Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gt sura 67
  • Washindwa Kumkamata

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Washindwa Kumkamata
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Habari Zinazolingana
  • Wao Washindwa Kumkamata
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • ‘Hakuna Mtu Mwingine Ambaye Amewahi Kuzungumza Hivyo’
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Jifunze Kutoka kwa Nikodemo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2002
  • Amfundisha Nikodemo Usiku
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
Pata Habari Zaidi
Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
gt sura 67

Sura 67

Washindwa Kumkamata

SIKUKUU ya Mahema (Vibanda) inapokuwa ingali ikiendelea, viongozi wa kidini wanapeleka maofisa wa polisi wakamkamate Yesu. Yeye hajaribu kujificha. Badala ya hivyo, Yesu anaendelea kufundisha peupe, akisema: “Mimi naendelea kitambo kidogo pamoja na nyinyi kabla sijaenda kwa yule aliyenituma. Nyinyi mtanitafuta, lakini nyinyi hamtanipata, na niliko mimi nyinyi hamwezi kuja.”

Wayahudi hawaelewi, na kwa hiyo wanauliza miongoni mwao wenyewe: “Ni wapi ambako mwanamume huyu anakusudia kwenda, hivi kwamba sisi hatutampata? Yeye hakusudii kwenda kwa Wayahudi waliotawanyika miongoni mwa Wagiriki na kuwafundisha Wagiriki, sivyo? Usemi huu unamaanisha nini ambao yeye amesema, ‘Nyinyi mtanitafuta, lakini nyinyi hamtanipata, na niliko mimi nyinyi hamwezi kuja’?” Bila shaka, Yesu anaongea juu ya kifo chake kinachokaribia na kufufuliwa kwenye uhai mbinguni, ambako maadui wake hawawezi kumfuata.

Siku ya saba ya sikukuu iliyo ya mwisho inafika. Kila asubuhi ya sikukuu, kuhani fulani amemimina maji, ambayo alitoa katika kidimbwi cha Siloamu, hivi kwamba yatiririka chini ya madhabahu. Inaelekea ni kwa kukumbusha watu juu ya sherehe hiyo ya kila siku, Yesu anapaaza sauti hivi: “Ikiwa mtu yeyote ni mwenye kiu, acheni huyo aje kwangu mimi na kunywa. Yeye ambaye huweka imani katika mimi sawasawa na vile Andiko limesema, ‘Kutoka katika sehemu yake ya ndani kabisa vijito vya maji yenye uhai vitatiririka.’”

Kwa kweli, hapa Yesu anasema juu ya matokeo makubwa wakati ambapo roho takatifu ingemiminwa. Mmimino huu wa roho takatifu unatukia siku ya Pentekoste mwaka unaofuata. Huko, vijito vya maji yenye uhai vyatiririka wakati wale wanafunzi 120 wanapoanza kuwahudumia watu. Lakini mpaka wakati huo, hakuna roho katika maana ya kwamba hakuna wowote wa wanafunzi wa Kristo wamepakwa mafuta kwa roho takatifu na kuitwa kwenye uhai wa kimbingu.

Kwa kuitikia mafundisho ya Yesu, watu fulani wanaanza kusema: “Kwa uhakika huyu ndiye Yule Nabii,” kwa uwazi wakirejeza kwenye yule nabii mkuu zaidi ya Musa aliyeahidiwa kuja. Wengine wanasema: “Huyu ndiye Kristo.” Lakini wengine wanabisha hivi: “Yule Kristo kwa kweli haji kutoka Galilaya, sivyo? Je! Andiko halikusema kwamba Kristo anakuja kutokana na uzao wa Daudi, na kutoka Bethlehemu kijiji ambako Daudi alikuwa?”

Kwa hiyo mgawanyiko unatokea miongoni mwa umati ule. Watu fulani wanataka Yesu akamatwe, lakini hakuna mmoja anayemgusa. Wakati maofisa wa polisi wanaporudi bila Yesu, wakuu wa makuhani na Mafarisayo wanauliza? “Kwa nini nyinyi hamkumleta ndani?”

“Hajanena kamwe mwanamume mwingine kama huyu,” maofisa wanajibu.

Kwa kujawa na hasira, viongozi wa kidini wanaanza sasa kudhihaki, kusingizia, na kutusi. Wao wanacheka kwa dharau hivi: “Nyinyi pia hamkuongozwa vibaya, sivyo? Hata mmoja wa watawala wala wa Mafarisayo hajaweka imani katika yeye, sivyo? Lakini umati huu usiojua Sheria ni watu walaaniwa.”

Hapo, Nikodemo, Farisayo na mtawala wa Wayahudi (yaani, mshiriki wa Sanhedrini), anathubutu kusema ili atetee Yesu. Huenda wewe ukakumbuka kwamba miaka miwili na nusu iliyotangulia, Nikodemo alijia Yesu usiku na akaonyesha imani katika yeye. Sasa Nikodemo anasema: “Sheria yetu haihukumu mtu isipokuwa iwe kwanza imesikia kutoka kwake na kupata kujua analofanya, sivyo?”

Mafarisayo wanakasirika hata zaidi kwamba mmoja wa watu wao wenyewe anamtetea Yesu. “Wewe pia si wa kutoka Galilaya, sivyo?” wanajibu kwa uchungu. “Tafuta uone kwamba hakuna nabii atakayeinuliwa kutoka Galilaya.”

Ingawa Maandiko hayasemi moja kwa moja kwamba nabii angekuja kutoka katika Galilaya, yanaonyesha kwamba yule Kristo atakuja kutoka huko, yakisema kwamba “nuru kubwa” ingeonwa katika jimbo hilo. Na zaidi, Yesu alizaliwa katika Bethlehemu, na yeye alikuwa mzao wa Daudi. Ingawa labda Mafarisayo wana habari za jambo hili, inaelekea wao ndio wenye lawama la kueneza dhana hizo zisizofaa walizo nazo watu juu ya Yesu. Yohana 7:32-52; Isaya 9:1, 2; Mathayo 4:13-17, NW.

▪ Ni jambo gani linalotukia kila asubuhi ya sikukuu, na huenda Yesu akawa anavutaje fikira kwenye jambo hilo?

▪ Kwa nini wale maofisa wanashindwa kukamata Yesu, na viongozi wa kidini wanajibuje?

▪ Nikodemo ni nani, maoni yake ni nini juu ya Yesu, naye anatendwaje na Mafarisayo wenzake?

▪ Kuna uthibitisho gani kwamba yule Kristo angekuja kutoka katika Galilaya?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki