Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gt sura 56
  • Ni Mambo Gani Yanayochafua Mtu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ni Mambo Gani Yanayochafua Mtu?
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Habari Zinazolingana
  • Ni Mambo Gani Yanayochafua Mtu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Ni Nini Hasa Kinachomchafua Mtu?
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Yesu Aponya Siku ya Sabato
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Mafarisayo Wamhoji Mtu Aliyekuwa Kipofu
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
Pata Habari Zaidi
Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
gt sura 56

Sura 56

Ni Mambo Gani Yanayochafua Mtu?

UPINZANI kwa Yesu unakuwa wenye nguvu zaidi. Si kwamba tu wengi wa wanafunzi wake wanaondoka bali Wayahudi katika Yudea wanatafuta kumuua, hata kama vile walivyofanya wakati yeye alipokuwa katika Yerusalemu wakati wa Sikukuu ya Kupitwa ya 31 W.K.

Sasa ni wakati wa Sikukuu ya Kupitwa ya 32 W.K. Inaelekea, kupatana na takwa la Mungu la kuhudhuria, Yesu anakwea kwenda kwenye Sikukuu ya Kupitwa katika Yerusalemu. Hata hivyo, yeye anafanya hivyo kwa tahadhari kwa sababu maisha yake yamo hatarini. Baadaye yeye anarudi Galilaya.

Pengine Yesu yuko Kapernaumu wakati Mafarisayo na waandishi kutoka Yerusalemu wanapomjia. Wao wanatafuta msingi ambao juu yao wanaweza kumshtakia kuvunja sheria ya kidini. “Kwa nini wanafunzi wako wanapita lile pokeo la watu wa nyakati zilizopita?” wao wanauliza. “Kwa kielelezo, wao hawanawi mikono yao wakati wanapokaribia kula mlo.” Hili si jambo fulani linalotakwa na Mungu, hata hivyo Mafarisayo wanalifikiria kuwa kosa zito kutofanya sherehe hii ya kimapokeo, iliyotia ndani kuosha mikono kufika viwiko.

Badala ya kuwajibu kuhusu shtaka lao, Yesu aelekeza kwenye uovu wao na kuvunja kwao kimakusudi sheria ya Mungu. “Kwa nini nyinyi pia mnapita ile amri ya Mungu kwa sababu ya pokeo lenu?” yeye anataka kujua. “Kwa kielelezo, Mungu alisema, ‘Heshimu baba yako na mama yako,’ na, ‘Acha yeye ambaye hutukana kwa maneno ya dharau baba au mama aishie katika kifo.’ Lakini nyinyi husema, ‘Yeyote anayesema kwa baba au mama yake: “Chochote mimi nilicho nacho ambacho kwacho wewe ungepata manufaa kutoka kwangu mimi ni zawadi iliyowekwa wakfu kwa Mungu,” yeye si lazima aheshimu baba yake hata kidogo.’”

Kweli kweli, hao Mafarisayo hufundisha kwamba, mali au kitu chochote ambacho kimewekwa wakfu kuwa zawadi kwa Mungu ni mali ya hekalu, na hakiwezi kutumiwa kwa kusudi jinginelo. Hata hivyo, kwa kweli, ile zawadi iliyowekwa wakfu inabaki na yule mtu ambaye aliiweka wakfu. Katika njia hii, kwa kusema tu kwamba pesa au mali yake ni “korbani”—zawadi iliyowekwa wakfu kwa Mungu au kwa hekalu—mwana anaepa daraka lake la kusaidia wazazi wake waliozeeka, ambao huenda wakawa katika shida kubwa sana.

Akighadhibikia kwa kufaa Mafarisayo kwa kupotosha vibaya Sheria ya Mungu,” Yesu anasema: “Nyinyi mnafanya neno la Mungu kuwa bure kwa sababu ya pokeo lenu. Nyinyi wanafiki, Isaya alitoa unabii kwa kufaa juu yenu nyinyi, wakati yeye alisema, ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao, hata hivyo mioyo yao imeondolewa mbali nami. Ni kwa bure kwamba wao wanaendelea kuniabudu kwa sababu wao hufundisha amri za wanadamu kuwa mafundisho ya kidini.’”

Pengine umati ule ulikuwa umerudi nyuma ili kuruhusu Mafarisayo wamuulize Yesu swali. Sasa, wakati hao Mafarisayo wanapokosa jibu kwa kemeo lenye nguvu la Yesu kuwahusu, yeye anaita umati ukaribie. “Nisikilizeni,” yeye anasema, “na mpate maana. Hakuna kitu kutoka nje ya mtu kinachomwingia chaweza kumchafua; lakini vile vitu ambavyo hutoka nje kutoka ndani ya mtu ndivyo vitu ambavyo huchafua mtu.”

Baadaye, wakati wanapoingia ndani ya nyumba, wanafunzi wake wanauliza: “Je! wewe unajua kwamba wale Mafarisayo walikwazika kwa kusikia yale wewe ulisema?”

“Kila mpando ambao Baba yangu wa kimbingu hakupanda utang’olewa,” Yesu anajibu. “Acheni wao. Wao ni viongozi vipofu. Ikiwa, basi, kipofu amwongoza kipofu, wote wawili wataanguka katika shimo.”

Yesu anaonekana kushangaa wakati, kwa niaba ya wanafunzi, Petro anaomba maelezo ya wazi kuhusu mambo yanayochafua mtu. “Je! nyinyi pia mngali hamna ufahamu?” Yesu anaitikia. “Je! nyinyi hamjui kwamba kila kitu kinachoingia kinywani hupitia ndani ya matumbo nacho hutoka na kuingia katika shimo la takataka? Lakini, vile vitu vinavyotoka katika kinywa hutoka ndani ya moyo, na vitu hivyo ndivyo vinachafua mtu. Kwa kielelezo, ndani ya moyo hutoka mawazo maovu, mauaji ya kukusudia, uzinzi, uasherati, wivi, mashuhuda bandia, makufuru. Haya ndiyo mambo ambayo huchafua mtu; bali kula mlo kwa mikono isiyooshwa hakumchafui mtu.”

Hapa Yesu havunji moyo watu wasiwe na usafi wa kawaida wa kiafya. Yeye hatoi hoja kwamba mtu hahitaji kuosha mikono yake kabla ya kutayarisha chakula au kula mlo. Badala ya hivyo, Yesu analaumu vikali unafiki wa viongozi wa kidini ambao kwa hila hujaribu kuzunguka sheria za uadilifu za Mungu kwa kusisitizia mapokeo yasiyo ya kimaandiko. Ndiyo, vitendo vibaya ndivyo ambavyo huchafua mtu, na Yesu anaonyesha kwamba hivyo huanzia katika moyo wa mtu. Yohana 7:1; Kumbukumbu 16:16; Mathayo 15:1-20; Marko 7:1-23; Kutoka 20:12; 21:17; Isaya 29:13, NW.

▪ Ni upinzani gani ambao sasa Yesu anaelekeana nao?

▪ Mafarisayo wanafanya shtaka gani, lakini kulingana na Yesu, Mafarisayo hao wanavunjaje sheria ya Mungu kwa makusudi?

▪ Yesu anafunua kwamba ni mambo gani ambayo huchafua mtu?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki