Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gf somo la 8 uku. 14
  • Adui za Mungu Ni Nani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Adui za Mungu Ni Nani?
  • Wewe Unaweza Kuwa Rafiki ya Mungu!
  • Habari Zinazolingana
  • Uwe Macho​—Shetani Anataka Kukumeza!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
  • Mjue Adui Yako
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2018
  • Shetani
    Amkeni!—2013
  • Ibilisi Ni Nani?
    Mungu Anataka Tufanye Nini?
Pata Habari Zaidi
Wewe Unaweza Kuwa Rafiki ya Mungu!
gf somo la 8 uku. 14

SOMO LA 8

Adui za Mungu Ni Nani?

Adui mkuu wa Mungu ni Shetani Ibilisi. Yeye ni kiumbe cha roho aliyemwasi Yehova. Shetani anaendelea kupigana na Mungu naye huwasababishia wanadamu matatizo makubwa. Shetani ni mwovu. Yeye ni mwongo na mwuaji.—Yohana 8:44.

Viumbe wengine wa roho waliungana na Shetani katika uasi wake dhidi ya Mungu. Biblia huwaita viumbe hao roho waovu. Kama Shetani, roho waovu ni adui za wanadamu. Wanapenda kuwaumiza watu. (Mathayo 9:32, 33; 12:22) Yehova atamharibu Shetani na roho wake waovu milele. Wana wakati mfupi tu unaobaki wa kuwasababishia wanadamu matatizo.—Ufunuo 12:12.

Ukitaka kuwa rafiki ya Mungu, lazima usifanye mambo ambayo Shetani anataka ufanye. Shetani na roho waovu humchukia Yehova. Wao ni adui za Mungu, nao wanataka kukufanya uwe adui ya Mungu. Ni lazima uchague yule unayetaka kumpendeza—Shetani au Yehova. Ukiwa unataka uhai udumuo milele, lazima uchague kufanya mapenzi ya Mungu. Shetani ana mbinu na njia nyingi za kudanganya watu. Yeye anawadanganya watu wengi.—Ufunuo 12:9.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki