‘Yehova Alipowasimamisha Waamuzi’
UNAWEZA kuona kwa urahisi Mlima Tabori (F4) kwenye ramani, uko kusini-magharibi ya Bahari ya Galilaya, katika Bonde la Yezreeli. Ebu wazia wanajeshi 10,000 wakiwa wamekusanyika juu ya mlima huo. Yehova alitumia Mwamuzi Baraka na nabii Debora ili kuwachochea Waisraeli waungane dhidi ya Mfalme Yabini wa Kanaani, aliyekuwa amewakandamiza kwa muda wa miaka 20. Chini ya Sisera, mkuu wa jeshi, magari ya vita 900 ya Yabini yenye miundu mikali ya chuma yalitoka Haroshethi hadi kwenye mto mkavu wa Kishoni, kati ya Megido na Mlima Tabori.
Mwamuzi Baraka aliwaongoza Waisraeli hadi kwenye bonde ili kupigana na majeshi ya Sisera. Yehova aliwapa ushindi kwa kutuma mafuriko ya ghafula yaliyofanya magari ya vita ya Sisera yakwame matopeni, jambo lililowaogopesha Wakanaani. (Amu 4:1–5:31) Huo ulikuwa mojawapo wa ushindi ambao Mungu aliwapa Waisraeli katika kipindi cha Waamuzi.
Nchi ya Kanaani ilipotekwa, iligawanywa kwa makabila ya Israeli. Ona mahali yalipoishi makabila ambayo hayakuwa ya Lawi. Kabila dogo la Simeoni lilipewa majiji yaliyokuwa katika eneo la Yuda. Baada ya kifo cha Yoshua, hali ya kiroho na ya kiadili ya taifa hilo ilizorota. Waisraeli “wakawa katika dhiki kali sana,” kwa sababu ya kukandamizwa na maadui. Kwa huruma zake, ‘Yehova alisimamisha waamuzi’—watu 12 wenye imani na ujasiri—waliowakomboa Waisraeli kwa muda wa karne tatu.—Amu 2:15, 16, 19.
Mwamuzi Gideoni alitumia wanajeshi 300 tu ambao hawakuwa na silaha za kutosha, lakini walikuwa wepesi na wenye nguvu na hivyo akawashinda askari wa Midiani 135,000. Uwanja wa mapigano ulikuwa katikati ya Mlima Gilboa na More. Baada ya kupata ushindi wa kwanza, Gideoni aliwafukuza adui hadi upande wa mashariki kwenye jangwa.—Amu 6:1–8:32.
Yeftha, Mgileadi wa kabila la Manase alikomboa miji ya Israeli iliyokuwa mashariki ya Yordani kutoka kwa wakandamizaji Waamoni. Ili kupata ushindi, yaelekea Yeftha alitumia Barabara ya Mfalme iliyounganisha Ramoth-gileadi na eneo la Aroeri.—Amu 11:1–12:7.
Samsoni alipigana na Wafilisti hasa kwenye eneo la pwani karibu na Gaza na Ashkeloni. Eneo la Gaza liko katika sehemu yenye maji mengi ambayo ni mashuhuri kwa ukulima. Samsoni alitumia mbweha 300 kuteketeza mashamba ya Wafilisti ya nafaka, mizabibu, na mizeituni.—Amu 15:4, 5.
Kama inavyoonyeshwa na simulizi hilo la Biblia au inavyodokezwa na makabila yao, waamuzi walikuwa viongozi katika sehemu zote za Nchi ya Ahadi. Iwe walipigana wapi, Yehova aliwasaidia watu wake wakati wa taabu walipotubu.
[Ramani katika ukurasa wa 15]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Makabila na Waamuzi
Waamuzi
1. Othnieli Makabila ya Manase
2. Ehudi Makabila ya Yuda
3. Shamgari Makabila ya Yuda
4. Baraka Makabila ya Naftali
5. Gideoni Makabila ya Isakari
6. Tola Makabila ya Manase
7. Yairi Makabila ya Manase
8. Yeftha Makabila ya Gadi
9. Ibzani Makabila ya Asheri
10. Eloni Makabila ya Zabuloni
11. Abdoni Makabila ya Efraimu
12. Samsoni Makabila ya Yuda
Mafungu ya Makabila (Ona kichapo)
Majiji Mengine ya Manase
E4 Dori
E5 Megido
E5 Taanaki
F4 En-dori
F5 Beth-sheani (Beth-shani)
F5 Ibleamu (Gath-rimoni)
Majiji Mengine ya Simeoni
C9 Sharuheni (Shaaraimu) (Shilhimu)
C10 Beth-lebaothi (Beth-biri)
D8 Etheri (Tokeni)
D9 Siklagi
D9 Aini
D9 Hasar-susa?
D9 Ashani
D9 Beer-sheba
D10 Hasar-shuali
E9 Etamu
E9 Beth-markabothi
E9 Bethueli? (Kesili?)
E9 Sheba? (Yeshua)
E10 Baalath-beeri (Baali)
E10 Esemu
Majiji ya Makimbilio ya Walawi
E8 Hebroni
F3 Kedeshi
F6 Shekemu
H4 Golani
H5 Ramoth-gileadi
H8 Beseri
Barabara Kuu
B10 Via Maris
G10 Barabara ya Mfalme
Makabila Ya Israeli
DANI (D7)
D7 Yopa
E8 Sora
YUDA (D9)
C8 Ashkeloni
C9 Gaza
C9 Sharuheni (Shaaraimu) (Shilhimu)
C10 Beth-lebaothi (Beth-biri)
C12 Asimoni
C12 Kadeshi
D7 Yabneeli
D8 Etheri (Tokeni)
D9 Siklagi
D9 Aini
D9 Hasar-shuali
D9 Ashani
D9 Beer-sheba
D10 Hasar-shuali
E8 Lehi
E8 Bethlehemu
E8 Hebroni
E9 Etamu
E9 Beth-markabothi
E9 Bethueli? (Kesili?)
E9 Sheba? (Yeshua)
E10 Baalath-beeri (Baali)
E10 Esemu
ASHERI (E3)
E2 Tiro
E4 Haroshethi
E4 Dori
F1 Sidoni
MANASE (E5)
E6 Shamiri (Samaria)
E6 Pirathoni
F6 Shekemu
G5 Abel-mehola
EFRAIMU (E7)
E7 Timnath-sera
F6 Tapua
F6 Shilo
F7 Betheli (Luzi)
NAFTALI (F3)
F2 Beth-anathi
F3 Kedeshi
G3 Hasori
ZABULONI (F4)
E4 Bethlehemu
ISAKARI (F5)
E5 Megido
E5 Kedeshi (Kishioni)
E5 Taanaki
F4 En-dori
F5 Beth-shita
F5 Beth-sheani (Beth-shani)
F5 Ibleamu (Gath-rimoni)
BENYAMINI (F7)
F7 Gilgali
F8 Yerusalemu
DANI (G2)
G2 Dani (Laishi)
MANASE (H3)
H4 Golani
GADI (H6)
G6 Sukothi
G6 Penueli
G6 Mispa (Mispe)
G7 Yogbeha
H5 Ramoth-gileadi
H7 Raba
H7 Abel-keramimu
RUBENI (H8)
G7 Heshboni
G9 Aroeri
H7 Minithi
H8 Beseri
[Mahali Pengine]
I1 Damasko
[Milima]
F4 Ml. Tabori
F4 More
F6 Ml. Ebali
F5 Ml. Gilboa
F6 Ml. Gerizimu
[Bahari]
C5 Bahari ya Mediterania (Bahari Kuu)
F9 Bahari ya Chumvi
G4 Bahari ya Galilaya
[Mito na Vijito]
B11 B.M. la Misri
F6 Mto Yordani
G6 B.M. la Yaboki
G9 B.M. la Arnoni
G11 B.M. la Zeredi
[Picha katika ukurasa wa 14]
Mlima Tabori, katika eneo la Isakari, juu ya Bonde la Yezreeli
[Picha katika ukurasa wa 14]
Mto Kishoni uliofurika ulifanya magari ya vita ya Sisera yakwame matopeni