Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gt sura 68
  • Fundisho Zaidi Katika Siku ya Saba

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Fundisho Zaidi Katika Siku ya Saba
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Habari Zinazolingana
  • Fundisho Zaidi Siku ya Saba
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Mwana wa Mungu​—“Nuru ya Ulimwengu”
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Majaribio Zaidi ya Kumuua Yesu
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Kuwatayarisha Mitume kwa Ajili ya Kuondoka Kwake
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
Pata Habari Zaidi
Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
gt sura 68

Sura 68

Fundisho Zaidi Katika Siku ya Saba

SIKU ya mwisho ya Sikukuu ya Mahema (Vibanda), ile siku ya saba, ingali inaendelea. Yesu anafundisha katika kisehemu cha hekalu kinachoitwa “chumba cha hazina.” Inaonekana hapa ni katika eneo linaloitwa Ua wa Wanawake ambapo pana masanduku ambamo watu hutumbukiza michango yao.

Kila usiku wa sikukuu, kuna wonyesho wa mmuliko wa pekee katika eneo hili la hekalu. Vinara vikubwa vinne vya taa vimesimamishwa hapa, kila kimoja kikiwa na mabakuli makubwa manne yaliyojazwa mafuta. Nuru inayotoka katika taa hizi, zikichoma mafuta kutoka yale mabakuli 16, ina nguvu za kutosha kumulikia sehemu zinazozunguka, mpaka kufika umbali mrefu wakati wa usiku. Jambo ambalo sasa Yesu anasema huenda likakumbusha wasikilizaji wake juu ya wonyesho huu. “Mimi ndimi nuru ya ulimwengu,” Yesu apiga mbiu. “Yeye ambaye ananifuata mimi hatatembea kwa vyovyote katika giza, bali atakuwa na nuru ya uhai.”

Mafarisayo wanapinga: “Wewe unatoa ushahidi juu yako mwenyewe; ushahidi wako si wa kweli.”

Yesu atoa jibu hivi: “Hata kama mimi natoa ushahidi juu yangu mwenyewe, ushahidi wangu ni wa kweli, kwa sababu mimi najua ambako mimi nilitoka na ambako mimi ninaenda. Lakini nyinyi hamjui ambako mimi nilitoka na ambako mimi ninaenda.” Yeye anaongezea hivi: “Mimi ni mmoja ambaye natoa ushahidi juu yangu mwenyewe, na Baba ambaye alinituma anatoa ushahidi juu yangu.”

“Yuko wapi Baba yako?” Mafarisayo wanataka kujua.

“Nyinyi hamjui wala mimi wala Baba yangu,” Yesu anajibu. “Kama mngalinijua mimi, nyinyi mngalijua Baba yangu pia.” Hata ingawa Mafarisayo bado wanataka Yesu akamatwe, hakuna mmoja ambaye anamgusa.

“Mimi naenda zangu,” Yesu anasema tena. “Mahali ambako mimi ninaenda nyinyi hamwezi kuja.”

Kwa sababu hiyo Wayahudi wanaanza kushangaa wakitaka kujua: “Yeye hatajiua, sivyo? Kwa sababu yeye anasema, ‘Mahali ambako mimi ninaenda nyinyi hamwezi kuja.’”

“Nyinyi ni wa kutoka yale makao ya chini,” Yesu anaeleza. “Mimi ni wa kutoka yale makao yaliyo juu. Nyinyi ni wa kutoka kwenye ulimwengu huu; mimi si wa kutoka kwenye ulimwengu huu.” Ndipo yeye anapoongezea hivi: “Ikiwa nyinyi hamwamini kwamba mimi ndiye, nyinyi mtakufa katika dhambi zenu.”

Bila shaka, Yesu anarejezea kwenye kuwako kwake kabla ya kuwa mwanadamu, na kuwa yeye ndiye Mesiya aliyeahidiwa, au Kristo. Hata hivyo, wao wanauliza hivi, bila shaka kwa dharau kubwa: “Wewe ni nani?”

Akikaidi kumkataa kwao, Yesu anajibu: “Ni kwa nini hata ninasema na nyinyi?” Na bado yeye anaendelea kusema: “Yeye aliyenituma mimi ni wa kweli, na mambo yale yale yenyewe ambayo mimi nilisikia kutoka kwake mimi ninanena katika ulimwengu.” Yesu anaendelea hivi: “Mara nyinyi mkiisha kuwa mmemwinua Mwana wa binadamu, hapo ndipo nyinyi mtajua kwamba mimi ndiye, na kwamba mimi sifanyi jambo kwa kujianzishia mwenyewe; bali sawasawa na vile Baba alivyonifundisha ndivyo mimi ninavyonena mambo haya. Na yeye ambaye alinituma mimi yuko pamoja nami; yeye hakuniacha nibaki peke yangu mwenyewe, kwa sababu sikuzote mimi nafanya mambo yanayomfurahisha.”

Wakati Yesu anaposema mambo haya, wengi wanaweka imani katika yeye. Kwa hao yeye anasema: “Nyinyi mkibaki katika neno langu, nyinyi ni wanafunzi wangu kweli kweli, na nyinyi mtaujua ule ukweli, nao huo ukweli utawaweka nyinyi huru.”

“Sisi ni uzao wa Abrahamu,” wapinzani wake wanafoka, “nasi hatujawa kamwe watumwa kwa mtu yeyote. Wewe unasemaje, ‘Nyinyi mtakuwa huru’?”

Ingawa mara nyingi Wayahudi wamekuwa chini ya utawala wa kigeni, wao hawakiri mwonevu yeyote kuwa bwana-mkubwa. Wao wanakataa kuitwa watumwa. Lakini Yesu anaonyesha wazi kwamba wao ni watumwa kweli kweli. Kwa njia gani? “Kweli kweli kabisa mimi nawaambia nyinyi,” Yesu anasema, “kila mtenda dhambi ni mtumwa wa dhambi.”

Kukataa kukubali utumwa wao kwa dhambi kunatia Wayahudi katika msimamo hatari. “Mtumwa habaki kati ya watu wa nyumbani milele,” Yesu anaeleza. “Mwana anabaki milele.” Kwa kuwa mtumwa hana haki za urithi, huenda akawa katika hatari ya kuondolewa kazini wakati wowote. Mwana ambaye kwa kweli alizaliwa au alichukuliwa alelewe kati ya watu wa nyumba ile ndiye peke yake anayebaki “milele,” yaani, maadamu yeye yuko hai.

“Basi ikiwa yule Mwana anawaweka nyinyi huru,” Yesu anaendelea, “nyinyi kwa kweli mtakuwa huru.” Hivyo, ukweli ambao unaweka watu huru ni ule ukweli kuhusu yule Mwana, Yesu Kristo. Ni kwa njia ya dhabihu tu ya uhai wake mkamilifu wa kibinadamu kwamba mtu yeyote anaweza kuwekwa huru kutoka kwenye dhambi inayoleta kifo. Yohana 8:12-36, NW.

▪ Yesu anafundisha wapi siku ya saba? Ni jambo gani linalotukia huko wakati wa usiku, nalo linahusianaje na fundisho la Yesu?

▪ Yesu anasema nini juu ya asili yake, na hilo linapasa kufunua nini juu ya utambulishi wake?

▪ Ni kwa njia gani Wayahudi ni watumwa, lakini ni ukweli gani utakaowaweka huru?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki