Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • yp2 uku. 287
  • Mfano wa Kuigwa—Asafu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mfano wa Kuigwa—Asafu
  • Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
  • Habari Zinazolingana
  • Ufanisi Waweza Kutahini Imani Yako
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Kuvumilia Udhalimu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • Jinsi ya Kukabiliana na Kuvunjika Moyo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Kulindwa na Imani na Tumaini
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
Pata Habari Zaidi
Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
yp2 uku. 287

Mfano wa Kuigwa—Asafu

Asafu yuko katika njia panda. Kila mahali anaona watu wanaovunja sheria za Mungu nao hawapatwi na lolote baya! Kwa hiyo, Asafu anaanza kujiuliza ikiwa kuna faida yoyote ya kujitahidi kumpendeza Mungu. Anasema: “Hakika nimeusafisha moyo wangu bure na kuiosha mikono yangu katika kutokuwa na hatia.” Hata hivyo, baada ya kufikiria kwa uzito jambo hilo, Asafu anabadili maoni yake. Anatambua kwamba furaha ya waovu ni ya muda tu. Asafu anakata kauli gani? “Isipokuwa wewe,” amwambia Yehova katika wimbo, “sina mapendezi mengine duniani.”—Zaburi 73:3, 13, 16, 25, 27.

Huenda nyakati nyingine wewe hujiuliza ikiwa kuna faida ya kuishi kulingana na viwango vya Mungu. Lakini uwe kama Asafu, na uchunguze mambo kindani. Fikiria hali ya wale ambao wamepuuza sheria za Yehova. Je, kweli wana amani? Je, wamegundua siri ya kupata furaha, siri ambayo wale walio waaminifu kwa Mungu wamekosa? Baada ya kufikiria mambo kikamili, bila shaka wewe pia utachochewa kusema kama alivyosema Asafu: “Kumkaribia Mungu ni kwema kwangu.”—Zaburi 73:28.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki