yake kwa umati ulio ufuoni wa bahari, Yesu anaandaa vielezi vingine viwili zaidi. Yeye anaeleza kwamba “ufalme wa mbingu” ni kama punje ya haradali ambayo mtu anapanda. Ingawa hiyo ndiyo mbegu iliyo ndogo sana sana kati ya mbegu zote, yeye anasema, inakua na kuwa mboga iliyo kubwa zaidi ya mboga zote. Inakuwa mti ambao ndege wanaendea, wakipata makao miongoni mwa matawi yao.

Watu fulani leo wanapinga wakisema kwamba kuna mbegu zilizo ndogo sana kuliko mbegu za haradali. Lakini Yesu hatoi somo la elimu-mimea. Kati ya mbegu ambazo Wagalilaya wa siku zake wanafahamu sana, mbegu ya haradali kwa kweli ndiyo iliyo ndogo zaidi ya zote. Kwa hiyo wao wanalithamini jambo la ukuzi wa ajabu sana ambao Yesu anatolea kielezi.

Mwishowe, Yesu analinganisha “ufalme wa mbingu” na chachu ambayo mwanamke amechukua na kuchanganya ndani ya vipimo vitatu vikubwa vya unga. Baada ya muda, yeye anasema, chachu hiyo inaenea kila sehemu ya kinyunya kile.

Baada ya kutoa vielezi hivi vitano, Yesu anaambia umati uende zao kisha yeye anarudi kwenye nyumba anamokaa. Baada ya muda mfupi mitume wake 12 na wengine wanamjia humo.

Kunufaishwa na Vielezi vya Yesu

Wanafunzi wanapomjia Yesu baada ya hotuba yake kwa umati wa watu ufuoni mwa bahari, wanataka kujua juu ya njia yake mpya ya kufundisha. Oh, wamemsikia akitumia vielezi mbeleni lakini si kwa wingi sana hivyo. Kwa hiyo wanauliza: “Kwa nini wewe unasema nao kwa kutumia vielezi?”

Sababu moja ya kufanya hivyo ni kutimiza maneno ya nabii: “Mimi nitafumbua kinywa changu kwa vielezi, nitatangaza mambo yaliyofichwa tangu kuwekwa misingi.” Lakini kuna zaidi ya hilo katika jambo hili. Matumizi yake ya vielezi hutumikia kusudi la kusaidia kufichua mwelekeo wa moyoni wa watu.

Kwa kweli, watu wengi wanapendezwa na Yesu akiwa tu msimuliaji hadithi stadi na mfanya miujiza, si akiwa mmoja anayepasa kutumikiwa akiwa Bwana na kufuatwa bila ubinafsi. Wao hawataki kusumbuliwa katika maoni yao juu ya mambo au njia yao ya maisha. Wao hawataki ujumbe upenye kwa kadiri hiyo.

Kwa hiyo Yesu anasema: “Hii ndiyo sababu mimi nanena nao kwa kutumia vielezi, kwa sababu, kutazama, watazama bure, na kusikia, wasikia bure, wala hawapati maana yayo; na kuwaelekea unabii wa Isaya unapata utimizo, usemao, ‘ . . . Kwa kuwa moyo wa watu hawa umekuwa usioitikia.’”

“Hata hivyo,” Yesu aendelea kusema, “yenye furaha ni macho yenu kwa sababu yanaona, na masikio yenu kwa sababu yanasikia. Kwa kuwa kweli kweli mimi nawaambia nyinyi, Manabii wengi na watu waadilifu walitamani kuona mambo mnayoyaona nyinyi na hawakuyaona, na kusikia mambo mnayoyasikia nyinyi na hawakuyasikia.”

Ndiyo, wale mitume 12 na wale walio pamoja nao wana mioyo yenye kuitikia. Kwa hiyo Yesu anasema: “Kwa nyinyi imejaliwa kufahamu zile siri takatifu za ufalme wa mbingu, lakini kwa watu hao haikujaliwa.” Kwa sababu ya tamaa yao ya kufahamu, Yesu anaandalia wanafunzi wake elezo la kielezi cha mpanzi.

“Ile mbegu ni neno la Mungu,” Yesu asema, na ule udongo ni moyo. Kwa habari ya ile mbegu iliyopandwa juu ya uso mgumu wa kandokando ya barabara, yeye anaeleza: “Yule Ibilisi huja na kunyakua neno kutoka mioyo yao ili kwamba wasiamini na kuokolewa.”

Kwa upande mwingine, mbegu iliyopandwa katika udongo ulio juu ya mwamba inarejezea mioyo ya watu wanaolipokea neno kwa shangwe. Hata hivyo, kwa sababu neno haliwezi kutia mizizi yenye kina katika mioyo kama hiyo, watu hao wanaanguka kando wakati pindi ya kutahiniwa au mnyanyaso ifikapo.

Kwa habari ya mbegu iliyoanguka miongoni mwa miiba, Yesu anaendelea, hiyo inarejezea watu waliolisikia neno. Hata hivyo, hawa, wanachukuliwa na mahangaiko na utajiri na anasa za maisha haya, hivyo wanasongwa kabisa wasilete chochote kwenye ukamilifu.

Mwishowe, kwa habari ya ile mbegu iliyopandwa katika udongo mzuri, Yesu anasema, hao ndio wale ambao, baada ya kulisikia neno kwa moyo mzuri na mwema, wanabaki nalo na kuzaa tunda kwa uvumilivu.

Wanabarikiwa kama nini wanafunzi hao waliomtafuta Yesu wapate elezo la mafundisho yake! Yesu anakusudia kwamba vielezi vyake vifahamiwe ili viwape wengine ukweli. “Taa hailetwi ikawekwe chini ya kikapu cha kupimia au chini ya kitanda, sivyo?” Yeye auliza. Hapana, “inaletwa ikawekwe juu ya kinara cha taa.” Hivyo Yesu anaongeza: “Kwa hiyo, angalieni jinsi nyinyi mnavyosikiliza.”

Wabarikiwa kwa Mafundisho Zaidi

Baada ya kupokea elezo la Yesu juu ya kielezi cha mpanzi, wanafunzi wanataka kujifunza zaidi. “Tueleze,” wanaomba, “kile kielezi cha yale magugu katika shamba.”

Lo! jinsi ulivyo tofauti mwelekeo wa wanafunzi na ule wa umati mwingine kwenye ufuo wa bahari! Watu hao wanakosa tamaa yenye bidii ya kujifunza maana ya vielezi, wakitosheka na muhtasari tu wa mambo yaliyo katika vielezi hivyo. Akitofautisha wasikilizaji hao kwenye ufuo wa bahari na wanafunzi wenye udadisi ambao wamemjia nyumbani, Yesu anasema:

“Kipimo ambacho kwa hicho nyinyi mnapima, nyinyi mtapimiwa kwa hicho, ndiyo, nyinyi mtakuwa na zaidi yakiongezwa kwenu.” Wanafunzi hao wanampimia Yesu upendezo wenye bidii na usikivu, na kwa hiyo wanabarikiwa kwa kupokea mafundisho zaidi. Hivyo, katika kujibu swali la wanafunzi wake, Yesu anaeleza hivi:

“Yule mpanzi wa mbegu nzuri ni Mwana wa binadamu; shamba ni ulimwengu; kwa habari ya ile mbegu nzuri, hao ndio wana wa ufalme; bali magugu ni wana wa yule mwovu, na adui aliyeyapanda ni Ibilisi. Mavuno ni umalizio wa mfumo wa mambo na wavunaji ni malaika.”

Baada ya kutambulisha kila sehemu ya kielezi chake, Yesu anaeleza matokeo. Kwenye umalizio wa mfumo wa mambo, yeye anasema kwamba wavunaji, au malaika, watatenganisha Wakristo wa mwigo walio kama magugu na wale ‘wana wa kweli wa ufalme.’ Ndipo “wana wa yule mwovu” watakapotiwa alama kwa ajili ya uharibifu, lakini wale wana wa Ufalme wa Mungu, “wale waadilifu,” watang’aa kwa uangavu katika ule Ufalme wa Baba yao.

Kisha Yesu anawabariki wanafunzi wake wenye udadisi kwa vielezi vitatu zaidi. Kwanza, yeye asema: “Ufalme wa mbingu ni kama hazina iliyofichwa katika shamba, ambayo mtu mmoja aliipata na kuificha; na kwa ajili ya shangwe aliyo nayo anaenda zake na kuuza vitu alivyo navyo na kununua shamba hilo.”

“Tena,” yeye anaendelea, “ufalme wa mbingu ni kama mfanya biashara mwenye kusafiri atafutaye lulu nzuri. Akiisha kupata lulu moja ya thamani ya juu, alienda zake na mara hiyo akauza vitu vyote alivyokuwa navyo akainunua.”

Yesu mwenyewe ni kama huyo mtu anayegundua hazina iliyofichwa na kama mfanya biashara huyo anayepata lulu ya thamani ya juu. Ilikuwa ni kama aliuza kila kitu, akaacha cheo chenye heshima katika mbingu awe binadamu dhalili. Kisha, akiwa mwanadamu duniani, anapatwa na mashutumu na mnyanyaso wenye chuki, akijithibitisha kuwa anastahiki kuwa Mtawala wa Ufalme wa Mungu.

Mwito wenye ushindani unawekwa mbele ya wafuasi wa Yesu pia wauze kila kitu ili wapate thawabu nzuri ajabu ya kuwa ama mtawala mwenzi wa Kristo au raia wa kidunia wa Ufalme. Je! sisi tutaona kuwa na ushirika katika Ufalme wa Mungu kuwa jambo fulani lenye thamani kubwa zaidi ya kila kitu kinginecho maishani, kuwa kama hazina ya bei kubwa au lulu yenye thamani kubwa?

Mwishowe, Yesu anafananisha “ufalme wa mbingu” na wavu unaokusanya samaki wa kila aina. Wakati samaki wanapotenganishwa, wasiofaa kitu wanatupiliwa mbali lakini wale wazuri wanawekwa. Ndivyo, Yesu asema, itakavyokuwa katika umalizio wa mfumo wa mambo; malaika watatenga waovu kutoka kwa waadilifu, wakiwaweka waovu kwa ajili ya kuangamizwa kabisa.

Yesu mwenyewe anaanza mradi huo wa kuvua samaki, akiwaita wanafunzi wake wa kwanza wawe “wavuvi wa watu.” Chini ya uangalizi wa kimalaika, kazi hiyo ya kuvua inaendelea kupitia karne nyingi. Hatimaye wakati wafika wa kuvuta ule “wavu,” unaofananisha yale matengenezo duniani yanaojidai kuwa ya Kikristo.

Ingawa samaki wasiofaa wanatupwa kwenye uharibifu, kwa shukrani sisi tunaweza kuhesabiwa miongoni mwa wale ‘samaki wazuri’ wanaowekwa. Kwa kuonyesha tamaa yenye bidii kama ile ambayo wanafunzi wa Yesu walionyesha ya kutaka maarifa na uelewevu zaidi, sisi tutabarikiwa si kwa mafundisho zaidi tu bali pia kwa baraka ya Mungu ya uhai wa milele. Mathayo 13:1-52; Marko 4:1-34; Luka 8:4-18; Zaburi 78:2; Isaya 6:9, 10, NW.

▪ Ni wakati gani na mahali gani ambapo Yesu ananena kwa vielezi kwa umati?

▪ Ni vielezi gani vitano ambavyo sasa Yesu anasimulia umati?

▪ Kwa nini Yesu anasema kwamba mbegu ya haradali ndiyo iliyo ndogo zaidi ya zote?

▪ Kwa nini Yesu anasema kwa vielezi?

▪ Wanafunzi wa Yesu wanajionyeshaje wenyewe kuwa tofauti na umati?

▪ Ni elezo gani la kielezi cha mpanzi analoandaa Yesu?

▪ Wanafunzi wanatofautianaje na umati ulio ufuoni?

▪ Ni nani au ni nini kinachowakilishwa na yule mpanzi, lile shamba, ile mbegu nzuri, yule adui, yale mavuno, na wale wavunaji?

▪ Ni vielezi gani vitatu zaidi anavyoandaa Yesu, nasi tunaweza kujifunza nini kutokana navyo?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki