Yesu “Katika Nchi Ya Wayahudi”
ALIPOKUWA akimhubiria Kornelio, mtume Petro alitaja mambo ambayo Yesu alifanya “katika nchi ya Wayahudi na pia katika Yerusalemu.” (Mdo 10:39) Unafikiri Yesu alitembelea maeneo gani wakati wa huduma yake iliyoathiri historia ya ulimwengu?
“Nchi ya Wayahudi” ilitia ndani Yudea, ambapo Yesu alifanya kazi ya Mungu. (Lu 4:44) Baada ya kubatizwa, Yesu alikaa siku 40 katika nyika ya Yuda (au Yudea), eneo kame na lenye ukiwa ambalo mara kwa mara lilikuwa na waasi na majambazi. (Lu 10:30) Baadaye, Yesu alipokuwa akielekea kaskazini kutoka Yudea alimhubiria mwanamke Msamaria karibu na Sikari.—Yoh 4:3-7.
Vitabu vya Injili vinaonyesha kwamba Yesu alihubiri hasa katika eneo la Galilaya. Ingawa alisafiri kuelekea kusini hadi Yerusalemu ili kuhudhuria sherehe za kila mwaka, alitumia sehemu kubwa ya ile miaka miwili ya kwanza ya huduma yake katika eneo lililo kaskazini mwa Nchi ya Ahadi. (Yoh 7:2-10; 10:22, 23) Kwa mfano, alifunza mambo mengi muhimu na kufanya miujiza yenye kuvutia alipokuwa kwenye Bahari ya Galilaya au karibu na eneo hilo. Kumbuka kwamba alituliza bahari hiyo ilipochafuka na hata akatembea juu yake. Akiwa kwenye mashua, alihubiria umati uliokuwa kwenye fuo zenye changarawe za bahari hiyo. Wafuasi wake wa mapema ambao walikuwa na uhusiano wa karibu naye walitoka katika jamii za wakulima na wavuvi zilizoishi karibu na bahari hiyo.—Mk 3:7-12; 4:35-41; Lu 5:1-11; Yoh 6:16-21; 21:1-19.
Yesu alipokuwa akihubiri huko Galilaya, alifanya Kapernaumu, “jiji lake,” lililokuwa ufuoni kuwa kituo cha huduma yake. (Mt 9:1) Alikuwa kando ya kilima kilichokuwa karibu na mahali hapo wakati wa yale Mahubiri yake maarufu ya Mlimani. Nyakati nyingine, alisafiri kwa mashua kutoka Kapernaumu hadi Magadani, Bethsaida, au maeneo yaliyokuwa karibu.
Ona kwamba ‘jiji la Yesu’ halikuwa mbali na majiji yafuatayo: Nazareti, ambapo alikulia; Kana, ambapo aligeuza maji yakawa divai; Naini, ambapo alimfufua yule mwana wa mjane; na Bethsaida, ambapo alilisha kimuujiza wanaume 5,000 na kumponya kipofu.
Baada ya Pasaka ya mwaka wa 32 W.K., Yesu alielekea kaskazini hadi Tiro na Sidoni, majiji yenye bandari ya Foinike. Kisha akapanua huduma yake hadi kwenye baadhi ya yale majiji kumi ya Kigiriki yaliyoitwa Dekapoli. Yesu alikuwa karibu na Kaisaria Filipi (F2) Petro alipokiri kwamba yeye ndiye Mesiya, na muda mfupi baada ya hapo Yesu aligeuka sura labda akiwa kwenye Mlima Hermoni. Baadaye, Yesu alihubiri katika eneo la Perea lililokuwa ng’ambo ya Yordani.—Mk 7:24-37; 8:27–9:2; 10:1; Lu 13:22, 33.
Yesu alitumia juma lake la mwisho duniani akiwa pamoja na wanafunzi wake huko Yerusalemu, “jiji la yule Mfalme mkuu,” na katika maeneo yaliyokuwa karibu na jiji hilo. (Mt 5:35) Unaweza kuona maeneo yaliyokuwa karibu na Yerusalemu ambayo umesoma katika vitabu vya Injili, kama vile Emau, Bethania, Bethfage, na Bethlehemu.—Lu 2:4; 19:29; 24:13; ona “Eneo la Yerusalemu,” ramani ndogo kwenye ukurasa wa 18.
[Ramani katika ukurasa wa 29]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Nchi ya Ahadi (Siku za Yesu)
Maeneo Katika Siku Za Yesu
Majiji ya Dekapoli
E5 Hipo
E6 Pela
E6 Sikithopoli
F5 Gadara
F7 Gerasa
G5 Dion
G9 Filadelfia
H1 Damasko
H4 Raphana
I5 Kanatha
Barabara Kuu (Ona kichapo)
Njia ya Kawaida Kati ya Galilaya na Yerusalemu (Ona kichapo)
Njia Nyingine Kati ya Galilaya na Yerusalemu, Kupitia Perea (Ona kichapo)
A11 Gaza
B6 Kaisaria
B8 Yopa
B9 Lida
B12 Beeri-sheba
C4 Tolemai
C8 SAMARIA
C8 Antipatrisi
C8 Arimathea
C9 Emau
C10 YUDEA
C11 Hebroni
C12 IDUMEA
D1 Sidoni
D2 Tiro
D3 FOINIKE
D4 GALILAYA
D4 Kana
D5 Sefori
D5 Nazareti
D5 Naini
D7 Samaria
D7 Sikari
D9 Ephraimu
D9 Bethfage
D9 Yerusalemu
D9 Bethania
D10 Bethlehemu
D10 Herodiumu
D10 NYIKA YA YUDA
D12 Masada
E4 Korazini
E4 Bethsaida
E4 Kapernaumu
E4 Magadani
E5 Tiberiasi
E5 Hipo
E6 Bethania? (ng’ambo ya Yordani)
E6 Sikithopoli
E6 Pela
E6 Salimu
E6 Ainoni
E9 Yeriko
F1 ABILENE
F2 Kaisaria Filipi
F4 Gamala
F5 Abila?
F5 Gadara
F7 PEREA
F7 Gerasa
G3 ITURUAEA
G5 Dioni
G6 DEKAPOLISI
G9 Filadelfia
H1 Damasko
H3 TRAKONITISI
H4 Raphana
H12 ARIABIA
I5 Kanatha
[Milima]
D7 Ml. Ebali
D7 Ml. Gerizimu
F2 Ml. Hermoni
[Bahari na Ziwa]
B6 Bahari ya Mediterania (Bahari Kuu)
E4 Bahari ya Galilaya
E10 Bahari ya Chumvi
[Mito]
E7 Yordani Mto
[Chemchemi na Visima]
D7 Jacob’s Fountain
[Picha katika ukurasa wa 28]
Bahari ya Galilaya. Kapernaumu liko upande wa mbele kushoto. Nchi Tambarare ya Genesareti iko upande wa kusini-magharibi mwa picha hii
[Picha katika ukurasa wa 28]
Wasamaria waliabudu kwenye Mlima Gerizimu. Mlima Ebali uko nyuma yake