Israeli Na Mataifa Yaliyolizunguka
YEHOVA alimwambia Abrahamu: ‘Nenda kutoka Uru wa Wakaldayo mpaka katika nchi ambayo nitakuonyesha.’ Nchi hiyo ilikuwa inakaliwa na kuzungukwa na mataifa mengine.—Mwa 12:1-3; 15:17-21.
Watu wa Mungu walipokuwa wakitoka Misri, walijua kwamba huenda wangekabili upinzani kutoka kwa maadui kama vile “wadhalimu wa Moabu.” (Kut 15:14, 15) Waamaleki, Wamoabu, Waamoni, na Waamori waliishi katika maeneo ambayo Waisraeli wangepitia walipokuwa wakielekea Nchi ya Ahadi. (Hes 21:11-13; Kum 2:17-33; 23:3, 4) Nao Waisraeli wangekabiliana na mataifa mengine maadui yaliyoishi katika nchi ambayo Mungu alikuwa amewaahidi.
Mungu aliwaambia Waisraeli ‘waondolee mbali mataifa saba yenye hesabu kubwa ya watu’—Wahiti, Wagirgashi, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi—ambao walipaswa kuangamizwa. Watu hao walikuwa na mazoea yaliyopotoka kidini na kiadili. Baadhi ya miungu waliyoabudu ilitia ndani Baali (aliyewakilishwa na nguzo za mawe zilizokuwa na umbo la uume), Moleki (ambaye watoto walitolewa dhabihu kwake), na Ashtorethi (Astarte), mungu wa kike wa nguvu za uzazi.—Kum 7:1-4; 12:31; Kut 23:23; Law 18:21-25; 20:2-5; Amu 2:11-14; Zb 106:37, 38.
Wakati mwingine eneo lote ambalo Mungu angewapa Waisraeli, kuanzia kaskazini ya Sidoni hadi “bonde la mto la Misri,” liliitwa “Kanaani.” (Hes 13:2, 21; 34:2-12; Mwa 10:19) Nyakati nyingine Biblia hutaja majina ya mataifa mbalimbali, majiji yenye kujitawala, au watu walioishi katika eneo hilo. Baadhi ya mataifa hayo yalikuwa na maeneo hususa. Kwa mfano, Wafilisti waliishi pwani, nao Wayebusi waliishi kwenye milima iliyokuwa karibu na Yerusalemu. (Hes 13:29; Yos 13:3) Baada ya muda, mataifa mbalimbali yalihamia maeneo mengine.—Mwa 34:1, 2; 49:30; Yos 1:4; 11:3; Amu 1:16, 23-26.
Waisraeli walipokuwa wakitoka Misri, yaelekea kabila la Waamori ndilo lililokuwa lenye nguvu zaidi.a (Kum 1:19-21; Yos 24:15) Waamori walikuwa wameteka nchi ya Moabu kuanzia kusini hadi kwenye bonde la mto la Arnoni, ingawa eneo lililokuwa ng’ambo ya Mto Yordani kuanzia Yeriko bado liliitwa “nchi tambarare za jangwa la Moabu.” Wafalme Waamori walitawala pia Bashani na Gileadi.—Hes 21:21-23, 33-35; 22:1; 33:46-51.
Ingawa Waisraeli walikuwa wakisaidiwa na Mungu, hawakufutilia mbali mataifa yote yaliyokuwa yamehukumiwa kuangamizwa ambayo baada ya muda yalikuja kuwa mtego kwa Israeli. (Hes 33:55; Yos 23:13; Amu 2:3; 3:5, 6; 2Fa 21:11) Naam, Waisraeli walinaswa licha ya onyo hili: “Usiifuate miungu mingine, miungu yoyote ya vikundi vya watu wanaowazunguka pande zote.”—Kum 6:14; 13:7.
[Maelezo ya Chini]
a Jina “Waamori” sawa na jina “Wakanaani” linaweza kurejelea watu wa eneo fulani kwa ujumla au kurejelea kabila fulani hususa.—Mwa 15:16; 48:22.
[Ramani katika ukurasa wa 11]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Mataifa Ambayo Yangeondolewa Kutoka Nchi Ya Ahadi
UFILISTI (D8)
C8 Ashkeloni
C9 Gaza
D8 Ashdodi
D8 Gathi
D9 Gerari
KANAANI (D8)
B10 WAAMALEKI
C12 Hasar-adari (Adari?)
C12 Kadeshi (Kadesh-barnea)
D8 Lakishi
D9 Beer-sheba
D10 WAAMORI
D11 NEGEBU
E4 Dori
E5 Megido
E5 Taanaki
E6 Afeki
E6 WAHIVI
E7 WAYEBUSI
E8 Beth-shemeshi
E8 Hebroni (Kiriath-arba)
E9 WAHITI
E9 Debiri
E10 Aradi (Mkanaani)
E10 WAKENI
E11 Akrabimu
F4 WAGIRGASHI
F6 Shekemu
F7 WAPERIZI
F7 Gilgali
F7 Yeriko
F8 Yerusalemu
G2 WAHIVI
G2 Dani (Laishi)
G3 Hasori
FOINIKE (D8)
E2 Tiro
F1 Sidoni
EDOMU
F11 SEIRI
G11 Bosra
WAAMORI (SIHONI) (G8)
G6 GILEADI
G7 Shitimu
G7 Heshboni
G9 Aroeri
SIRIA (H1)
G1 Baal-gadi
G2 WAHIVI
I1 Damasko
MOABU (H10)
WAAMORI (OGU)
G6 GILEADI
H3 BASHANI
H4 Ashtarothi
H4 Edrei
AMONI (I7)
H7 Raba
[Jangwa]
h12 JANGWA LA UARABUNI
[Milima]
E4 Ml. Karmeli
E11 Ml. Hori
G1 Ml. Hermoni
G8 Ml. Nebo
[Bahari]
C6 Bahari ya Mediterania (Bahari Kuu)
F9 Bahari ya Chumvi
G4 Bahari ya Galilaya
[Mito na kijito]
B11 B.M. la Misri
F6 Mto Yordani
G6 B.M. la Yaboki
G9 B.M. la Arnoni
G11 B.M. la Zeredi
[Picha katika ukurasa wa 10]
Kulia: Mfalme Ogu wa Amori alitawala Bashani, eneo lililokuwa mashuhuri kwa ufugaji wa mafahali na kondoo
Chini: Moabu, nyika ya Yuda ikiwa ng’ambo ya Bahari ya Chumvi
[Picha katika ukurasa wa 11]
Yehova aliwaagiza Waisraeli wayaondoe mataifa yaliyokuwa yakiabudu miungu ya uwongo, kama vile Baali, Moleki, na Ashtorethi, mungu wa kike wa nguvu za uzazi (ona picha)