Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • rq somo la 12 kur. 24-25
  • Kustahi Uhai na Damu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kustahi Uhai na Damu
  • Mungu Anataka Tufanye Nini?
  • Habari Zinazolingana
  • Heshimu Zawadi ya Uhai
    Biblia Inatufundisha Nini?
  • Maoni ya Mungu Kuhusu Uhai
    Biblia Inafundisha Nini Hasa?
  • Heshima ya Kimungu kwa Uhai na Damu
    Kweli Iongozayo Kwenye Uzima wa Milele
  • Kuokoa Uhai kwa Damu—Jinsi Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
Pata Habari Zaidi
Mungu Anataka Tufanye Nini?
rq somo la 12 kur. 24-25

Somo la 12

Kustahi Uhai na Damu

Tuoneje uhai? (1) utoaji-mimba? (1)

Wakristo huonyeshaje kwamba wanajali usalama? (2)

Je, ni kosa kuwaua wanyama? (3)

Ni nini baadhi ya mazoea ambayo hayaonyeshi staha kwa uhai? (4)

Sheria ya Mungu ni nini juu ya damu? (5)

Je, hiyo yatia ndani utiaji-damu mishipani? (6)

1. Yehova ndiye Chanzo cha uhai. Vitu vyote vyenye uhai vilipata uhai wao kutoka kwa Mungu. (Zaburi 36:9) Uhai ni mtakatifu kwa Mungu. Hata uhai wa mtoto asiyezaliwa bado aliye ndani ya mama yake ni wenye thamani kwa Yehova. Kuua kimakusudi kitoto hicho kinachokua ni kosa machoni pa Mungu.—Kutoka 21:22, 23; Zaburi 127:3.

2. Wakristo wa kweli wanajali usalama. Wao huhakikisha kwamba magari yao na nyumba zao ni zenye usalama. (Kumbukumbu la Torati 22:8) Watumishi wa Mungu hawahatarishi uhai wao ovyoovyo ili tu kuona raha au msisimuko. Kwa hiyo hawashiriki katika michezo yenye jeuri ambayo huumiza watu wengine kimakusudi. Wao huepuka vitumbuizo vinavyochochea ujeuri.—Zaburi 11:5; Yohana 13:35.

3. Uhai wa wanyama pia ni mtakatifu kwa Muumba. Mkristo ana ruhusa ya kuwaua wanyama ili kujiandalia chakula na mavazi au kujilinda dhidi ya ugonjwa na hatari. (Mwanzo 3:21; 9:3; Kutoka 21:28) Lakini ni kosa kuwatenda wanyama vibaya au kuwaua kwa sababu ya mchezo au kuona raha tu.—Mithali 12:10.

4. Kuvuta sigareti, kutafuna miraa, na kutumia dawa za kulevya ili kuona raha hakuwafai Wakristo. Mazoea haya ni mabaya kwa sababu (1) yanatufanya watumwa wayo, (2) yanadhuru miili yetu, na (3) hayo ni machafu. (Warumi 6:19; 12:1; 2 Wakorintho 7:1) Inaweza kuwa vigumu sana kuacha tabia hizi. Lakini ni lazima tufanye hivyo ili kumpendeza Yehova.

5. Damu pia ni takatifu machoni pa Mungu. Mungu husema kwamba nafsi, au uhai, imo katika damu. Kwa hiyo ni kosa kula damu. Ni kosa pia kula nyama ya mnyama ambaye hakuondolewa damu ifaavyo. Ikiwa mnyama amenyongwa au amekufa katika mtego, hapasi kuliwa. Ikiwa amechomwa mkuki au kupigwa risasi, ni lazima aondolewe damu upesi ikiwa ataliwa.—Mwanzo 9:3, 4; Mambo ya Walawi 17:13, 14; Matendo 15:28, 29.

6. Je, ni kosa kukubali utiaji-damu mishipani? Kumbuka, Yehova hutaka tujiepushe na damu. Hiyo yamaanisha kwamba ni lazima tusiingize miilini mwetu kwa njia yoyote ile, damu ya watu wengine au hata damu yetu wenyewe ambayo imewekwa akiba. (Matendo 21:25) Kwa hiyo Wakristo wa kweli hawatakubali utiaji-damu mishipani. Wao watakubali aina nyinginezo za utibabu, kama vile utiaji-mishipani wa vitu visivyofanyizwa kwa damu. Wao wanataka kuishi, lakini hawatajaribu kuokoa uhai wao kwa kuvunja sheria za Mungu.—Mathayo 16:25.

[Picha katika ukurasa wa 25]

Ili kumpendeza Mungu, ni lazima tuepuke utiaji-damu mishipani, tabia chafu, na kuhatarisha uhai ovyoovyo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki