Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gt sura 77
  • Suala la Urithi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Suala la Urithi
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Habari Zinazolingana
  • Suala la Urithi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Yesu Atoa Ushauri Kuhusu Utajiri
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Hazina Yako Iko Wapi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • “Mjifunze Kutoka Kwangu”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
Pata Habari Zaidi
Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
gt sura 77

Sura 77

Suala la Urithi

INAONEKANA wazi kwamba watu wanajua Yesu amekuwa akila mlo mkuu kwenye nyumba ya yule Farisayo. Kwa hiyo wanakusanyika nje kwa maelfu na wanakuwa wakingoja wakati Yesu anapotoka ndani. Tofauti na Mafarisayo ambao wanapinga Yesu na kujaribu kumshika katika kusema jambo lisilofaa, watu hao wanamsikiliza kwa hamu nyingi wakiwa na uthamini.

Akigeukia wanafunzi wake kwanza, Yesu anasema: “Mwe macho kuona chachu ya Mafarisayo, ambayo ni unafiki.” Kama ilivyoonyeshwa wakati wa ule mlo, mfumo mzima wa kidini wa Mafarisayo umejawa na unafiki. Lakini hata ingawa uovu wa Mafarisayo huenda ukafichwa kwa kujionyesha kuwa wenye utawa, mwishowe utafichuliwa. “Hakuna kitu ambacho kimefichwa kwa uangalifu,” Yesu anasema, “ambacho hakitafunuliwa, na siri ambayo haitakuja kujulikana.”

Yesu anaendelea kurudia kile kitia-moyo alichokuwa amewapa wale 12 wakati alipowatuma waende katika ziara ya kuhubiri ya Galilaya. Yeye anasema: “Msihofu wale ambao wanaua mwili na baada ya hilo hawawezi kufanya jambo lolote zaidi.” Kwa kuwa Mungu hasahau hata shomoro mmoja, Yesu anahakikishia wafuasi wake kwamba Mungu hatawasahau wao. Yeye anataarifu hivi: “Wakati wao wanapoleta nyinyi ndani mbele ya makusanyiko ya umma na maofisa wa serikali na wenye mamlaka, . . . roho takatifu itafundisha nyinyi katika saa hiyo hiyo yenyewe mambo ambayo nyinyi mnapaswa kusema.”

Mwanamume mmoja katika umati huo anajitokeza kunena. “Mwalimu,” yeye anafanya ombi rasmi, “ambia ndugu yangu agawanye urithi pamoja nami.” Sheria ya Musa inaweka sharti kwamba mwana mzaliwa wa kwanza apaswa kupokea sehemu mbili za urithi kwa hiyo hakuna sababu ya kuwa na ubishi. Lakini inaonekana mwanamume yule anataka zaidi ya fungu lake halali la urithi huo.

Kwa kufaa Yesu anakataa kujihusisha ndani. “Mwanamume, nani aliyeniweka rasmi niwe hakimu au mgawaji wa mafungu juu yenu watu?” yeye auliza. Ndipo yeye anatolea umati huo onyo hili la upole lililo muhimu: “Wekeni macho yenu yakiwa yamefunguka na mlinde dhidi ya kila namna ya uchoyo kwa sababu hata wakati ambao mtu ana utele uhai wake hautokani na vitu ambavyo yeye anamiliki.” Ndiyo, hata mtu aje kuwa na kiasi gani, kwa kawaida yeye atakufa na kuacha vyote nyuma. Kukazia uhakika huo, na pia kuonyesha upumbavu wa kushindwa kujenga sifa njema pamoja na Mungu, Yesu anatumia kielezi. Yeye anaeleza hivi:

“Shamba la mwanamume mmoja tajiri lilizaa vizuri. Basi yeye akaanza kusababu-sababu ndani yake mwenyewe, akisema, ‘Mimi nitafanya nini, kwa kuwa sasa sina mahali popote pa kukusanya mazao yangu?’ Kwa hiyo yeye akasema, ‘Mimi nitafanya hivi: Nitabomoa nyumba zangu za kuwekea akiba na kujenga kubwa zaidi, na humo mimi nitakusanya nafaka yangu yote na vitu vyangu vyote vilivyo vizuri; nami nitaiambia nafsi yangu: “Nafsi, wewe una vitu vingi vizuri ambavyo vimewekwa kwa ajili ya miaka mingi; starehe, ule, unywe, ujifurahishe mwenyewe.”’ Lakini Mungu akasema kwake, ‘Mmoja usiyesababu vizuri, usiku huu wao wanadai nafsi yako kutoka kwako wewe. Ni nani, basi, atakuwa na vitu vile ambavyo wewe umejirundikia akibani?’”

Katika kumalizia, Yesu anaonelea hivi: “Ndivyo inavyokuwa kwa mtu ambaye anaweka rundo kwa ajili yake mwenyewe lakini si tajiri kuelekea Mungu.” Ingawa huenda ikawa wanafunzi hawatiwi mtegoni na upumbavu wa kurundika utajiri, kwa sababu ya mahangaiko ya maisha ya kila siku wao wangeweza kwa urahisi kuvutwa fikira zitoke kwenye utumishi wa nafsi yote kwa Yehova. Kwa hiyo Yesu anatumia pindi hiyo kurudia yale mashauri mema aliyokuwa ametoa karibu mwaka mmoja na nusu mapema katika yale Mahubiri ya Mlimani. Akigeukia wanafunzi wake, yeye anasema:

“Kwa sababu hii mimi nasema kwenu nyinyi, Acheni kabisa kuwa wenye wasiwasi juu ya nafsi zenu kwa habari ya kile ambacho nyinyi mtakula au juu ya miili yenu kwa habari ya kile ambacho nyinyi mtavaa. . . . Angalieni vizuri kwamba kunguru hawapandi mbegu wala hawavuni, nao hawana ghala wala nyumba za kuwekea akiba, na bado Mungu analisha wao. . . . Angalieni vizuri jinsi maua-lili yanavyokua; hayo hayajitaabishi wala hayafumi; lakini mimi naambia nyinyi, Wala hata Solomoni katika utukufu wake wote hakuvikwa vizuri kama moja la haya. . . .

“Kwa hiyo acheni kabisa kutafuta kile ambacho nyinyi huenda mkala na kile ambacho nyinyi huenda mkanywa, na acheni kabisa kuwa katika engoengo la wasiwasi; kwa maana hivi vyote ndivyo vitu ambavyo mataifa ya ulimwengu yanafuatia kwa hamu nyingi, lakini Baba yenu anajua nyinyi mnahitaji vitu hivi. Hata hivyo, tafuteni ufalme wake kwa kuendelea, na vitu hivi vitaongezwa kwenu nyinyi.”

Maneno ya Yesu yanafaa kufikiriwa kwa umakini hasa nyakati za ugumu wa kiuchumi. Kwa hakika, mtu ambaye anakuwa mwenye wasiwasi wa kupita kiasi juu ya mahitaji ya vitu vya kimwili na kuanza kulegea katika mifuatio ya kiroho anaonyesha ukosefu wa imani katika uwezo wa Mungu wa kuandalia watumishi Wake. Luka 12:1-31; Kumbukumbu 21:17, NW.

▪ Labda ni kwa nini mwanamume yule anauliza juu ya urithi, naye Yesu anatoa onyo gani la upole?

▪ Yesu atumia kielezi gani, na maana yacho ni nini?

▪ Yesu arudia shauri gani, na kwa nini linafaa?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki