Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w88 4/15 kur. 8-9
  • Wao Washindwa Kumkamata

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wao Washindwa Kumkamata
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Habari Zinazolingana
  • Washindwa Kumkamata
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • ‘Hakuna Mtu Mwingine Ambaye Amewahi Kuzungumza Hivyo’
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Jifunze Kutoka kwa Nikodemo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2002
  • Amfundisha Nikodemo Usiku
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
w88 4/15 kur. 8-9

Maisha na Huduma ya Yesu

Wao Washindwa Kumkamata

SIKUKUU ya Mahema (Vibanda) inapokuwa ingali ikiendelea, viongozi wa kidini wanapeleka maafisa wa polisi wakakamate Yesu. Yeye hajaribu kujificha. Yesu anaendelea kufundisha peupe, akisema: “Mimi naendelea kitambo kidogo pamoja na ninyi kabla sijaenda kwa yule aliyenipeleka mimi. Ninyi mtanitafuta mimi, bali ninyi hamtanipata mimi, na ambako mimi niko ninyi hamwezi kuja.”

Wayahudi hawaelewi, na kwa hiyo wanauliza miongoni mwao wenyewe: “Ni wapi ambako mwanamume huyu anakaza nia kwenda, hivi kwamba sisi hatutampata? Yeye hakazi nia kwenda kwa Wayahudi waliotawanywa miongoni mwa Wagiriki na kuwafundisha Wagiriki, sivyo? Usemi huu unamaanisha nini ambao yeye amesema, ‘Ninyi mtanitafuta mimi, lakini ninyi hamtanipata mimi, na ambako mimi niko ninyi hamwezi kuja’?” Bila shaka, Yesu anaongea juu ya kifo chake kinachokaribia na kufufuliwa kwenda mbinguni, ambako adui zake hawawezi kumfuata.

Siku ya saba iliyo ya mwisho ya sikukuu inafika. Kila asubuhi ya sikukuu, kuhani fulani amemimina maji, ambayo alitoa katika kidimbwi cha Siloamu, hivi kwamba yakatiririka kwenda sehemu ya chini ya madhabahu. Inaelekea ni kwa kukumbusha watu juu ya sherehe hiyo ya kila siku, Yesu anapaaza sauti hivi: “Ikiwa mtu ye yote ni mwenye kiu, acheni huyo aje kwangu mimi na kunywa. Yeye ambaye hutia imani katika mimi, sawa na vile lile Andiko limesema, ‘Kutoka katika sehemu yake ya ndani kabisa vijito vya maji yenye uhai vitatiririka.’”

Kwa kweli, hapa Yesu anasema juu ya matokeo makubwa wakati ambapo roho takatifu ingemiminwa. Mmimino huu wa roho takatifu unatukia siku ya Pentekoste mwaka unaofuata. Huko, vijito vya maji yenye uhai vinatokeza vikitiririka wakati wale wanafunzi 120 wanapoanza kuwahudumia watu. Lakini mpaka wakati huo, hakuna roho katika maana ya kwamba hakuna wo wote wa wanafunzi wa Kristo wanaopakwa mafuta kwa roho takatifu na kuitwa kwenye uhai wa kimbingu.

Kwa kuitikia fundisho la Yesu, watu fulani wanaanza kusema: “Kwa uhakika huyu ndiye Yule Nabii,” kwa uwazi wakirejeza kwenye yule nabii mkubwa kuliko Musa aliyeahidiwa kuja. Wengine wanasema: “Huyu ndiye Kristo.” Lakini wengine wanabisha hivi: “Yule Kristo kwa kweli haji kutoka Galilaya, sivyo? Je! Andiko halijasema kwamba Kristo anakuja kutokana na mzao wa Daudi, na kutoka Bethlehemu kijiji ambako Daudi alikuwa akiwa huko?”

Kwa hiyo mgawanyiko unatokea miongoni mwa kutano lile. Watu fulani wanataka Yesu akamatwe, lakini hakuna mmoja anaweka mkono juu yake. Wakati maafisa wa polisi wanaporudi bila Yesu, wakuu wa makuhani na Mafarisayo wanauliza: “Kwa sababu gani ninyi hamkumleta ndani?”

“Hajanena kamwe mwanamume mwingine kama huyu,” maafisa wanajibu.

Kwa kujawa na kasirani, viongozi wa kidini wanaanza sasa kudhihaki, kusingizia, na kuita majina mabaya. Wao wanacheka kwa madharau: “Ninyi pia hamkuongozwa vibaya, sivyo? Hata mmoja wa watawala wala wa Mafarisayo hajatia imani katika huyo, sivyo? Lakini kutano hili ambalo haliijui Sheria ni watu walaaniwa.”

Hapo, Nikodemo, Farisayo na mtawala wa Wayahudi (yaani, mshiriki wa Sanhedrini), anathubutu kusema ili atetee Yesu. Huenda wewe ukakumbuka kwamba miaka miwili na nusu iliyotangulia, Nikodemo alijia Yesu usiku na akaonyesha imani katika yeye. Sasa Nikodemo anasema: “Sheria yetu haihukumu mtu isipokuwa iwe kwanza imesikia kutoka kwake na kuja kujua analofanya, sivyo?”

Mafarisayo wanapata kasirani hata zaidi kwamba mmoja wa watu wao wenyewe anamkinga Yesu. “Wewe pia si wa kutoka Galilaya, sivyo?” wao wanakejeli. “Tafuta na uone kwamba hakuna nabii atakayepasa kuinuliwa kutoka Galilaya.”

Ingawa Maandiko hayasemi moja kwa moja kwamba nabii angekuja kutoka ndani ya Galilaya, yanaonyesha kuwa yule Kristo atakuja kutoka kwenye mahali hapo, yakisema kwamba “nuru kubwa” ingeonwa katika jimbo hili. Na tofauti na dhana zisizofaa, Yesu alizaliwa katika Bethlehemu, na yeye alikuwa mzao wa Daudi. Ingawa labda Mafarisayo wana habari za jambo hili, inaelekea wao ndio wenye lawama la kueneza dhana hizo zisizofaa ambazo watu wanazo juu ya Yesu. Yohana 7:32-52; Isaya 9:1, 2; Mathayo 4:13-17, NW.

◆ Ni jambo gani linalotukia kila asubuhi ya sikukuu, na ni jinsi gani huenda Yesu akawa anavuta fikira kwenye jambo hili?

◆ Kwa sababu gani wale maafisa wanashindwa kukamata Yesu, na viongozi wa kidini wanajibu jinsi gani?

◆ Nikodemo ni nani, mwelekeo wake ni nini juu ya Yesu, na yeye anatendewa jinsi gani na Mafarisayo wenzake?

◆ Kuna ithibati gani kwamba yule Kristo angekuja kutoka ndani ya Galilaya?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki